Binti wa kiafrika alivyomteka Bob Marley kimapenzi

Binti wa kiafrika alivyomteka Bob Marley kimapenzi

O Diafro

New Member
Joined
Mar 13, 2021
Posts
3
Reaction score
5
Waliosema ukiachana na pesa, kitu kingine 'kinacho-run Dunia' ni mapenzi, wanathibitisha hili katika kisa hiki kifupi cha mapenzi.
FB_IMG_1778519830283.jpg
Pichani, anaonekana msichana mdogo akiwa ameketi chini na wazazi wake waliosimama. Picha hii ilipigwa mwishoni mwa miaka ya 1950 nchini Gabon.

Msichana huyu akiwa na wazazi wake pichani, ndiye baadaye aliyesababisha kwa mara ya kwanza mfalme wa reggae Duniani Robert Nesta Marley - maarufu kama Bob Marley kufanya tamasha kubwa la muziki Afrika kwa sababu ya kunasa katika penzi lake.

Msichana huyu ambaye kwa sasa ni mama mtu mzima, anaitwa Pascaline Omar Bongo, na mtoto wa aliyekuwa Rais wa pili wa Gabon 1967-2009, Omar Bongo Odimba(pichani).
image_search_1778560202264.jpg

Kwa mara ya kwanza Pascaline alikutana na Bob Marley hotelini Beverly Hills, Los Angeles Marekani Disemba 1979 akiwa binti wa umri wa miaka 23 tu. Bob Marley alipanga hoteli moja na Pascaline mara baada ya tamasha la reggae alilofanya siku hiyo.
image_search_1746989527894.jpg

Ni nani ambaye hakumfahamu mfalme huyu wa reggae nyakati hizo katika ulimwengu wa muziki wa reggae uliokuwa unarindima wakati huo? Umaarufu wa Bob Marley ulikuwa ni mkubwa sana Duniani kiasi kwamba hakuna mwanamke aliyeweza kumkataa. Na si ajabu mrembo wa Dunia 1976, mwanadada Cindy Breakspeare alijirahisi kwa mfalme huyu na kumtunuku penzi lililozaa mtoto aitwaye Damian Marley, na akawa mmoja wa wanawake saba waliotimiza idadi ya watoto kumi na moja wa Bob kabla ya umauti kumfika Mei 11, 1981 akiwa na umri wa miaka 36 tu.
image_search_1778560257915.jpg

Pascaline aliyekuwa masomoni Marekani, alipata taarifa kuwa yupo hoteli moja na mfalme wa reggae Duniani. Alijisogeza na dada yake ili amsalimie. Baada ya kumsalimia na kujitambulisha kuwa anatoka Afrika, Bob Marley alimwambia neno moja gumu, "wewe ni mbaya".

Aliambiwa neno hili, ambalo Pascaline ameongelea kwenye documentary yake aliyoitoa mwaka 2012 juu ya maisha yake na Bob Marley, kwamba ni kwa sababu ya muonekano wa nywele zake zilizolazwa kama za wazungu zikikinzana na uafrika wake pamoja na imani ya kirastafariani. Ni kwamba hakumaanisha ubaya wa sura, bali wa kiimani.

Pascaline anakiri kuwa alitumia usiku mzima na Bob wakipiga soga za hapa na pale, bila ya kufanya chochote(mapenzi). Lakini usiku huo ndio uliotengeneza njia ya wawili hawa kuzama katika penzi zito la siri licha ya kwamba walitoka dunia zinazofanana kwa hali ya kimaisha, ila zenye tamaduni na imani tofauti.
image_search_1778442143532.jpg

Pascaline aliporudi Gabon akiwa mwenyefuraha, ndani ya Ikulu ya 'geti kali' ya nchi hiyo hakuwa na kazi ya kumshawishi baba yake, Rais wa Gabon mzee Omar Bongo kwamba amkaribishe Bob Marley kufanya tamasha la reggae nchini humo. Kwa sababu alikuwa ni mtoto pendwa kwa baba, licha ya Bongo kutoupenda mziki wa harakati wa reggae, alikubali ili kumridhisha bintiye.

Mapenzi yalishinda nguvu ya misimo. Mapenzi ya baba kwa bintiye; na mapenzi ya Pascaline kwa Bob na kinyume chake, yalifanya tamasha kubwa la reggae kufanyika kwa mara ya kwanza katika ardhi ya Afrika katika uwanja wa Gymase Omnisport Bongo Januari 4 na 6, 1980 nchini Gabon.
image_search_1778560375963.jpg

Na hii ikawa imefungua milango kwa Bob Marley kutumbuiza Afrika ile aliyokuwa akiimba mara nyingi katika nyimbo zake . Kwani miezi mitatu mbele, Aprili 18 mwaka huohuo, alialikwa nchini Zimbabwe kutumbuiza kwa aajili ya sherehe za uhuru na kuzaliwa kwa wimbo maarufu wa "Zimbabwe".

Mapenzi ya wawili haya yalikuwa ya siri sana licha ya kwamba Bob alikuwa tayari na mke wa ndoa, Rita Marley, lakini haikumzuia kuwa na michepuko akiamini kwamba moja ya falsafa ya kirasta ni kusambaza upendo.

Kwa nyakati zote wakiwa pamoja, Bob Marley alimshawishi mara kadhaa Pascaline amzalie mtoto. Lakini alikuwa anasita kwa sababu ya umaarufu na uhuni wa Bob uliofanya awe na wanawake wengi aliozaa nao kwamba asingemuoa na kutulia naye, na umbali wa kimazingira.

Hivyo mara kadhaa walipokuwa wakikutana kimapenzi, Pascaline alitumia vidonge vya uzazi wa mpango.

Hawakufaidi sana mapenzi yao, si zaidi ya mwaka hadi pale Bob Marley alipogundulika kuwa na saratani Disemba 1980 ambayo aliambiwa amebakiza wiki tatu tu za kuishi, lakini akamaliza miezi sita.

Wakati akiugua, Pascaline mara kwa mara alimtembelea moenzi wake hospitali akiwa bega kwa bega na mama yake Bob, Cedella Booker. Na ndipo hapa Cedella alipotambua mahusino ya mwanye na binti huyu.

Bob Marley alifariki Mei 11, 1981 akiwa na umri wa miaka 36, na watoto 11 kwa wanawake 7. Ni wakati huu ndipo Pascaline alipokiri kujutia kutomzalia mtoto Bob licha ya kushawishiwa kwa nuda murefu.

Hata baada ya kifo cha Bob, ukaribu kati ya Pascaline na mama yake Bob ilikuwa ni kama 'meno na fizi'.

Nawasilisha kisa hiki kifupi kati ya Bob Marley na mtoto wa Rais, ikiwa leo ni kumbikizi ya kifo chake.
 
 
Mume wa huyo bint kwa SASA anajisikiaje akisikia habar kama hiz kwamba mkewe alikitembeza SANA kwa bob

Kaam hajaolewa imekaa poa
 
Back
Top Bottom