Ukiangalia kwa jicho la tatu utaona anae mdharau mtu mweusi ndie huyo huyo yupo kwenye nchi ya watu weusi.
Tena yupo madarakani kwa kutumia nguvu ya silaha ili wawaweke hao watu weusi chini kimaisha na kifikra.
Akimuona mweusi alie taka kuleta maendeleo kwa weusi wenziwe watamuuwa mifano yake ipo. Angeulizwa Botha kama hayo kweli Madela alimuweka kizuizini kwanini?.
Jicho la tatu ukiangalia kama afrika kungekuwa na maendeleo nani angelikwenda ulaya na America?. Jamii ya watu weupe wanatumia nguvu kubwa kukandamiza jamii ya watu weusi ili kuwepo juu.
Gaddafi aliposema ataleta sarafu ya Afrika akiwa kama rais wa umoja wa Afrika kule Addis Ababa kifo kilimfika kutoka kwa hao hao wanao wadharau weusi. Wakijua siku watu weusi wakijiweza nao ndio anguko lao.