Kakobe ni bora aendelee hivyo hivyo kuwa mpiga kura kutokana na hisia zake lakini asiwabague wafuasi wake wanaotaka serikali mbili,au tuseme kakobe hana wafuasi wa CCM
mkuu tupia audio yake fasta hawa ndo viongozi wa dini sio kina askofu mdegela na mtetema hawawezi kukemea maovu ya watawala
Safi sana mkuu, humu huwa kuna watu wapuuzi wakiona uzi unawachoma wanaanza kuleta vitu vya kipuuzi ili kuhamisha mjadala.Usichanganye mada utapeli wake hautuhusu sie tuko na ishu ya Tanganyika yetu hizo ishu za utapeli kuna sehemu ya kuzipeleka usituchanganyie ishu hapa!!
Hili suala la kuchanganya dini na siasa ambalo baadhi ya watu kwa nia binafsi wamekuwa wakilipigia kelele na ukiwauliza waeleze kwenye Biblia wapi inazuia hawakuelezi!Mbaya zaidi wanalipigia kelele kwa mtu anayesema ukweli unaowagusa wao.Askofu Kakobe angesema mambo yanayowafurahisha watawala usingesikia kabisa suala la kuchanganya dini na siasa.Wapo viongozi wa dini kadhaa wanaozungumza mambo yanayowafurahisha watawala,husikii huyu amechanganya dini na siasa!.Ifikie pahala tupende kuambiwa ukweli ili tuiponye nchi na vizazi vijavyo.Tusifurahie kudanganywa hakuwezi kulijenga Taifa.Anayedhani anaweza kumnyamazisha Askofu Kakobe kwa kauli za kusema anachanganya dini na siasa ni kupoteza muda.Kwa suala la Biblia amepewa neema kubwa sana ya Mungu ya kuijua kwahiyo huwezi kumdanganya kwa porojo hizo!Soma Biblia uone jinsi watumishi wa Mungu walivyowakemea watawala walipofanya maovu.Watanzania sio matahira hivyo mnavyodhani,wanajua ngano na makapi.Kama kuna mshirikina bado anawadanganya kwamba watanzania wataendelea kuwa mazezeta kwa uchawi wake anajidanganya nafsi yake.KILA LENYE MWANZO LINA MWISHO.
ni -------- pekee anayeweza kuidai tanganyika ya wakoloni na kuibeza Tanzania yetu
Duh, kutetea Utanganyika sasa kumebatizwa ushetani na wahafidhina. CCM, mtawatukana na kuwakana wangapi? Jaji Joseph Sinde Warioba, Jaji Augustino Ramadhani, Mwenyekiti mstaafu wa OAU Salim Ahmed Salim na waheshimiwa wote waliokuwa kwenye Tume ya Katiba, waliodiriki kusikiliza maoni ya wananchi badala ya CCM, sasa wanatuhumiwa kuwa na tabia chafu za kishetani. Mbonamasabo Job, safari hii CCM have bitten more than they can chew...subirini, hizi ni rasha rasha tu! Tanganyika inakuja mtake msitake!Usiseme BISHOP KAKOBE sema SHETANI KAKOBE maana hakuna Bishop mwenye tabia chafu kama za Kakobe hilo ni jini sio Bishop
Dini na siasa ni vitu viwili tafauti,ushauru wangu Askofu angalia neno la bwana acha siasa kwa wanasiasa
Naskia 2015 atagombea ubunge
siasa kanisani! sio sahihi
Hivi unamjua Kakobe? HIYO MACHINE KUBWA
Asante sana baba Askofu Kakobe tunakushukuru kwa kutuelewesha kwa kutumia maandiko. Tanganyika yetu yunaipenda na tunaitaka. Mungu akuzidishie maisha marefu ili watu wamjue Yesu wajue na haki zao pia.
hata nabii "Samuel" alikemea maovu aliyoyafanya Mfalme "Sauli",na pia Mfalme "Daudi" kutembea na mke wa mtu,alikemewa na nabii "Nathani",naye akatubu,ila "Sauli" hakutubu akafa kifo kibaya,yupo Mfalme Ahabu alifanya mabaya kwa kumuua "Nabothi",Myzreeli,Mungu akamtuma Nabii "Eliya" amkemee kwa kitendo alichofanya,baadaye naye Mfalme "Ahabu" alikufa kifo kibaya.Leo tunahitaji watumishi wa Mungu wanaosema kweli kwa viongozi,big up Mch.Kakobe na Rev.Mtikila
Shetani ambaye anatenda kazi ndani yako anajua kuwa Kakobe ni mtumishi wa Mungu na hapa anafanya kile ambacho shetani na watawala wasingependa watu wajue; yaani kuziexpose kazi za shetani mojawapo ikiwa ni ya wizi wa kuliiba taifa na kulificha kuzimu, Tanganyika njoooooooooo!!!Usiseme BISHOP KAKOBE sema SHETANI KAKOBE maana hakuna Bishop mwenye tabia chafu kama za Kakobe hilo ni jini sio Bishop