Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi, njia ni moja na kila mtu atapitia, mwenzetu ametangulia nasi katika saa wala tarehe wala mwaka tusiojua tutafatia.
Nawaombea Mungu awatie nguvu katika kipindi hiki kigumu cha msiba,Bwana ametoa na Bwana ametwaa kazi ya Mungu haina makosa. Amina.poleni sana wanafamilia.
sisi wana JF hatuwezi kukufariji ama kuziba pengo la mzazi wako!! Zaidi ya yote tunamkaribisha rohomtakatifu awe mfariji wako, akutie nguvu, akukumbatie, akufundishe kutoka na kuingia!!!
Molla, awajalie subira na kheri muweze kupita kipindi hiki kigumu, na kumuombea Pepo na neema za utukufu wake Mwenyezi, Baba Bishanga alale mahali pema peponi Ameen.