Mhabarishaji
JF-Expert Member
- Oct 5, 2010
- 1,007
- 600
Somo katika Ibada hiyo Kuu ya Pasaka, lilikuwa na kichwa,"JE, NI HALALI KUIDAI TANGANYIKA KATIKA MPANGO WA MUNGU?" Alianza kwa kusema,"Kabla sijatoa ufafanuzi, niseme kwanza kifupi bila kuumauma maneno, NDIYO NI HALALI, NA NI MPANGO WA MUNGU, kwa herufi kubwa." Akasema, yeye hatajenga hoja kwa ushabiki wa kisiasa, bali atajenga hoja kwa Neno la Mungu, ambalo ndilo linaloelezea mpango au mapenzi ya Mungu katika mambo yote.