Bingwa Wa Dunia Wa Masumbwi Crawford Kuitangaza Serengeti Kimataifa

Bingwa Wa Dunia Wa Masumbwi Crawford Kuitangaza Serengeti Kimataifa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
BINGWA WA DUNIA WA MASUMBWI CRAWFORD KUITANGAZA SERENGETI KIMATAIFAKatika muendelezo wa kuitanga.jpg

BINGWA WA DUNIA WA MASUMBWI CRAWFORD KUITANGAZA SERENGETI KIMATAIFAKatika muendelezo wa kuitan...jpg
Katika muendelezo wa kuitangaza Tanzania duniani kupitia utalii wa michezo, leo Mei 28, 2026, bingwa wa masumbwi duniani, Terence “Bud” Crawford, amekabidhiwa rasmi ubalozi wa utalii baada ya kukutana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Ashatu Kijaji. Tukio hilo limefanyika ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ikiwa ni siku ya tano ya ziara yake nchini.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Dkt. Kijaji alisema Serikali ya Tanzania chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuifungua na kuitangaza sekta ya utalii kimataifa kupitia kampeni mbalimbali ikiwemo filamu za “Tanzania: The Royal Tour” na “Amazing Tanzania” ambazo zimeendelea kuvutia wageni na watu mashuhuri kutoka mataifa mbalimbali kutembelea Tanzania.

“Michezo ni sehemu muhimu ya ajira na maendeleo ya uchumi, lakini pia imekuwa daraja la kuunganisha Tanzania na watu mashuhuri duniani. Kupitia michezo tunaendelea kuitangaza Tanzania kimataifa na kufungua fursa mpya za utalii, uwekezaji na ajira kwa vijana,” amesema Waziri Kijaji.
BINGWA WA DUNIA WA MASUMBWI CRAWFORD KUITANGAZA SERENGETI KIMATAIFAKatika muendelezo wa kuitan...jpg

BINGWA WA DUNIA WA MASUMBWI CRAWFORD KUITANGAZA SERENGETI KIMATAIFAKatika muendelezo wa kuitan...jpg
Aidha, Waziri Kijaji amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kupokea watu mashuhuri kutoka mataifa mbalimbali watakaotembelea vivutio vya utalii nchini, hatua itakayoongeza thamani ya utalii wa Tanzania katika soko la kimataifa. Pia amemkabidhi Crawford cheti cha kutambua mchango wake na kumpa ubalozi wa kuvitangaza vivutio vya utalii vya Tanzania.

Kwa upande wake, Crawford amepongeza ukarimu wa Watanzania pamoja na uzuri wa vivutio vya asili alivyovitembelea katika Hifadhi za Taifa Tarangire na Serengeti tangu kuwasili kwake nchini Mei 24, 2026, huku akiahidi kuwa balozi mzuri wa utalii wa Tanzania.
BINGWA WA DUNIA WA MASUMBWI CRAWFORD KUITANGAZA SERENGETI KIMATAIFAKatika muendelezo wa kuitan...jpg

BINGWA WA DUNIA WA MASUMBWI CRAWFORD KUITANGAZA SERENGETI KIMATAIFAKatika muendelezo wa kuitan...jpg
Naye, Kamishna wa Uhifadhi, CPA Musa Nassoro Kuji amesema utalii wa michezo unaendelea kuongeza sifa za vivutio vya utalii nchini na kuchangia kukuza pato la Taifa.

Akiwa Serengeti, Crawford atashiriki shughuli mbalimbali za kitalii ikiwemo utalii wa puto, utalii wa gari na utalii wa usiku, shughuli hizi zitakazosaidia kuitangaza hifadhi hiyo kimataifa.
 
Back
Top Bottom