Binti wa miaka 10, shujaa alivyookoa watu zaidi ya 100 kutosombwa na mafuriko ya Tsunami

Binti wa miaka 10, shujaa alivyookoa watu zaidi ya 100 kutosombwa na mafuriko ya Tsunami

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
365
Reaction score
1,374
Tilly Smith akiwa na umri wa miaka 10, kwenye mapumziko katika Ufukwe wa Maikhao nchini Thailand mwaka 2004, aliona kuna kitu hakipo sawa ufukweni hapo.

Ilikuwa zimepita wiki mbili tu tangu aliposoma katika somo la Geography kuhusu Tsunami nchini kwao England, hivyo kwa kukumbuka kile alichofundishwa akaona kuna kitu hakipo sawa ufukweni hapo.

Hivyo, haraka sana binti huyo akawaambia watu wa familia yake na watalii wengine zaidi ya 100 wakasikia kile alichokizungumza wakaondoka eneo hilo, japokuwa awali mama yake alitaka kukataa kuondoka na hata alipokubali akikuwa mtu wa mwisho katika famili yake kuondoka ufukweni.

Muda mfupi baada ya wao kuondoka ufukweni hapo kukatokea Tsunami kubwa ambayo iliua idadi kubwa ya watu na kuharibu mali nyingi. (inadawa zaidi ya watu 250)

Alipokuja kuulizwa baadaye alisema alijifunza darasani kile kilichotokea katika Kisiwa cha Hawaii mwaka 1946, hivyo akajua kuwa Tsunami inaweza kusababishwa na tetemeko la ardhi na mlipuko wa volkano.

Mwaka mmoja baada ya tukio hilo la Ufukwe wa Maikhao, binti huyo alipewa tuzo maalum nchini Uingereza kwa ushujaa wake huo, kwa sasa ana umri wa miaka 28.

390044266.jpg
 
Mwalimu anae ichora microscope ubaon ili wanafunzi waone mfano wake kwakua shule Haina vifaa
Hata huyo mwalimu mwenyewe asingeweza kuwaokoa watu kwenye hiyo tsunami
 
Kawaida sana wewe umewahi kufanya lipi mzee baba? Msipende kurahisisha mambo nna uhakika hata upepo wa Tsunami hujawahi kuuona
Nimeona vingi sana, niemfanya mengi sana na bado naendelea kufanya mengi makubwa...

Ni vile tu mambo yangu nakaayo mwenyewe...
 
Back
Top Bottom