Bingwa wa UEFA msimu huu anaweza kuwa Liverpool au Bayern Munchen

Bingwa wa UEFA msimu huu anaweza kuwa Liverpool au Bayern Munchen

changaule

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2020
Posts
6,039
Reaction score
10,151
Kwa michezo kadhaa niliyofuatilia msimu huu, naona bingwa wa msimu huu atakuwa kati ya Bayern Munich au Liverpool.

Kwa upande wa Liverpool itategemea endapo hatakutanishwa na waingereza wenzie maana anaweza kumsumbua kwavile wanajuana.

Update:

Thread closed, Real Madrid bingwa wa UEFA champions league 2021/2022
Tukutane msimu mpya wa 2022/2023.
 
Huu ni utabiri ama?

Nakupa hii hebu waangalie Chelsea wanavocheza alafu njoo tena ufanye utabiri wako.
Chelsea maji kupwa, maji kujaa bado hawajanishawishi. Ni moja ya timu iliyokuwa kwenye kundi jepesi mno lakini pamoja na kuwa katika kundi jepesi, unaona mechi dhidi ya zenit anavyopata tabu kupata ushindi. Unaona mechi ya marudiano dhidi ya kibonde Malmo mnavyopata ushindi mwembamba. Jana imemfunga Juventus iliyobakia jina tu haina ubora wowote na ndio maana kwenye ligi wanashika nafasi ya nane.
 
Ukiongelea hivo inamaana hao Liverpool na Bayern wana 100% ya ushindi katika ligi zao mpaka sasa?

Ina maana Liverpool na Bayern wao hawapati shida kushinda mechi ?

Punguza ushabiki anza kuangalia mpira kivingine.Msimu ulopita mliongea mengi lakini mwisho mliaibika hivihivi.
 
Back
Top Bottom