BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Maisha ni safari ndefu, kuna milima na mabonde. Ndivyo unavyoweza kumwelezea Lightness Shirima, ambaye amepitia changamoto nyingi za maisha katika umri mdogo.
Katika kuhakikisha anatimiza ndoto zake za elimu, Lightness amekuwa akitafuta msaada wa hapa na pale ili kufikia malengo, licha ya kukutana na vikwazo vingi, ikiwemo kuwazika mama na baba yake.
Msichana huyo mwenye miaka 22, amesimulia mambo mbalimbali, ikiwemo kusitisha masomo baada ya kukosa ada na kuamua kufanya kazi ya kuosha magari, lengo likiwa kutimiza ndoto za kupata elimu.
Lightness amesimulia hayo siku chache tangu deni la Sh9 milioni alilokuwa akidaiwa na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili- Mlonganzila kufutwa na Serikali.
Deni hilo lilitokana na gharama za matibabu ya baba yake mzazi, Priscuss Shirima (49) baada ya kulazwa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) kwa muda wa siku 40. Hata hivyo, Julai 4, mwaka huu alifariki dunia.
Lightness ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa pili wa Chuo cha Serikali za Mitaa (LGTI), Hombolo jijini Dodoma anakumbuka kifo cha mama yake mzazi, Gloria Temba kilichotokea 2009 ambapo alimwacha akiwa mdogo yeye pamoja na mdogo wake, Brayton Shirima (16).
Anasema baada ya mama yao kufariki waliendelea kuishi na baba yao na mwaka 2015 alipata shinikizo la damu lililosababisha kupata matatizo ya macho, hali iliyomfanya kushindwa kumudu majukumu, ikiwemo kujitafutia kipato.
Lightness anasema mwaka 2021 alishindwa kuendelea na masomo baada ya kukosa ada, hali ambayo ilimfanya aache chuo kwa mwaka mmoja na kufanya kazi ya kuosha magari ili kukusanya fedha kwa ajili hiyo.
“Hivyo mwaka 2021 nilirudi Moshi kutafuta kibarua cha kuniingizia kipato, nilibahatika kupata kazi ya kuosha magari kwa kuwa nilikuwa sina namna nyingine na nilikuwa ninalipwa Sh120,000 kwa mwezi, niliifanya bila kuona aibu na nilifanikiwa kupata ada na mwaka huu ndio nilirudi chuoni kuendelea na masomo yangu.
“Kwa sasa naendelea na masomo yangu ya mwaka wa pili na ndio hivi naendelea kujiokotea kidogo kidogo hivyo hivyo kwa shida nipate ada ya chuo na ya kujikimu mimi na mdogo wangu maana mimi ndio mtoto wa kwanza na sina ndugu mwingine ambaye nasema anaweza kunisaidia kunisomesha,” anasema.
“Namshukuru Mungu baada ya kusimama mwaka mmoja wa masomo nilifanya kazi kwa muda mfupi na nilipopata fedha nilirudi chuoni.”
Lightness anasema kwa sasa alitakiwa awe amemaliza mwaka wa tatu lakini haikuwa hivyo, baada ya kusimama mwaka mmoja wa masomo kwa kukosa ada ya chuo.
“Pamoja na changamoto hizi ninazopitia naiomba Serikali kama itaweza kunisaidia tena nimalize masomo yangu maana mimi ndio nimebaki mwenyewe, sina baba wala mama na nina mdogo wangu ambaye bado na yeye anahitaji msaada,” anasema Lightness.
Kuhusu malengo yake anasema, “Natamani nifanikiwe kumaliza chuo kusiwe na mikwamo yoyote na pia nijiendeleze na masomo ya elimu ya juu, lengo langu niwe mwanasheria.
“Ndiyo maana ninaomba kama kuna atakayeguswa anisaidie kufikia ndoto zangu kwa sababu ninaamini ni elimu pekee ndiyo itakuja kunikwamua kimaisha iwe kwa kuajiriwa au kujiajiri.”
Source: Mwananchi