Biteko afuta likizo zote za Watumishi wa TANESCO

Turudi kwenye sheria za kazi je waziri anamamlaka ya kufuta likizo za wafanyakazi? wataalam wa sheria mtusaidie hasa akina P
 
Alivyokuja Makamba alituambia enzi za Kalemani mitambo ilikufa kwa kufanyishwa kazi bila kupumzika sasa atakayekuja mwingine tusishangae akasema mainjinia wamekufa kwa sababu enzi za Biteko walifanyishwa kazi bila kupumzika🐒
 
Huenda isisaidie maana dhana ya upungufu wa umeme inasababishwa na mpango wa hujuma kukata umeme ovyo na kuhujumu uzalishaji kwa malengo mahsusi. Ni swala la uhujumu ambalo linahitaji kufanyiwa kazi kama uhujumu uchumi na vyombo mahsusi vya serikali.
 
Huyu biteko anazeeka vibaya sana.
Kabla hajawazuia kwa mamlaka niliyopewa namuuliza biteko anao ushahidi kuwa hao wafanyakazi ndio walio saini mkataba wa Richmond, kagoda, IPTL, Dowans na Dpworld?
Au anao uhakika ndio walio beba mijela ya walipa kodi wengine kwenye sandarusi, magunia, vikapu, ktk kashfa za Escrow na Epa?
 
Changamoto zisizokwisha. Watu wataingia na kutoka ofisini, kama kawaida na tatizo litakuwepo tu kama kawaida.
 
NDUMBARO ALIRUDI KUSEMA SORRY..NAPITATU
 
Kufuta likizo sio suluhisho hata.Kuna mzizi haushughulikiwi pale Tanesco ndio unaoleta tatizo.
 
Ina maana Tanzania tumeshindwa kabisa kuweka sawa masuala ya umeme? Huko wenzetu wamewezaje kiasi kwamba haukatiki?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…