Binti wa Dkt. Wilbert Kleruu atoa ya moyoni

EMT

Platinum Member
Joined
Jan 13, 2010
Posts
14,477
Reaction score
15,325
Mnara.jpg

"Ni vigumu, kuvumilia hali hii, bali naamini haya ni matokeo na ni mipango ya Mungu kuifanya hali hii, baba yetu alikuwa ni muumini wa Ujamaa na Kujitegemea aliyesimamia sera za Ujamaa na kujitegemea kama ilivyokuwa kwa wakati ule enzi za Mwalimu Nyerere."

"Serikali ilikuwa inahimiza vijiji vya Ujamaa, ili wananchi washiriki kwa pamoja kwenye Kilimo cha Kufa na Kupona, baba alifuatilia kwa kina maagizo ya Mwalimu, inawezekana hili ndilo lililosababisha kuuawa akiamini alichosimamia kilikuwa sahihi,''anasema Eva Wilbert Kleruu huku akibubujikwa na machozi.

Picture+029.jpg

Eva Kleruu akifuta machozi baada ya kukumbuka jambo juu ya mauaji ya baba yake miaka 43 iliyopita.

"Samahani umenikumbusha mbali sana miaka 43 sasa baada ya kifo cha baba yangu, nilikuwa bado binti mdogo miaka ile ya mwanzo ya miaka ya 70, baba alikuwa ni mfuasi wa Ujamaa na Kujitegemea na alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa aliyeagizwa kusimamia siasa ya Ujamaa na Kujitegemea,''anasema.

Anasema ni hali ambayo imekuwa ngumu kuisahau kutokana na aina ya tukio lenyewe lilivyojiri na kwamba ingekuwa kifo kile kilitokana na ugonjwa jambo hilo lingezoeleka kwa haraka, bali hata hivyo anaamini kilichotendeka kilitokana na uelewa mdogo juu ya mpango wa serikali kuimarisha vijiji vya Ujamaa na kujitegemea.

Anafafanua kuwa anaamini kifo cha baba yake kilikuwa ni sawa na kujitolea mhanga katika harakati za Ujamaa na Kujitegemea kwani baba yake alikuwa ni miongoni mwa waumini wa Ujamaa ambao walisimamia na kuamini kuwa siku moja nchi inaweza kujitegemea kwa sera ya ujamaa na Kujitegemea.

Anasema serikali wakati ule ilisimamia mpango kwa nia ya kuboresha huduma za wananchi wka pamoja na kuondoa ukiritimba wa ubepari kwa mtu mmoja kuhodhi eneo kubwa la ardhi jambo ambalo baadhi ya watu wasioenda maendeleo walikuwa wakilipinga.

Aidha anasema hata hivyo anayofursa ya kuishukuru serikali kwa kuwajali na kuwasomesha kwa ngazi ya juu ya elimu ambapo yeye alisoma hadi nchini Burgaria na mdogo wake alipelekwa nchini Urusi katika nchi zilezile zilizokuwa zinaamini siasa ya Ujamaa na Kujitegemea.

Anasema pamoja na tukio hilo kukatisha mapenzi baina ya baba na familia yake kwa kukatishwa maisha kikatili serikali ilikuwa bega kwa bega na familia ya marehemu Dkt Kleruu kwa hali na mali ambapo Mwalimu Julius Nyerere, Mzee Abeid Karume ambapo kwa bahati mbaya mzee Karume aliuawa akiwa katika harakati za kuendelea kuienzi familia hiyo.

"Mzee Karume alikuwa upande wetu sana alijitahidi kwa hali na mali kuhakikisha tunaishi kwa upendo, amani na utulivu, lakini bahati mbaya naye aliuawa mwaka uliofuatwa kwa risasi,'' anazungumza Eva huku akibubujikwa na machozi.

Anasema hata mrithi wa Marehemu Karume Mzee Aboud Jumbe naye aliendeleza mahusiano ya kuijali familia yetu ambapo pia Mzee Rashid Kawawa na Mama Getrude Mongela nao walikuwa mstari wa mbele katika kutufariji.
"Mama yetu bado yupo hai amestaafu alikuwa akifanya kazi katika ofisi ya Mkuu wa mkoa, baada ya kutoka Iringa kufuatia mauaji yale tulirudi Moshi, tukaendelea kusomeshwa na serikali Mzee Karume alikuwa mstari wa mbele kutusaidia.

Picture+036.jpg

'Mama yetu kwa sasa anaishi Moshi, niko na wadogo zangu, watatu, mmoja anaitwa Andrew, mwingine Carmen ambaye ni Bibi Afya na Edwin ambaye ni mjasiriamali wote tulisomeshwa kwa ngazi za juu, tunaishukuru serikali kwa kutujali,'' anabainisha.

Kadhalika anasema kuwa katika kuendelea kujisahaulisha tukio lile la kikatili lililofanywa dhidi ya baba yake amepanga kukutana na familia ya marehemu Mwamwindi ambaye ndiye aliyemuua baba yake, ili wazungumze na kuanzisha ukurasa mpya wa maisha.

"Unajua visasi vinarithishwa kimaumbile, bila kukutana na familia ile vizazi vyetu vinaweza kujikuta vikiingia katika dhambi isiyotarajiwa, napenda nikutane na mtoto mkubwa wa Mzee Mwamwindi, ili tufungue ukurasa mpya wa maisha, hatujawahi kukutana hata mara moja wala hatujuani,'' anasema Eva.

Anasema nia ya kukutana naye ni kuanzisha uhusiano mpya ambao ulitoweka kwa zaidi ya miaka 40 huku viongozi wa wakati huo Mwalimu Nyerere, na Mzee Karume nao wakiwa wametangulia mbele ya haki hivyo anaamini kwa kukutana na wanafamilia hao utaanzishwa uhusiano chanya wenye lengo la kudumisha amani na utulivu.

"Sifikirii wala sijawahi kufikiria kulipiza kisasi, tulikaa kama familia tukamuomba Mungu atulinde na vitendo vya kishetani, tunaamini Mungu anaendelea kutulinda na kilichotokea kilikuwa ni dhamira iliyosukumwa na vitendo vya kishetani,'' anasema Eva.

Chanzo: BINTI WA DKT WILBERT KLERUU ATOA YA MOYONI, WALIOMUUA BABA YAKE MKOANI IRINGA MIAKA 43 ILIYOPITA ~ FASIHI MEDIA INC. 'Mwanafasihi Mahiri'

Habari zaidi, soma;

Mkuu wa Mkoa wa iringa Dr. Kleruu alidhani kila mtu ni mkristo kwa kumlazimisha Mzee Saidi mwamwindi aache kulima ili asherehekee Krismas matokeo yake ndiyo hayo! mauaji dhidi ya binaadamu wenzetu hayakubaliki! lakini kutumia mamlaka uliyopewa na wananchi kuwadhalilisha raia zako pia haikubaliki!

Uamuzi wa binti wa Dr. Kleruu kutaka kujenga mahusiano na familia ya Marehemu Saidi Mwamwindi ni uamuzi wa busara ambao kila mpenda amani atayakaribisha! ila kifo cha Kleruu ni fundisho kwa kila dikteta na kiongozi anaeongoza kimabavu!

Kisa kizima cha mauaji ya Dr. Kleruu gonga hapa: Raia Mwema - Kwa nini mkulima Mwamwindi alimpiga risasi RC Dk. Kleruu? VII
 
Mkuu wa Mkoa wa iringa Dr. Kleruu alidhani kila mtu ni mkristo kwa kumlazimisha Mzee Saidi mwamwindi aache kulima ili asherehekee Krismas matokeo yake ndiyo hayo! mauaji dhidi ya binaadamu wenzetu hayakubaliki! lakini kutumia mamlaka uliyopewa na wananchi kuwadhalilisha raia zako pia haikubaliki!
Uamuzi wa binti wa dr. Kleruu kutaka kujenga mahusiano na familia ya Marehemu Saidi Mwamwindi ni uamuzi wa busara ambao kila mpenda amani atayakaribisha! ila kifo cha Kleruu ni fundisho kwa kila dikteta na kiongozi anaeongoza kimabavu!

kumbe alikuwa DIKTETA ? Basi ALIVUNA ALICHOPANDA .
 
it was very poor judgement kwa upande wa mzee mohamed kwani hata kama alifanya hivyo death penalty was not appropriate. i beleive yeye alipewa full access to the court of law and receive fair justice.
 
Mkuu wa Mkoa wa iringa Dr. Kleruu alidhani kila mtu ni mkristo kwa kumlazimisha Mzee Saidi mwamwindi aache kulima ili asherehekee Krismas matokeo yake ndiyo hayo! mauaji dhidi ya binaadamu wenzetu hayakubaliki! lakini kutumia mamlaka uliyopewa na wananchi kuwadhalilisha raia zako pia haikubaliki!
Uamuzi wa binti wa dr. Kleruu kutaka kujenga mahusiano na familia ya Marehemu Saidi Mwamwindi ni uamuzi wa busara ambao kila mpenda amani atayakaribisha! ila kifo cha Kleruu ni fundisho kwa kila dikteta na kiongozi anaeongoza kimabavu!

Kisa kizima cha mauaji ya Dr. Kleruu gonga hapa: Raia Mwema - Kwa nini mkulima Mwamwindi alimpiga risasi RC Dk. Kleruu? VII

Kwa nini Dr. Kleruu awalazimishe watu kusherekea Krismasi, wakati siku ile ile ya Krismasi yeye mwenyewe alishiriki kupanda mahindi kwenye shamba la ushirika?.

Akili za kuambiwa changanya na zako, hata huyo Mjengwa uliyemuweka kama reference anakiri kuwa hiyo story ya kuwa Kleruu alimlazimisha Mzee Saidi mwamwindi aache kulima ili asherehekee Krismas hana uhakika nayo (anasema inahitaji utafiti zaidi).
 
Huyu binti hajui lolote kuhusu tabia mbaya za Marehemu Baba Yake,pole sana binti lakini napenda kukushauri kuachana
Na jambo hili endelea tu kumuombea Mungu Baba Yako mungu amsamehe kwa yote aliyotenda hapa Duniani
Ni toa mfano Akiwa Mkuu wa mkoa Mtwara alishiriki na kufanikiwa njama ambazo Ndugu Yetu alihukumiwa miaka zaidi ya mitatu

Kwenda jela na kuchapwa viboko kwa mambo ya kusingiziwa kisa mwanamke moja wa hapo mjini Mtwara
Sasa sisi ndugu tuliomba mungu sana lakini mambo haya Kuwa rahisi pamoja na rufaa bado kleruu aliweka mkono wake hukumu

Ile ikabaki pale pale tukakata rufaa tena hukumu ikabaki pale pale mwisho kwa uwezo wa mungu na juhudi kubwa katika Mahakama ya Africa Mashariki ndiyo jamaa Yetu akatoka na Kuwa Huru sasa wewe unalilia nini sisi tulilia sana maana ndugu

Yetu alikuwa ndiyo jembe pekee kwanye familia Yetu kisa Mwanamke looo Aibuu Mkuu wa Mkoa unagombea mwanamke
Basi tulifanya Dua kubwa sana Kama kawaida malipo ni hapa hapa Duniani
Asalaam alykuum
 
kleruu amevuna matokeo ya siasa za Ujamaa na Kujitegemea
 
EMT As a free marketeer, I believe that the government and people who serve in the government shouldn't intefere with means of productions and people's lives. I am sorry to say Dr. Kleruu got what deserved.
 
Last edited by a moderator:
Asante JF nimeweza Kumjua Kleruuu, Nasijiaga KLERUU TTC Binge La Chuo pale Iringa Kumbe ni Huyu Mzee, Atleast i've learnt something",, R.I.P Mzeee, Pole Binti Ni Lazima Usamehe!
 
Hivi kwa nini usijadili hoja bila kuingiza udini?

Mkuu wa Mkoa wa iringa Dr. Kleruu alidhani kila mtu ni mkristo kwa kumlazimisha Mzee Saidi mwamwindi aache kulima ili asherehekee Krismas matokeo yake ndiyo hayo! mauaji dhidi ya binaadamu wenzetu hayakubaliki! lakini kutumia mamlaka uliyopewa na wananchi kuwadhalilisha raia zako pia haikubaliki!
Uamuzi wa binti wa dr. Kleruu kutaka kujenga mahusiano na familia ya Marehemu Saidi Mwamwindi ni uamuzi wa busara ambao kila mpenda amani atayakaribisha! ila kifo cha Kleruu ni fundisho kwa kila dikteta na kiongozi anaeongoza kimabavu!

Kisa kizima cha mauaji ya Dr. Kleruu gonga hapa: Raia Mwema - Kwa nini mkulima Mwamwindi alimpiga risasi RC Dk. Kleruu? VII
 
Asante JF nimeweza
Kumjua Kleruuu, Nasijiaga KLERUU TTC Binge La Chuo pale Iringa Kumbe ni
Huyu Mzee, Atleast i've learnt something",, R.I.P Mzeee, Pole Binti Ni
Lazima Usamehe!

Kleruu TTC ni miongoni mwa vyuo bora kabisa vya waalimu wa sayansi kuwahi kujengwa.ilikuwa mwaka wa 1970 msaada toka Denmark
 
Nimerudi tena jamvini ukweli utabaki Kuwa ukweli hamna ujamaa kuhusiana na kifo cha Dr kleruu

Kwanza mzingira ya kumfuata mtu shambani kwake sikuu ya Christmas kwa jambo la kiserikali na bila ulinzi Kama Mkuu wa mkoa tayari huo ni ubabe wa viongozi wengi katika nchi hii soma makala nyingi sasa utakuta maneno ya viongozi wengi kwamba wamekata tamaa ya kuongoza watu kauli za wapigwe tu, nao wauwawe , hakuna sababu ya Mimi kujiudhuru vyote hivi ni kauli za kejeli wana pambana nazo wananchi masikini wa vjijijini kila siku kwa hiyo yaliotokea Ismani Kitabu au muandishi asifiche ukweli

Aweke wazi kila kitu mpaka mahakamani hukumu ilikuwaje na mwisho ilikuwaje mwamindi alinyongwa au je ,je hapo ndiyo watanzania tutajua pumba na mchele

Wasi wasi wangu huyu Muandishi sijuii Kama hili jambo ataweza sijuii kweli miaka 40 kueleza ukweli kwa Tanzania sijuii
Na haijawahi kutokea mungu mpe Nguvu na busara muandshi huyu tuone kalamu yake kwenye Kitabu hiki
Asante
 
''Mama yetu kwa sasa anaishi Moshi, niko na wadogo zangu, watatu, mmoja anaitwa Andrew, mwingine Carmen ambaye ni Bibi Afya na Edwin ambaye ni mjasiriamali wote tulisomeshwa kwa ngazi za juu, tunaishukuru serikali kwa kutujali,'' anabainisha.
Mkuu EMT, kwanza asante kwa hii kitu!, mimi ni interested party nilisoma darasa moja na mtoto wa Kleruu aitwae Edwin pale Ilboru!.
Jamaa was humble and down to earth!.

Mwamwindi na mhindi mmoja ndie watu pekee Nyerere alisaini death warrants zao za Capital punishment kutekelezwa, nasikia katika utekelezaji ilisumbua, baada ya kunyogwa mara ya kwanza, hakunyongeka na kufa, then ilibidi kitu fulani kifanyike ndipo alikufa, mtu akishahukumiwa kunyongwa, ukinyongwa bila kufa unapaswa kuachiliwa, maana utekelezaji wa adhabu ilikuwa ni "kunyongwa"

Nasikia ikatolewa order, sio tuu anyongwe, bali ni "anyongwe mpaka afe!", from then hukumu ya kunyongwa inapaswa kuandika "Anyongwe Mpaka Afe!"

Kiukweli hukumu hii ni "barbaric!" thanks God, we'll do away kwenye katiba mpya!, japo kwenye rasimu bado ipo!.
Pasco.
 
Nadhani wewe hujaipata vyema historia yake, sababu ya kifo chake hayahusiani na ukristo wal uislamu, tafuta usome vizuri na uelewe

Mkuu wa Mkoa wa iringa Dr. Kleruu alidhani kila mtu ni mkristo kwa kumlazimisha Mzee Saidi mwamwindi aache kulima ili asherehekee Krismas matokeo yake ndiyo hayo! mauaji dhidi ya binaadamu wenzetu hayakubaliki! lakini kutumia mamlaka uliyopewa na wananchi kuwadhalilisha raia zako pia haikubaliki!
Uamuzi wa binti wa dr. Kleruu kutaka kujenga mahusiano na familia ya Marehemu Saidi Mwamwindi ni uamuzi wa busara ambao kila mpenda amani atayakaribisha! ila kifo cha Kleruu ni fundisho kwa kila dikteta na kiongozi anaeongoza kimabavu!

Kisa kizima cha mauaji ya Dr. Kleruu gonga hapa: Raia Mwema - Kwa nini mkulima Mwamwindi alimpiga risasi RC Dk. Kleruu? VII
 
Hii sotry sio ya kweli, tafuteni sababu hasa na mfahamu kilichotokea

Kwa nini Dr. Kleruu awalazimishe watu kusherekea Krismasi, wakati siku ile ile ya Krismasi yeye mwenyewe alishiriki kupanda mahindi kwenye shamba la ushirika?.

Akili za kuambiwa changanya na zako, hata huyo Mjengwa uliyemuweka kama reference anakiri kuwa hiyo story ya kuwa Kleruu alimlazimisha Mzee Saidi mwamwindi aache kulima ili asherehekee Krismas hana uhakika nayo (anasema inahitaji utafiti zaidi).
 
Huyu binti hajui lolote kuhusu tabia mbaya za Marehemu Baba Yake,pole sana binti lakini napenda kukushauri kuachana
Na jambo hili endelea tu kumuombea Mungu Baba Yako mungu amsamehe kwa yote aliyotenda hapa Duniani
Ni toa mfano Akiwa Mkuu wa mkoa Mtwara alishiriki na kufanikiwa njama ambazo Ndugu Yetu alihukumiwa miaka zaidi ya mitatu
Kwenda jela na kuchapwa viboko kwa mambo ya kusingiziwa kisa mwanamke moja wa hapo mjini Mtwara
Sasa sisi ndugu tuliomba mungu sana lakini mambo haya Kuwa rahisi pamoja na rufaa bado kleruu aliweka mkono wake hukumu
Ile ikabaki pale pale tukakata rufaa tena hukumu ikabaki pale pale mwisho kwa uwezo wa mungu na juhudi kubwa katika Mahakama ya Africa Mashariki ndiyo jamaa Yetu akatoka na Kuwa Huru sasa wewe unalilia nini sisi tulilia sana maana ndugu
Yetu alikuwa ndiyo jembe pekee kwanye familia Yetu kisa Mwanamke looo Aibuu Mkuu wa Mkoa unagombea mwanamke
Basi tulifanya Dua kubwa sana Kama kawaida malipo ni hapa hapa Duniani
Asalaam alykuum

Mhhhh haya sikuyajua na kama kweli ni hivyo basi malipo ni hapahapa duniani
 
wazee wa iringa wamenieleza kuwa kleruu alikuwa katiri sana. alithubutu kuchapa viboko wakulima. wanamuona mwamwindi kama MTU aliyekuwa shujaa. lakini kesi yake ilizungukwa na maluweluwe mahakama haikuzingatia Defance ya provocation ili Ku reduce punishment. mwamwindi alinyongwa dodoma
 
Kleruu alikuwa dikteta kama Nyerere, huwezi mlazimisha mtu afuate imani yako na hii tabia Nyerere alikuwa nayo sana hata hukumu ya kunyongwa ni shinikizo la Nyerere.
 
Back
Top Bottom