kilimasera
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 3,068
- 277
MABINGWA wa Kombe la Carling nchini England, Birmingham City, wanatarajiwa kutua nchini Julai mwaka huu kwa ziara maalumu ya kimichezo ambapo watakipiga na vigogo wa soka nchini, Simba na Yanga, jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Simba, Alhaj Ismail Aden Rage, alisema jijini Dar es Salaam jana kuwa baadhi ya maofisa wa juu wa timu hiyo, akiwemo kocha msaidizi, Andy Watson, pamoja na daktari Ian Mc Guinness, wanatarajiwa kuwasili nchini Mei 9 kwa ajili ya kukagua Uwanja na Hoteli.
Rage alisema, ujumbe huo utakagua Uwanja wa Taifa utakaotumika, pamoja na hoteli ya Kilimanjaro Kempinski ili kuona kama vinakidhi vigezo vya timu hiyo, ambayo itaambatana na mashabiki wasiopungua 1,000 ambao watajilipia gharama za hoteli na uwanjani.
Alisema, usiku wa Julai 7, Birmingham itakipiga na Simba kabla ya jioni ya Julai 12 kukipiga na mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2010/2011, Yanga.
Tunafurahi kupata wasaa wa kuwa wenyeji wa timu kubwa kama hiyo, ujio wao huo utafungua mipaka ya kimataifa baina yetu na wao tayari tumeshazungumza na watu wa Wizara ya Maliasili na Utalii juu ya ujio huo, alisema Rage.
Katika hatua nyingine, Rage alisema mkutano mkuu wa mwaka wa wanachama wa klabu hiyo, unatarajiwa kufanyika Mei 15 katika Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam na wanachama watakaoruhusiwa kushiriki ni wale ambao watakuwa wamelipa ada ya mwaka ambayo ni sh 12,000 pamoja na ile ya uwanja sh 20,000 na kwamba malipo hayo yafanywe katika akaunti ya wanachama.
Pia Rage alisema, uongozi umetoa saa 48 kwa wapangaji wanaotaka kuendelea kupanga katika jengo lao kuwasiliana na uongozi, kinyume cha hapo watakwenda kuomba kibali chama mahakama kwa ajili ya kuwaondoa kwa nguvu.
Wakati huo huo, beki wa timu hiyo Kelvin Yondani amewasilisha barua ya kuomba msamaha kutokana na utovu wa nidhamu huku akisihi arudishwe kundini, wakati mshambuliaji Mussa Hassan Mgosi ambaye naye aliadhibiwa kutokana na kukiuka mkataba kwa kuzungumza sana na vyombo vya habari, akitakiwa kusoma upya mkataba wake na kutoa maelezo.