Nimehamia nyumba ingine hivi karibuni, ya kupanga. Ni upande wa nyumba, chumba kimoja na sebule. Kasheshe ni jirani wa upande wa pili. Dada mmoja hivi. Hapo miaka ya nyuma kidogo nimewahi kuwa na tabia (mbaya) ya kutembelea maeneo ya burudani ambako wanapatikana 'dada poa', na mara kwa mara nilikuwa namchukua huyu dada. Nimeacha hiyo tabia siku hizi. Lakini tangu nimehamia hapa, huyu dada kuniona tu anaanza tabia ya kunichangamkia sana na kuonesha kunifahamu mno. Mimi naona aibu kuonekana nikiwa nae hasa kwa sababu ya shughuli yake, na pia kwa sababu tabia hiyo nilishaiacha. Lakini alivyogundua namkwepa, ameanza tabia mpya, ya kuja kwangu kuomba hela. Na kwa kuwa sipendi aonekane kwangu, huwa nampa hela anayoomba haraka ili aondoke. Sasa kazoea na naona ananinyanyasa. Majuzi alikuja kuomba elfu 20, nikaona amezidi nikamweleza siwezi kumpa. Akatishia hatoondoka hadi nimpe hizo hela, na nikizidi kumbania atafichua siri yangu. Kusema kweli natishika, na kodi nimeshalipa ya mwaka! Ushauri plz.