Kakobe aliongeza kusema,"Inashangaza kuona kila tarehe 9.12. tunasherehekea Uhuru wa nchi ambayo watu wengi, pamoja na Viongozi wakuu wa Taifa, wanashindwa kuitaja, na kuionea haya. Kutamka "Uhuru wa Tanganyika" kwao ni kosa kubwa. Baadhi yao wanathubutu kusema,"Uhuru wa Tanzania Bara" au "Uhuru wa Tanzania", wakati katika historia, hakuna Uhuru wa nchi hizi! Tunaposema "Tanzania Bara", je, na wakazi wa Mafia, wao nao wako Bara ipi, wakati Mafia ni Kisiwa? Upande wa pili, mambo yasiyo ya Muungano yanashughulikiwa na Serikali ya Zanzibar, sasa upande wetu, mambo yasiyo ya Muungano, yanashughulikiwa na Serikali ipi, wakati hakuna Serikali ya Tanganyika, wala Serikali hiyo ya "Tanzania Bara"????? Muungano wa namna hii siyo mpango wa Mungu, na ni Mwasisi wake tu Nyerere, aliyekuwa na uwezo wa kuushikilia, kutokana na "mamlaka yake ya ubaba, na uasisi". Yeyote ambaye siyo baba au Mwasisi, hawezi kuushikilia Muungano wenye muundo huu. Ikiwa wakati wa uhai wa Nyerere, bado kulikuwa na Tume za akina Nyalali n.k, pamoja na G55, basi nyakati za sasa moto wa kuidai Tanganyika, hakuna awezaye kuuzima. Hata Marekani hivi leo, yako mambo mengi ya Mwasisi wa Taifa lao, George Washington, ambayo yamebomolewa kabisa, na kutupwa kule!! HATA HAPA NI SUALA LA MUDA TU!!!!!!!!