Biochemia ya ugonjwa wa albino

Biochemia ya ugonjwa wa albino

genuineme

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2014
Posts
387
Reaction score
131
Hitilafu ya rangi (albinism) husababishwa na mabadiliko hasi katika eneo kinasaba(Gene) kwenye chromosome ya 11; eneo hili hutengeneza kimeng'enyo au catalist (enzyme) iitwayo tyrosinase. Kuharibika(mutation) kwa eneo kinasaba huathiri ubora wa enzyme tyrosinase inayopelekea kushindwa kutengenezwa rangi ( melanin) katika ngozi,nywele,mboni ya jicho(iris) na ukuta wa nyuma ndani ya jicho(retina) .

Viungo vyote vya albino ni vya kawaida kabisa isipokua kukosa rangi hiyo(melanin pigment).

Katika sehemu zote hizo rangi hii ufanya kazi ya kufyonza mionzi mibaya ya jua ,yaani UV light,type A,B&C; inayoweza kusababisha cancer. Mionzi hii inayokuwa na mawimbi yenye (wavelength) around 300nm hunyonywa na processed amino acid tyrosine yenye uwezo wa kunyonya mionzi katika wavelength hiyo.kuna aina mbili za melanin, moja ya mchanganyiko nyeusi na kahawia (eumelanin) hasa kwa waafrika,na nyingine nyekundu na njano(pheomelanin) hasa kwa wazungu.
 
.... .....
 

Attachments

  • 1411579300267.jpg
    1411579300267.jpg
    9 KB · Views: 104
..... .......
 

Attachments

  • 1411579568724.jpg
    1411579568724.jpg
    28.4 KB · Views: 92
tunashukuru kwa elimu uliyotoa.ila albinism sio ugonjwa
 
Na kwa wale waafrika wenye rangi nyeupe inakuwaje ila sio albinos?
 
Rangi zote hizi nne huweza kuzalishwa kutokana na amino acid moja hiyohiyo,yaani tyrosine inayopatikana katika vyakula vya protein. Kwa mfano wa sections viwandani ,huweza tengenezwa katika sections yaani pigment nyeusi,kahawia,nyekundu na njano. Rangi inayochukua asilimia kubwa katika mchanganyiko hubeba density ya mwonekano,na rangi chache hufanya moderation. Kumbuka enzyme yenye shida kwa albino Ni ya kwanza ambayo wale wazima wanayo, lakini mbele kutakua na enzyme nne za kuifanya kuwa rangi ya aina nne kabla ya proportions zake kuwakilisha athari katika mwonekano wa ngozi. Inakuwa kama mchoraji anayepaka rangi ,akimix pink na kijani anaeza pata rangi nyingine ya ajabu kabisa. Basi mchanganyiko huu hutegemea urithi wa genes toka kwa wazazi wako,na reorganization ya genes ulizorithi ili kuunda upekee wako yaani recombination
 
Back
Top Bottom