Binti Makamba, Lundenga, Miss Tanzania na roho zinazoelea!

Status
Not open for further replies.
Hapo kwenye red nakuunga mkono kwa sehemu kubwa. Shamhuna and His Co. aliishupalia sana SUMATRA iondoke zanzibar.
Lands, Housing, Water and Energy minister Ali Juma Shamhuna

Hawa ndio wanasiasa ambao vitendo vyao havielezeki. Wameitimua SUMATRA Zenj bila kuweka utaratibu unaeleweka kulinda usalama wa wananchi.
Ni vyema wakawajibika kwa vitendo vyao kuhatarisha maisha wa watu masikini kwa sababu za kisiasa.
 

Ndugu usiwe unaaandika kwa kutumia Masaburi, uwe unatumia mikono! Hakuna mtu aliyelaumu vodacom, Binti makamba ama Lundenga kwa kusababisha ajali. Suala la chanzo cha ajali kitabaki pale pale kwamba ni uzembe, na hatua za kuchunguza tayari zimeshachukuliwa ili kujua ukweli na hatua zaidi zichukuliwe!
Kuhusu kuwepo sumatra zanzibar haiwezi kuwa ndio chanzo cha ajali kama akili zako zinavyokutuma iwe hivyo, kwania Sumatra ipo bara na kila siku watanzania tunakufa kwa ajari za barabarani! Mwisho hivi leo huko moro ajali mbaya zimetokea na wtz wamekufa wengi. Mazizi karibu na wami hapa gari nne zimeanguka zikiwa na mizigo kupita kiasi na abiria pia.
Tunachojadili hapa ni kitendo cha kutoonyesha kujali tukio la huzuni kama lile la watz kufariki na wengine wakiwa hawajulikani hatma yao ndani ya bahari, huku watu wengine wakiendelea na shughuli za starehe na urembo. Pia ikumbukwe hakuna mtu aliyeshauri voda ingefunga shughuri za kibiashara ama kuamuru wafanya kazi wapumzike nyumbani wakiomboleza!
 
Tatizo lako hujajua nini kinaongelewa kwanini unachangia sasa?

 
Hujaelewa mada wewe, kinachozungumziwa ukisikia mdogo wako kafa nyumbani wewe utaendelea na harusi?? japo hata usipoendelea na harusi hawezi kufufuka ila ni lazima ukaomboleze na watu wengine kama utamaduni. Sasa umepata akili hapo? na umejiona kuwa IQ yako iko chini sana?


 
Uzalendo hakuna, kila mtu anaangalia maslahi binafsi.
 

Toka lini Vodacom wakawa na uzalendo??? Kulipa kodi kwenyewe wamezidiwa na Chibuku
 

It's not the responsibility of the government to tell the businesses to stop doing business when a disaster strikes! I think you've gone too far
 
It's not the responsibility of the government to tell the businesses to stop doing business when a disaster strikes! I think you've gone too far

.....And what is meant by "Cooperate Social responsibility" you son of fisad.
 
.....And what is meant by "Cooperate Social responsibility" you son of fisad.

How does the tragedy in Zanzibar got anything to do with Vodacom?
Why not blaming the daladalas, taxis, Radio and TV stations, FAT, Yanga, night clubs and bar owners, for not stopping their operations on that day of tragedy? It was business as usual for every kind of business/activity. So why is it a big deal for Vodacom to do what they were supposed to do?
 
Mimi naona haya malumbano hayasaidii chochote zaidi ya watu kuonyeshana nani anajua kuandika zaidi ya mwingine hapa! cha msingi ni tuomboleze kwa haya masaibu yaliyotukuta watanzania lakini tukianza kulaumu tutakujagusa hata waliokuwa igunga kuwa kwanini hawakusitisha kampeini ili kuungana na wafiwa kuomboleza?!
Mungu azilaze roho za marehemu woote pema peponi.
 

Hapo nafikiri ni uchochezi na siyo ushauri. Lundenga ndiyo anatakiwa kuomba radhi na tayari ameshafanya hivyo, sasa hao vodacom wanaingiaje? kama ni kudhamini walishadhamini siku nyingi hata kabla ya hiyo siku.

Afterall siyo waliosababisha ni tamaa na watu wachache wanopenda kucheza na roho za watu.

Mungu walaze mahalai pema peponi. AMEN
 

WRONG+WRONG=RIGHT.....Isnt it?
 
Lundenga alifuata kitu kimoja ya kwamba kukatokea mtu kafariki na kulikuwa na sherehe ya ndoa basi shughuli inaendelea kwanza baaada ya hapo kuzika,
 
Its my masaburi against your infertile masaburi.Na kama masaburi yako yangefaa chochote ungetumia muda huu kutafuta maiti za wahanga wa ajali zilizotapakaa pwani yote ya Afrika Mashariki,na kuyafuta chanzo cha ajali pamoja na mapungufu katika usimamizi na udhibiti wa udafori majini hulo Zenj.Tatizo nyie wenzetu mmezoea kulalama ,kulaumu na kukunja mikono vifuani mkitegemea vya mjomba. Hili tatizo its your stupid baby.Mmejitengenezea tatizo la kijinga na mnataka wote tuhusike.Hasa baada ya kuwafukuza SUMATRA huko Zenj,sasa zaodi ya kuwahurumia mwatala nini tena?Haya si mliyataka?Kuhusika kwangu mimi ni kuwahurumia wananchi wasio na hatia walioingizqa mkenge kwa matakwa ya kisiasa ya watu kama ninyi.Ati Zanzibar ni Nchi.Hamuwezi hata kuendesha usafiri endelevu na ulio salama. Ndo maana naona ni ujinga na unafiki uliokithiri kuilaumu Vodacom wakati marehemu wanaelea mpaka Mombasa.Waambieni basi Voda wakaopoe maiti huko Lamu kama mmeshindwa. Hii ndio athari ya mtoto kulilia wembe, mmeupata.
 
Hawa ni wenye hulka za kishabiki na hawajui mustakabali wao kama wananchi katika nchi huru yenye kufuata shria ,kanuni na taratibu hivyo hata uwaelimishe mpaka asubuhi watakuwa washabiki wa haya makampuni ya kigeni yasiyowathamini watanzania kwa sababu kuna mjomba wake pale ni Dereva.
 
Kuna watu wajinga wajinga wanaifuatilia Voda baada ya ajaili wakitolea hasira zao za ajali ya boti utafikiri Voda ndo walisababisha ajalai ile.
Voda wakiendlea kula bata wakati wengine wanalia ni utashi wao na biashara zao.
Wanaotakiwa kuwajibika ni viongozi pale Zanzibar waliosbabisha ajali ile.
Tukumbuke hili la kusimamia meli Nchi Zanzibar ni la kwenu huko huko Zanzibar.
Mkosefu mnaye , mtafuteni na mumnyonge.
Hapa hakuna cha uzalendo wala Muungano, ni kesi ya jinai tu na kama mko wakweli msingojee tume za uongo na kweli.
Anyongwe mtu kwa kuua watu zaidi ta 1000.
 

Kuna hoja nzito sana hapo.
Muungano wetu unaenda umbali gani ni swala la msingi sana,isije kuwa misiba si sehemu ya mambo ya muungano kama ilivyo Miss Tanzania nayo sio swala la Muungano,Hapa kweli swala lilikuwa ni la ujirani zaidi kuliko undugu. Kama kweli SUMATRA hawawezi kusimiamia usafiri hadi Unguja basi hii ajali ni ya kwao pekee yao sisi ni majirani tu ambao hatuwezi kuahirisha ratiba zetu labda siku ya mazishi,kwa mantiki hiyo kelele zote hizi na hata Hoja ya Zitto Kabwe haikuwa na maana kwa kuwa swala husika si la muungano.
Kwamba linatuhusu haina ubishi kwab sababu ya ujirani,kuna haja sasa kupitia msiba huu tuangalie nini faida za Muungano,Kwa kuwa swala la kuzama kwa mweli haliwezi kuwa la muungano kwa sababu taasisi inayoshughulikia usalama wa vyombo vya majini si ya kimuungano,Ingekuwa ni vigumu kwa bara kuchukua jukumu lolote katika kadhia hii bila idhini ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Haya ni moja ya mambo ambayo yaweza kuwa chachu ya kuangalia umuhimu wa Muungano na namna bora ya kuimarisha Muungano wetu...
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…