Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Naibu Waziri Mkuu, Dk Doto Biteko ametangaza kufuta likizo kwa watumishi wote wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) akiwataka wote wawe kazini kukabiliana na changamoto ya upungufu wa umeme.
Amesema hakuna mtumishi wa Tanesco atatakiwa kwenda likizo wakati huu wa changamoto ya mgawo wa umeme na kwamba, kila mmoja kwenye eneo lake atatakiwa kufanya kazi kwa bidii.
Dk Biteko, ambaye pia ni Waziri wa Nishati ametoa agizo hilo leo Ijumaa, Februari 23, 2024 wakati alipotembelea chanzo cha kuzalisha umeme cha Kidato mkoani Morogoro.
Naibu Waziri Mkuu huyo yupo kwenye ziara kukagua vyanzo vya kuzalisha umeme, kuangalia shughuli za uzalishaji ikiwa ni mkakati kumaliza changamoto ya upungufu wa umeme nchini.
Hatua hiyo ya Dk Biteko imetokana na kupewa taarifa kwamba, Meneja wa Tanesco Mkoa wa Morogoro, kuwa amekwenda likizo.
“Huu ni muda wa kukimbiza kutatua changamoto zilizopo mbele yetu. Nitoe wito kwa uongozi wa Tanesco kuwa hakutakuwa na likizo kipindi hiki ambacho watanzania wanakabiliwa na changamoto ya umeme.
Hakuna likizo tena kuanzia sasa hivi kwenda mbele kwa mtu yeyote anayefanya kazi Tanesco. Nilivyosema Tanesco hamtalala wakati huu wa mgawo nilikuwa naaminisha, haiwezekani tuko kwenye changamoto halafu kuna wengine wanataka kulala.
Sisi wenyewe tunazunguka kila mahali kuhakikisha wananchi wanapata umeme. Katika hili tutachukua hatua kwa aliyeidhinisha likizo n ahata huyo aliyeomba likizo wakati huu ametoa wapi ujasiri,” amesema Dk Biteko.
Anaanza kuonea watu
Unakosea sana mtoa hoja ni Biteko siyo wasukuma.Maamuz
Ya kingosha wnapokuwa failure
Hii jamii isijepewa nchi Tena
Kwani ni upungufu au ukosefu? Kama vyanzo au miundombinu havina maji au nyenzo, hii haiwezi kusaidiaHiyo inaweza ikawa suluhu kweli??
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]hii ndo banana republicSasa mfano mtu anataka kuchukua likizo ya uzazi asiende ???
Akijifungua hapo kazini ndio umeme utawaka??
Pitia hata comments za wadau ujifunze kitu, haihitaji hata elimu ya chekechea kujua hiyon hatua ya kihuni kuuhadaa umma.Afadhali waziri uwazuwie likizo,hawa ndiyo wanachangia,sisi kukaa gizani kisa mgao,wangepunguziwa na mishahara + posho
Hiyo inaweza ikawa suluhu kweli??
Sasa kama kuna changamoto ya kimfumo kwenye distribution network, inayohitaji uwekezaji mkubwa kutoka serikalini na zaidi ya mwaka mmoja wa matengenezo, kumnyima Mfagizi wa TANESCO Morogoro kwenda likizo yake kutasaidia nini hapo?Naibu Waziri Mkuu, Dk Doto Biteko ametangaza kufuta likizo kwa watumishi wote wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) akiwataka wote wawe kazini kukabiliana na changamoto ya upungufu wa umeme.
Amesema hakuna mtumishi wa Tanesco atatakiwa kwenda likizo wakati huu wa changamoto ya mgawo wa umeme na kwamba, kila mmoja kwenye eneo lake atatakiwa kufanya kazi kwa bidii.
Dk Biteko, ambaye pia ni Waziri wa Nishati ametoa agizo hilo leo Ijumaa, Februari 23, 2024 wakati alipotembelea chanzo cha kuzalisha umeme cha Kidato mkoani Morogoro.
Naibu Waziri Mkuu huyo yupo kwenye ziara kukagua vyanzo vya kuzalisha umeme, kuangalia shughuli za uzalishaji ikiwa ni mkakati kumaliza changamoto ya upungufu wa umeme nchini.
Hatua hiyo ya Dk Biteko imetokana na kupewa taarifa kwamba, Meneja wa Tanesco Mkoa wa Morogoro, kuwa amekwenda likizo.
“Huu ni muda wa kukimbiza kutatua changamoto zilizopo mbele yetu. Nitoe wito kwa uongozi wa Tanesco kuwa hakutakuwa na likizo kipindi hiki ambacho watanzania wanakabiliwa na changamoto ya umeme.
Hakuna likizo tena kuanzia sasa hivi kwenda mbele kwa mtu yeyote anayefanya kazi Tanesco. Nilivyosema Tanesco hamtalala wakati huu wa mgawo nilikuwa naaminisha, haiwezekani tuko kwenye changamoto halafu kuna wengine wanataka kulala.
Sisi wenyewe tunazunguka kila mahali kuhakikisha wananchi wanapata umeme. Katika hili tutachukua hatua kwa aliyeidhinisha likizo n ahata huyo aliyeomba likizo wakati huu ametoa wapi ujasiri,” amesema Dk Biteko.
Wafanyakazi wengine wa TANESCO mtawaonea tu.Kwenye hili yupo sahihi. Tena wafanyakazi wote wa TANESCO walistahili kulipwa nusu mishahara mpaka siku umeme utakapokuwa wa uhakika.