Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndio mjadili yote hayo ya idadi ya wanaume aliokuwa nao binti yako wa kazi?!! Halafu umesema anakuita kaka, kaka gani ww huogopeki unatajiwa had madanga ya mdogo wako?!Ni watu ambao tunasalimiana Kila siku napita hapo kwao.
Kala mmojawapo hapo 🤣🤣🤣Ngoja atoke kudai madeni yake ya kausha damu😂😂😂ana kampuni ya kutoa mikopo kwa riba katili
Shomile 🤣🤣🤣Huyu mwamba ana chembe chembe za kihaya
Ila wewe haumo humo?Nimesikitishwa sana na kilichotokea home, binti huyu WA KAZI nimepewa huko mbali na wakwe zangu ametoka karibia km 900 kufika ninapoishi !
Ni binti mstaarabu mpole mcheshi sana kiufupi nilisema hapa nimepata dada WA KAZI na Mimi nlikuwa nimemjumuisha kwenye familia na sikumchukulia kama mfanyakazi WA ndani.
Hata MTAANI hawakujua kama ni mfanyakazi maana alikuwa anapendeza vyakutosha na hakuna kazi nyingi anazofanya.
Mimi huwa natoka asubuhi narudi jioni kasoro siku za weekend Huwa nakuwa sana MTAANI, kuangalia Mpira WA Uingireza na kucheza bao.
Kiufupi hapa MTAANI hata nikigombea urais WA mtaa napita bila kupingwa na maarufu haswa kutokana na aina ya kazi ninayofanya.
Sasa siku nipo job wife anapiga simu anasema huyu mtoto amechoka kazi fanya aondoke, mimi sipendi kuongea kitu kimoja Kila mara.!
Kumuuliza wife kwani shida nini?? Anasema nimemwambia afue ye anahangaika tu huko MTAANI hajaja kufua mpaka sasa. Nikamwambia wacha nirudi.
Jion kumuuliza vipi mbona kama una ukaidi kulikoni anasema mimi nataka kwenda nyumbani! Khee nyumbani??? Nauli unayo anasema Sina nimwambia sasa unaendaje ? Unajua nauli ya kwenu ni 70,000 Tsh.????
.
Akasema basi ntasubiri mpaka utakapo pata ndio nitaondoka!
Kumbe hapo alishaenda kununua vitu vyake kwa ajili ya safari..
Wife akasema usilazimishe mwache aende tu, basi Mimi kupiga simu kwao kuwa mwanawenu anarudi wakasema sawa nikaenda kukata tiketi na kumpa siku ya pili yake na kumsimdikiza KUPANDA gari na kuenda kwao. Tukaishia hapo usiku akanicheki nimefika salama haya poa.
Kisanga.!
Zimepita takriban wiki 3 Kuna bint mmoja MTAANI nadhani walikuwa na urafiki WA hapa na pale akaniambia hivi unajua mdogo wako ana mimba.???? Nikamwambia hapana sijui.
Akaniambia ana mimba na aliempa mimba kaikataaa
Mmmh, kaikataa kwanini na yeye ndio kahusika
Mdogo wako mwenyewe mapepe alikuwa na mabwana wawili ila anasema huyo mmoja alishakuacha na huyu WA pili ndio kaikataa mimba! Kwahiyo mnafanyaje ??? Tunafanyaje tena mbona atajua yeye Cha kufanya.!?
Nikajiuliza Ina maana yule bint upole wote ule na 16 yrs kumbe alikuwa anamiliki mabwana wawili??
Basi wadau ndio kilichonikuta nadhani aliondoka baada ya kujua kashanasa mimba ingekuwa aibu mtaani ili kuzima soo ikabidi arudi kwao kijijini.
Sasa madhara atapata mtoto hapa maana anakuwa hana baba WA kueleweka atakuwa na familia ya upande mmoja tu.
😂Shomile 🤣🤣🤣