Binti Yangu; Huwezi kuwa Mchepuko kama sio Malaya. Kila mchepuko ni Malaya

Binti Yangu; Huwezi kuwa Mchepuko kama sio Malaya. Kila mchepuko ni Malaya

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,153
Reaction score
93,069
BINTI YANGU; HUWEZI KUWA MCHEPUKO KAMA SIO MALAYA. KILA MCHEPUKO NI MALAYA.

Anaandika, Robert Heriel Mtibeli.
Baba Mkali.

Wala sitakuonea aibu binti yangu. Nitakuambia Ukweli wote.

Ni kweli kabisa, hakika. Pasipo na shaka kwamba. Mwanamke yeyote ambaye ni Mchepuko huyo ni Malaya. Wala hakuna jina lingine.

Namaanisha, ukiona mwanamke yeyote, bila kujali nafasi yake, uhusiano wenu hata kama ni Mama, bibi, Shangazi, mama Mkwe, Binti yako/yangu. Ni Mchepuko. Jua huyo ni Malaya.

Hayo majina Mchepuko kwenye lugha yapo kwa lengo la kupunguza ukali wa maneno, wanaita kutumia tafsida. Yaani kuwastahi.

Mfano kusema Mavi na kinyesi. Kuzaa na kujifungua, haja kubwa na kunya. N.k.
Jambo ni lilelile.

Unaposikia mtu ni mchepuko au anajitambulisha kama mchepuko. Huyo ni Malaya.
Ni sawa wewe unaona mtu amekunya Mavi. Alafu yeye anakuambia nimejisaidia haja kubwa. Ni kitu kilekile.

Ukisikia Umalaya, ukahaba, ambapo siku hizi wameleta neno Kudanga. Ni jambo lilelile.

Zamani kulikuwa na madanguro ambapo ni nyumba za makahaba.
Kuna makahaba wa umma na makahaba yaliyobinafsishwa na kampuni au kikundi cha watu au mtu mmoja.

Binti yangu, wewe sio kahaba mpaka mwanaume akupangie chumba au nyumba ambayo mtakuja kufanyia ufuska wenu. Hilo ni dangerous. Hiyo sio nyumba.

Nyumba ina sifa na vigezo vyake.
Hata uwe maskini vipi. Usikubali kugeuzwa kahaba, Malaya na kukodishiwa danguro lako.

Binti yangu, najua unajua sisi Watibeli ni watu wa aina gani. Hushindwi kujua kile ninachokisema hata kama nisingekisema.

Nilikuambia huna uzuri wowote binti yangu.
Uzuri wako upo kwa yule atakayetaka kuishi na wewe, kukuoa kwa heshima, kula viapo vya mke na mume. Ninyi wawili kisha sisi kama wazazi ni kutupa taarifa.

Mtu hawezi kukuita mzuri wakati hataki kukufanya uwe mkewe binti yangu. Anakudanganya. Amekudharau binti yangu.
Anataka akutumie na kukudhalilisha kwa kukufanya kama kahaba na Malaya.

Sio sifa mbele za watu wenye akili na maadili kusema umepangiwa nyumba na mwanaume ambaye sio mumeo. Unajidhalilisha binti yangu.
Usijikosee heshima kiasi hicho.

Usiige watu wa jamii zingine. Wewe ni Mtibeli. Ni bora uishi maisha ya kimaskini kuliko kugeuzwa kahaba. Kuliko kudharau uanamke wako.

Nafikiri unajua sisi Baba zako tukoje. Hatutakubali uitwe binti yetu kwa kufanya ukahaba.

Yaani binti wa Tibeli uwe mchepuko? Mchepuko..! Haaa! Huko ni kujishusha kwa kiwango cha mwisho kwa mwanamke.

Kama umekosa wanaume au wanakuchanganya zungumza na
Mama zako. Zungumza na Baba zako. Sisi ni wazazi wako. Binti sisi ndio tuliokuzaa. Usione aibu kuomba msaada muhimu kama huo.

Sema, Wazazi wangu. Naomba mnitafutie Mume. Weka vigezo vyako. Tutavijadili. Nasi tutakutendea HAKI.

Sisi Watibeli tuna marafiki wengi. Tuna familia nyingi sehemu mbalimbali. Hatuwezi kukosa mume wa kukuoa binti yangu kiasi kwamba uwe mchepuko.

Mpaka unakuwa mchepuko ni huna wazazi au? Au ni ujuaji, ukahaba na umalaya vinakusumbua?

Achana na wale wajinga wanaokuambia mapenzi hayashauriki. Ni wajinga hao. Wao kila kitu hakishauriki sio mapenzi tuu.

Hiyari ikishindikana tumia nguvu.

Binti yangu, vigezo vya wanaume ambao ni waume bora unavijua. Usifuate Hisia zako. Nilikufundisha hivyo.
Mapenzi sio Hisia. Mapenzi ni uchaguzi.
Unachagua kisha hisia ndio zitafuata.

Tumia Akili binti yangu. Kama mwanaume anakupenda mwambie Akuoe. Kama anamke mwambie nitaongea na mkeo ili tuwe Wake wawili. Mkewe kama hataki usiingilie hiyo familia.

Tafuta wako. Wamejaa. Kama huwezi kutafuta. Omba msaada tutakusaidia.

Zingatia, ni muhimu kufuata zile kanuni nyingine.

Baba yako nimemaliza. Baba ninajivunia binti mwenye Akili na anayejua thamani yake. Anayejua dunia hii yeye ni nani.
Babaako sipendi uwe binti uliyejidharau na uliyekubali kudharauliwa na watu kwa hiyari yako.

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
 
Tho michepuko inasaidia sana.

Sometimes wife kisirani unaenda kujipooza kwa sidechick
Screenshot_20260616-001732~2.jpg
 
  • Tatizo lipo kwetu sisi wanaume, tunao oa na kubeba majukumu ya kiume tumebaki wachache sana, vijana wengi wakiume wanataka kulelewa, matokeo yake wanapoteza nguvu za kiume na wengine kugeuzwa wanawake.​
  • Dada zetu kuwa michepuko, imetokana na upungufu wa wanaume ambao wako tayari kubeba majukumu.​
 
Huo ndio ukweli japo wengi watabisha
 
Back
Top Bottom