The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Binti mmoja wa Nchini Uhispania Noelia (23), amepanda kizimbani kutoa ushahidi Mahakamani ili kumshawishi Hakimu amruhusu kufariki kwa hiyari yake baada ya Baba yake Mzazi kufungua shauri Mahakamani la kupinga Mtoto wake kutaka kujiua kwa hiyari.
Noelia atapanda kuzimbani kujitetea ambapo atatakiwa kutoa sababu ambazo zitamshawishi Hakimu aweze kutupilia mbali pingamizi la Baba yake mzazi alilofungua mara baada ya binti huyo kujaribu kujitoa uhai lakini kushindikana japo uamuzi wa Binti huyo uliungwa mkono na Serikali ya Catalonia nchini Hispania baada ya Bodi ya Euthanasia kutathmini na kuridhia uamuzi wake mwezi Julai mwaka 2024.
Euthanasia ni kitendo cha kukatisha maisha ya Mtu kimakusudi ili kuondoa mateso ambapo inaweza kuwa bila hiyari, kwa mfano ikiwa Mtu yuko katika hali ya kukosa fahamu na hawezi kutoa kibali chake au kwa hiyari kama ilivyo katika kesi hii.
Binti huyo alipaswa kufariki mwezi Agosti 2024 lakini mchakato huo ulisitishwa mara ya mwisho kutokana na pingamizi la kisheria lililowekwa na Baba yake kwa kuungwa mkono na Kikundi cha Kampeni cha Wanasheria wa Kikristo (Abogados Cristianos).
Noelia mwenyewe amenukuliwa akisema maneno yafuatayo “Ninahisi kutoeleweka na familia yangu, najihisi mpweke na mtupu, hali hii inanisababishia mateso makubwa”.
Tangu sheria ya euthanasia ianzishwe Nchini Hispania mwaka 2021, hii ni mara ya kwanza kwa kesi kwenda Mahakamani ili Jaji aamue ambapo mwaka 2024 Hakimu mmoja wa Barcelona alikataa jaribio la Mwanaume mmoja kukata rufaa dhidi ya kifo cha Mwanae mwenye umri wa miaka 54 ambaye uamuzi wake tayari ulishapitishwa na Bodi ya dhamana na tathmini.