Blanketi la ujima liondolewe katika mfumo mpya wa elimu

D-Frank

New Member
Joined
Nov 24, 2018
Posts
2
Reaction score
1
BLANKETI LA UJIMA LIONDOLEWE KATIKA MFUMO MPYA WA ELIMU.
Serikali ya nchi yetu kupitia wizara ya elimu ipo katika maandalizi ya sera mpya ya elimu ambayo inamabadiliko makubwa na kwa kiasi kikubwa imejikita katika kutengeneza watanzania ambao watapata elimu na mafunzo ya mapema ya kuwawezesha kujiajiri tofauti na muundo wa elimu wa sasa ambapo kila mtanzania aliyetaka elimu imsaidie kufanya maisha alilazimika kukaa darasani miaka isiyopungua takribani 15 kuweza kupata mafunzo ya kumwezesha kuwa na kitu kutumikia taifa na tumbo lake.

"UKINYOA UPAA UNAFUKUZWA SHULE"
Kwa sasa Mimi ni mwalimu, na nimekuwa mwanafunzi huko nyuma, nimeuliza kwanini mtoto/ mwanafunzi akija amenyoa upaa anadhibiwa? Majibu hayapo. Ombi na mtazamo wangu;

"TUNU NA MAADILI YA TAIFA VIPITIWE". Kila mtu ni shuhuda kuwa vipawa/vipaji vya watu wengi kwenye nchi zilizoendelea vimepatikana mapema chini ya miaka hata 10 na ndivyo vimejenga maisha yao na ya taifa pia. Tazama watu maarufu na weliofanikiwa katika tasnia mbalimbali duniani, niwataje wachache kama mfano;
VINICIOUS JR
tupac
Michael Jordan
@Mayweither
lil wayne
diamond Platnamz
Jux
Bob Marley
@R. Kelly
Michael jackson
Cr7
Lucky Dube
KIBU Denis

"MUNGU KAUMBA WATU WENYE VITU TOFAUTI, KWANINI TULAZIMISHWE KUFANANA?"

Ukitazama watu wote mashuhiri duniani kila mmoja anakitu chake. Kama Binadamu wote tungeumbwa kama mtu mmoja basi kusingekuwa na 'diversities' katika mahitaji na shughuli tunazofanya, kila mtu angefanya na angehitaji kile mwenzie anafanya na kuhitaji na hivyo kudumaza mnyororo wa kazi na mahitaji. Lakini ukweli ni kwamba maendeleo huja kwa kuwa na mchanganyiko wa shughuli na mahitaji ya watu walioumbwa tofauti.

Ukitizama katika ulimwengu wetu huu mpya, watu wengi maarufu na wenye mafanikio wamefanikiwa kutokana na vitu walivyoumbiwa navyo; mwingine kaumbwa na nywele nzuri,nyingi, ngumu, nyeusi. Mwingine kaumbwa na viungo vya mwili tofauti na mwingine. Mwingine kaumbwa mfupi, mwingine mrefu. Mifano hii ya maumbire na jinsi ambavyo watu wameumbwa ndivyo vimesaidia kufanikisha watu.

Hivyo,si kila mtu aweza kuwa bondia, si kila mtu awezakuwa mchezaji wa kikapu, si kila mtu aweza kuwa mwanamitindo, si kila mtu aweza kuwa mcheza mpira,si kila mtu aweza kimbia riadha. Tazama katika kinachoendelea hivi sasa ulimwenguni katika 'social media' watu wengi wameweza kujipata/kufahamika katika jamii kupitia mitandao ya kijamii sio kwa sababu wamesoma, wengi ni kwa vitu walivyoumbwa navyo, mwingine hata mtindo wake tu wa nywele au uvaaji au michoro katika mwili, au kujengeka tu kwa mwili , au tu sauti yake, vimeweza kumpa maisha/kumfanya atoboe.

"KWANINI KUWEPO SARE MASHULENI? "
Kuweka sare mashuleni ni kuaminisha watoto wetu waweke kichwani wazo kuwa tumeumbwa wa kufanana. Watoto wakijengeka katika 'mindset' hii ni chanzo cha kuminya/ kuzuia tofauti zilizo katika watu. Ukitizama watu wengi waliofanikiwa katika nyanja mbalimbali katika ulimwengu huu, mionekano yao imekuwa sehemu ya safari ya maisha ya mafanikio yao.

Maumbile na mwonekano wa mtu unanguvu pia katika kumwelekeza mtu katika kufanikiwa katika nyanja fulani ya maisha ya mafanikio. Tumefikia mahali katika nchi , mtanzania mwenye dreadlocks anaonekana wa tofauti,ukinyoa panki ni muhuni. Vitu ambavyo ni vidogo mno. Kwa nchi yangu mtu mwenye mchoro "tattoo" mwilini haonekani kama ni mzalishaji na mjenzi wa taifa. Nategemea mjadala huu kupanuliwa kwa maslai ya kizazi kijacho. Mwalimu.
 
muhimu kutunza historia sababu imebeba Utamaduni,sasa unataka tusibaki hata na chembe ya tamaduni yetu?
 
Kwenye Ethics and professionalism ndo ulivyojifunza kuhusu uniforms? Na hao mwenzetu waliofanikiwa wanafunzi wao hawavai uniform?
 
Back
Top Bottom