Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
Does he even have the authority to deny them their vacation time?Sasa kama kuna changamoto ya kimfumo kwenye distribution network, inayohitaji uwekezaji mkubwa kutoka serikalini na zaidi ya mwakanmmoja wa matengenezo, kumnyima Mfagizi wa TANESCO Morogoro kwenda likizo yake kutasaidia nini hapo?
Wako madarakani zaidi ya miaka 60 and they haven’t figured out how to solve the problem once and for all!Wafanyakazi wengine wa TANESCO mtawaonea tu.
Kuna matatizo ya kimfumo kutoka serikalini huko.
Serikali inafanya biashara ya umeme kijamaa, haiuzi umeme kwa bei halisi, Zanzibar wana deni sugu la umeme hawalipi, taasisi za serikali zenyewe zina madeni sugu hazilipi, wananchi wanapenda umeme wa bei chee, mifumo ya umeme inachakaa bila kufanyiwa matengenezo.
Umeme ukiwa unakatika kwa sababu hizo za kimfumo, mfanyakazi wa ngazi ya kati au chini TANESCO utamlaumu vipi hapo?
anatapatapa tu huyu chekecheaKuna uhusiano gani wa likizo ya Mtumishi na kukosekana kwa Umeme?
Hana.Does he even have the authority to deny them their vacation time?
These people are so used to operating outside the ambit of their authority and because no one really checks them, they think they can do anything they want!
This country is a hot stinking mess.
Likizo, kwa mfanyakazi, iko kisheria. Vinginevyo, serikali inunue likizo za wafanyakazi wote wanaostahili.Naibu Waziri Mkuu, Dk Doto Biteko ametangaza kufuta likizo kwa watumishi wote wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) akiwataka wote wawe kazini kukabiliana na changamoto ya upungufu wa umeme.
Amesema hakuna mtumishi wa Tanesco atatakiwa kwenda likizo wakati huu wa changamoto ya mgawo wa umeme na kwamba, kila mmoja kwenye eneo lake atatakiwa kufanya kazi kwa bidii.
Dk Biteko, ambaye pia ni Waziri wa Nishati ametoa agizo hilo leo Ijumaa, Februari 23, 2024 wakati alipotembelea chanzo cha kuzalisha umeme cha Kidato mkoani Morogoro.
Naibu Waziri Mkuu huyo yupo kwenye ziara kukagua vyanzo vya kuzalisha umeme, kuangalia shughuli za uzalishaji ikiwa ni mkakati kumaliza changamoto ya upungufu wa umeme nchini.
Hatua hiyo ya Dk Biteko imetokana na kupewa taarifa kwamba, Meneja wa Tanesco Mkoa wa Morogoro, kuwa amekwenda likizo.
“Huu ni muda wa kukimbiza kutatua changamoto zilizopo mbele yetu. Nitoe wito kwa uongozi wa Tanesco kuwa hakutakuwa na likizo kipindi hiki ambacho watanzania wanakabiliwa na changamoto ya umeme.
Hakuna likizo tena kuanzia sasa hivi kwenda mbele kwa mtu yeyote anayefanya kazi Tanesco. Nilivyosema Tanesco hamtalala wakati huu wa mgawo nilikuwa naaminisha, haiwezekani tuko kwenye changamoto halafu kuna wengine wanataka kulala.
Sisi wenyewe tunazunguka kila mahali kuhakikisha wananchi wanapata umeme. Katika hili tutachukua hatua kwa aliyeidhinisha likizo n ahata huyo aliyeomba likizo wakati huu ametoa wapi ujasiri,” amesema Dk Biteko.
Serikali kununua likizo wakati wa crisis itakuwa si mara ya kwanza.Likizo, kwa mfanyakazi, iko kisheria. Vinginevyo, serikali inunue likizo za wafanyakazi wote wanaostahili.
Si bora huko Tabora, njoo Kilimanjaro ndiyo utajua maana halisi ya Tanesco kukata umeme. Umeme kukatwa saa 140 kwa wiki wametuonea huruma.Mkoa wa tabora wanakata sana umeme shida nini haswaa? TANESCO naomba unieleze shida nini?
Hayupo sawa.Kwenye hili yupo sahihi. Tena wafanyakazi wote wa TANESCO walistahili kulipwa nusu mishahara mpaka siku umeme utakapokuwa wa uhakika.
Halafu eti dokta huyo!Hayupo sawa.
Likizo ni haki ya mfanyakazi na sio hisani ya Waziri.
Angekua sahihi kama tatizo.la umeme linatokana na uhaba wa wafanyakazi.
Ila source ya tatizo sio uhaba wa wafanyakazi ni mambo mengine kabisa ambayo hayawezi tatuliwa kwa kufuta likizo.
Kuna PHD na zile PHD za wanasiasa.Halafu eti dokta huyo!
Ana PhD?
Likizo zote zipo Kisheria kwa Wafanyakazi Yeye Biteko ni nani wa Kuzizuia? Biteko na Waandamizi Wenzake Rais Samia na Makamu Mpango wasijifanye hawajui nini hasa kinasababisha Mgawo wa Umeme kwa Watanzania wakati kuna Stock Kubwa tu ya Majenereta ipo na nyingine imewasili nchini.Naibu Waziri Mkuu, Dk Doto Biteko ametangaza kufuta likizo kwa watumishi wote wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) akiwataka wote wawe kazini kukabiliana na changamoto ya upungufu wa umeme.