life is Short
JF-Expert Member
- Apr 1, 2013
- 4,741
- 3,035
Laa laa...kwa mtindo huu uloanzisha hakuna Msalliye kwa siye tunaoendekeza mloo usitupite !! hapatapona mtu!!Hahahaha hupasuki tumbo bwana..m
Laa laa...kwa mtindo huu uloanzisha hakuna Msalliye kwa siye tunaoendekeza mloo usitupite !! hapatapona mtu!!
Yaani mwezi mzima wateremsha mapochpocho 5 stars bila mapumziko..... Mmmh unania mbaya binti Nass!!
Tiisllam yedeiki !!
Salaama yako !! sisi tule tuvimbiwe, tuneneane kama gunia la nchele !! Nawe utokeleze kaModels!! mmmh hapo kuna siri....!Hahahaaahha.....wewe kula tu mwili haujengwi kwa matofali lol
Salaama yako !! sisi tule tuvimbiwe, tuneneane kama gunia la nchele !! Nawe utokeleze kaModels!! mmmh hapo kuna siri....!
Hahahhahahahaha kwa raha zake....mpikie shem wangu bhana.beeee akhsanteeee mamiii mulo mutamu sana nitampikia shem wako
farkhina kuna chakula kimoja nimessahau jina lake nlishawahi kuekezwa siku moja kupika miaka mingi sana kama unajua nisaidie nakitamaniii sana.
Zinakuwa kama mkate wa ufuta ila hauweki hamira unabonda bonda unga ila unakandia maziwa sijui tui la nazi sikumbuki unaweka nyama na njegere katikati size zinakuwa kama mkate wa ufuta halafu unazikaanga kama na mafuta mengi kama ya kukaangia maandazi.Nitaaamu sana kama umeelewa naomba nisaidie mupenzi.
Mwaaaa mwaaa mwaaa
beeee akhsanteeee mamiii mulo mutamu sana nitampikia shem wako
Mahitaji
Nyama nusu
Chumvi kiasi
Mafuta 1 Kikombe
Vitunguu maji 3 vikubwa
Nyanya 3 kubwa
Nyanya kopo
Thomu 1 table spoon
Tangawazi 1 table spoon
Pilipili mbichi iliyosagwa 1 tea spoon
Kotmiri (giligilani) iliyokatwa 2 Vijiko vya chakula
Viazi 6
Uzile wa unga 1table spoon
Mtindi ¼ Kikombe cha chai
NAMNA YA KUTAYARISHA KUPIKA
1. Kwenye karai au (sufuria) mimina mafuta Yakishapata moto mimina vitunguu vikaange mpaka viwe rangi ya hudhurungi. Vitowe viweke pembeni.
2. Kaanga viazi na viweke pembeni.
3. Chukua sufuria tia nyama, thomu, tangawizi, pilipili, nyanya, nyanya ya kopo, mtindi. Chemsha mpaka iive.
4. Tia vile vitungu ulioyovikaanga, tia viazi, uzile, kotmiri na yale mafuta uliokaangia vitunguu kama ¼ kikombe, acha moto mdogo mdogo kama ¼ saa, epua weka pembeni.
VIPIMO VYA WALI
Mchele kg 1
Mdalasini mzima wa vijiti
Zafarani ½ kijiko cha chai
Rangi ya biriani ¼ Kijiko cha chai
Mafuta yaliyokaangiwa vitunguu ½ Kikombe
Chumvi kiasi
Zabibu kavu.
Roweka zafarani na rangi kwenye kikombe na ¼ kikombe cha maji. Roweka kabla ya robo saa.
NAMNA YA KUTAYARISHA
1. Osha mchele uroweke kwenye maji muda wa dakika 20.
2. Chemsha maji kwenye sufuria kama magi 10.
3. Tia mdalasini.
4. Yakishachemka unatia mchele,chemsha usiive sana, unamwaga maji.
5. Unamimina tena ule mchele ½ yake kwenye sufuria, unatia rangi na zafrani kidogo na zabibu halafu unamimina mchele uliyobakia unatia rangi iliyobakia.
6. Mafuta yake unayachemsha mpaka yachemke unamimina juu ya mchele, unarudisha motoni unaweka moto mdogo ukisha kuiva, tayari kupakuliwa.
7. Unapakuwa wali unaweka chini kwenye sahani na juu yake sosi ya nyama.
Umesomeka mamaaa.
Uzile ndio nini,hapo sijaelewa bado. Naomba unilekeze duka/mahali hapa dsm ambapo naweza pata spices/viungo vya kunogesha maanjumati ambavyo often unavitajaga humu jamvini km hiyo uzile,zafarani,zabibu kavu e.t.c
Uzile ni bizari ya pilau...
Maduka ya viungo kwa dsm sifaham ngoja wenyewe wa dar waje watakuambia
Shukrani sana.
Umesomeka mamaaa.
Uzile ndio nini,hapo sijaelewa bado. Naomba unilekeze duka/mahali hapa dsm ambapo naweza pata spices/viungo vya kunogesha maanjumati ambavyo often unavitajaga humu jamvini km hiyo uzile,zafarani,zabibu kavu e.t.c
Karibu sana
Ni binzari nyembamba
Nenda kariakoo, pale Shimoni, kwa nyuma kuna solo la nje, wanauza viungo vya kila aina mule ndani, Pia upande wa pili ule upande wa maduka ya Tahfif kuna duka moja kubwa sana la viungo, limeandikwa SPICE....something....hutokosa kiungo chochote pale.
Kila la kheri Ndesalee
Sasa hv nishakaribia humu jamvini. Mana nimechoka kula migahawani kila siku.
Wkt nipo primary to O-Level mamangu alikuwa ananifundishaga kupika. Nashukuru jikoni mimi sio mgeni sana,ingawa nimezaliwa na kukulia mjini.[/QUOTE
Usijali basi ntakua naku mention nikiweka mapishi mapya nawe uwe unatuwekea makulati yako ati lol