Tanesco iko na mizigo mingi haswa watendaji na vile imekuwa tochi ya wanasiasa ndiyo upuuzi umekuwa mwingi Mh Dk Biteko NWM WN chungulia hivi kwa ustawi wa Tanesco na Taifa kwa ujumla,
1. Punguza mzigo wa management ya shirika kwani iko na watu zaidi ya 15 ni upuuzi , ibaki na watu chini ya 10 si kila mtu anakuwa Mkurugenzi shirika linakuwa la kimwinyi sana.Hapa itaenda sambamba na kupunguza mameneja wa makao makuu.
2. Pata taarifa za utendaji wa mameneja wa Kanda, Mikoa, na Wilaya kwani wengi wao hawajui nini wanafanya zaidi ya kufanya kazi za wasaidizi wao WAULIZE KAMA HATA JDs kama wanapewa au wanafahamu majukumu yao licha ya kulipwa vizuri kwa kiasi chake. Chaku shangaza hadi kipindi hiki bado mpo na mameja wa wilaya mafundi mchundo (Technicians) hapa bado mnataka kupata matokeo chanya?. Wengi wao mizigo katika taratibu za utawala kuhakikisha hicho wapatie nafasi watoe walichonacho kwa wananchi kupitia vyombo vya habari utakuja shukuru hapa na ukizingatia ni sehemu ya fani yao .
3. Hakikisha materials za kufanyia kazi zinafika kwa wakati mfano nusu ya mwaka wa fedha 2023/2024 inaenda hakuna vifaa vya miradi hata matengenezo ili kufikia malengo ya kuwahudumia wateja store za mikoa, kanda na makao makuu zijae vifaa vyenye matumizi na si ili mradi vifaa , Hivi mteja amelipia kuunganishiwa umeme kwa nguzo inakuwaje mnashindwa mfungia kwa wakati hili nalo la kusubili taratibu za manunuzi za mabilioni. Rudisha hadhi za manunuzi kwa mikoa, Kanda na makao pia lakini hapa ufuatiliaji muhimu sana kwa maana kuna michezo inapigwa mno . Leo hii kazi hata ya cheche kweney nguzo/bracket Tanesco hawana connector kweli store hakuna hata connector za elfu 1 hii si sawa. Fanya matengenezo ya njia za umeme kwa kuzingatia hupatikanaji wa umeme kwa wakati na si kuzima hovyo hovyo kwa kazi chache tena si za tija( siyo kila nguzo ya mti ni kikwazo cha umeme kukatika tupunguze gharama zisizo na sababu).
4. Boresha maslahi ya wafanya kazi haswa wale wa katika mazingira magumu mfano kwenye vituo vya kufua umeme wapeni hardship allowance yenye tija na si 10% ya mshahara watu wanapitia ulemavu wa kusikia/akili kwa kelele za mitambo na hatarishi ya maisha kukaa chini ya migodi si kazi ndogo. Walipe masaa ya ziada ikiwa wamefanya kazi kwani watendaji ni wachache na kazi ni nyingi toa tabaka la Extra duty kwenda Overtime kwa wote , siyo kubagua generation na Transmission kuwalipa fully wengine masaa machache na bado kazi zipo au la hasha Ajiri watu ili wapate pumzika wengine.
5.Tengeneza wataalamu kwa gharama kubwa ili mitambo iwe inafanyiwa matengenezo makubwa na watu wako ni kiasi cha kuwapa mafunzo thabiti kutoka kwa hao watengeneza mitambo itaokoa muda na pesa ya kuita kampuni za kigeni kwa kazi ambazo hata shirika lingefanya tena kwa weledi.
6. Simamia nidhamu na lugha nzuri dhidi ya wateja Tanesco inapokwama ni kila mmoja kuwa msemaji bila kuzingatia weledi , Wateja wapewe taarifa za upatikanaji wa umeme na ukosekanaji wake kwa taarifa zenye kueleweka si ili mradi tu, Sikiliza mawazo ya watendaji wa chini utapata kitu hata cha kujifunza na utaona namna nidhamu haipo kwa kiwango kizuri ndani ya shirika.
7. Wajenge kila mfanyakazi ajue JD yake na si kwenda bila muongozo kwa maana shida hiyo ipo sana ndani ya shirika , wapimwe kwa kada zao na kupatiwa stahiki kwa upimaji huo .
Hitimisho,
Omba kwa Mh Raisi akupe msaidizi mwingine ili upate muda wa kufanya kazi zingine za uratibu wa serikali kwa maana mizigo uliyopewa utaishia lalamika na kupokea taarifa za uongo kwa chuki binafsi kisha kuwaumiza wengine hiyo haipunguzi nafasi yako Tanesco inataka waziri awe karibu nao mno la sivyo uzembe ni mwingi kufumba na kufumbua tu.