Nasubiri kukuche vizuri niende maeneo hayo leo. Ila naomba ni PM spices ambazo ni vzr nikawa nazo ndani kwa ajili ya mambo ya maakuli mbali mbali sio based on pilau tu.
Sasa hv nishakaribia humu jamvini. Mana nimechoka kula migahawani kila siku.
Wkt nipo primary to O-Level mamangu alikuwa ananifundishaga kupika. Nashukuru jikoni mimi sio mgeni sana,ingawa nimezaliwa na kukulia mjini.[/QUOTE
Usijali basi ntakua naku mention nikiweka mapishi mapya nawe uwe unatuwekea makulati yako ati lol
Itakuwa vizuri sana.
Muelekeze na duka la viungo
Amu shemegi hajambo?
I always wanted to learn how to cook Biriani as it is my favorite dish. Thanks.
Huyo alikuwa sato.
Sauce yake ni tamu balaa.
Basi namtaniaga Mpenzi niache kazi niwe nasimamia miradi na mama wa nyumbani.
Ananjibu "asa ukikaa home utakuwa na kazi gani kupika nakupikia mke wangu zaa kwanza ndo ukae home uwe unacheza na mtoto"
Hajambo.
Kuolewa na mwanaume anayejua kupika ni shida. farkhina shem wako anajua kupika balaa.
Mie hata robo simfikii.
Basi nimekosa ujasiri namuacha apike yeye mimi namsaidia kutayarisha tu au najilaza sitting room.
Kama ingekuwa nyumba ya kushare walah ningekoma maana maneno ya waja nimempa limbwata.
Wakati mwingine naona aibu farkhina hata kukupiga picha nashindwa....ngoja nikutumie baadhi ya picha nlizojiba nikajipiga
Asanteeeeeeee
Nimeshaijua hiyo nyama....ila babu weye una lako jambo lol
Umewahi kula maini pia yaliyopikwa hivo hivo?
Naomba unielekeze mapishi mazuri ya maini kama hutojali..nataka nianze nayo kesho
Rosti? Au ya kukausha?
Rosti itakuwa poa
Ya kula watu wangapi? Sorry kwa maswali mengi nijue naandikaje vipimo
Usijali we uliza tu..watu watatu
Okay...
Mahitaji
Maini kg 1
Nyanya ya kopo
Kitunguu maji kimoja kikubwa...
Kitunguu saumu kilichotwangwa kijiko kimoja cha chai...
Tangawizi kijiko 1 cha chai...
Limau 1....
Bizari ya pilau nusu kijiko cha chai..
Mdalasini nusu kijiko cha chai....
Chumvi kiasi...
Namna ya kutaarisha
Katakata maini yako weka katika sufuria tia chumvi,saumu na tangazi...
Bila ya kuweka maji chemsha maini moto mdogo mdogo...
Maji yakikaribia kukauka ongeza kdg kdg hadi kuwiva ila bakiza na supu.....
Katika sufuria ingine kaanga kitunguu hadi golden brown na weka maji tu bila ya maji...
Weka nyanya ya kopo,mdalasini na bizari ya pilau (cummin) na koroga acha vichemke...
Weka limau na chumvi kdg kama itahitajika...
Epua tayar kwa kuliwa..
Ukipenda weka hoho na giligilani