Binti wa aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amekamatwa na kufunguliwa mashtaka ya ugaidi

Binti wa aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amekamatwa na kufunguliwa mashtaka ya ugaidi

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Binti wa aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amekamatwa na kufunguliwa mashtaka ya ugaidi.

Mbunge wa Afrika Kusini Duduzile Zuma-Sambudla ameshutumiwa kwa kuchochea ghasia na mauaji katika ghasia za Julai 2021 zilizoua zaidi ya watu 350.

Zuma-Sambulida alifika ana kwa ana mbele ya Polisi leo. Ameshtakiwa kwa ugaidi pamoja na uchochezi wa ghasia na mauaji.

Chama cha Zuma-Sambulida, ANC, kilithibitisha kwamba alipangwa kufika mahakamani siku ya leo. Kesi yake inatokana na ujumbe alizochapisha kwenye mtandao wa X zamani Twitter.

Anadaiwa kuwachochea waandamanaji, kuwahimiza kuharibu na kuvunja mali katika machafuko ya nchi nzima.

Mzozo huo ulianza baada ya babake Jacob Zuma kufungwa jela.
 
Back
Top Bottom