Bless weekend yako na hizi movies..

Bless weekend yako na hizi movies..

SteveMollel

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2015
Posts
8,797
Reaction score
25,177
Kama si muda kubana, tungaliona thread hii tangu jana (Ijumaa), lakini hakuna kilichoharibika, bado ni weekend so twende na hizi hapa kuanzia usiku huu...

Hii itakuwa ni thread yangu ya nane sasa katika mfululizo wa 'movies to watch'... kama ni mgeni, basi waweza zipitia moja baada ya nyingine ukiwa na popcorn mkononi...

01. NO ESCAPE (2020)

88e85ba7a4c7c16d0c3cf7fe40e13912.jpg

Ushawahi kuitazama SAW? Vema. Na vipi kuhusu ESCAPE ROOM? … kama ndio, hii NO ESCAPE ya 2020 ni mchanganyiko wa maudhui hayo.

Ni movie ambayo haina story 'deep' bali yenye matukio mengi ya kukimbiza moyo na kuumiza kichwa kiasi cha wewe kukalia kiti chako mwanzo mpaka mwisho wake.

Ni hivi … Bwana Cole ambaye ni mwanamitandao maarufu,akiwa anamiliki account anayoitumia kurusha videos zake zenye wafuasi lukuki, yeye pamoja na rafiki zake kadhaa wanaenda 'tour' Urusi.

Huko kuna sehemu mathalani ya gereza, ndaniye kukiwa na 'games' mbalimbali za kufikirisha akili na kutumikisha mwili, lengo la Cole likiwa ni kurekodi kila kinachoendelea akikirusha mubashara kwenye 'vlog' yake.

So shida ilikuwa ni 'content'.

Sasa tatizo linakuja pale ambapo Bwana Cole na wenzake wanapoanza kuhisi 'game' inakuwa 'too real' kila wanaposonga mbele!

Kila hatua wanayopiga wanajikuta maisha yao yakiwa hatarini na hata miongoni mwao kufa! … mbele ya macho yao game inakuwa si game tena bali mapambano ya kupigania uhai … hamna tena kutafuta ushindi, bali kuhaha kwa kila namna, kwa kila njia iwezekanayo kubakiza pumzi!

Kila chumba na mtihani wake. Kila mtihani na tofauti yake.

Kila chumba kikidai kwanguvu kuondoka na maisha ya mmojawapo.

Kazi haikuwa ndogo.

02. THE LAST LAUGH (2020)

The-Last-Laugh-1.jpg

Bwana Myles ni 'Comedian' ambaye ameshasota sana. In fact, shows zake ni za 'mchangani', zile ambazo hazina 'impact' kubwa wala pesa ya maana.

Mbali na hilo ni 'mshikaji' anayesumbuliwa na mahusiano. Ameachana na mpenzi wake si muda mrefu kiasi kwamba hayupo sawa kiakili hivyo analazimika kutumia vidonge hapa na pale ili kichwa chake kikae sawa.

Basi katika harakati zake za kutafuta pa kutokea, Bwana Myles anakwaa nafasi mujarab ya kuonyesha kipaji chake … 'show' kubwa kabisa ya comedy! … show ambayo anaamini kwa kila kiungo cha mwili wake ndiyo itakuwa mlango wa yeye kumtambulisha ulimwenguni!

Lakini kinyume kabisa na matarajio hayo makubwa, kufumba na kufumbua, show hiyo inageuka kuwa mahangaza pale anapokuta mwili mfu ndani ya chumba chake cha maandalizi!

Akiwa bado yu kwenye butwaa … hajapata hata ufumbuzi wa hilo … anajikuta akishuhudia mwili mmoja baada ya mwingine kila baada ya muda fulani, ikiwa imelala mfu kabisa! Na huku anayefanya mauaji asijulikane ni nani na anataka nini.

Sasa hapa Bwana Myles anajikuta akiwa katika njia panda ya maisha yake. Je, aendelee na show yake aliyokuwa anaitamani na kuingoja kwa muda mrefu huku akijifanya hajui kinachoendelea ndani ya ukumbi, au amsake muuaji na kisa chake?

03. THE PALE DOOR (2020)

c046b954f2c83750a905f9d31c424e38.jpg

Jake na Duncan ni watoto wawili wa kiume waliotiwa uyatima na majambazi walioua familia yao na kuteketeza kabisa makazi yao kwa moto. Bahati nzuri waliokoka.

Miaka kadhaa mbele wanakuja kukutana na genge la wahuni linaloitwa Dalton. Genge lenye mkakati wa kuivamia treni kwa ajili ya wizi lakini wakiwa na tatizo la upungufu wa watenda kazi baada ya kumpoteza mwenzao kwenye mapambano ya risasi.

Kutokana na hilo, Jake na Duncan wanajiweka katika kundi hilo na kuhusika kwenye mpango wa utekaji treni ambao unafanikiwa kabisa isipokuwa kwenye mambo mawili.

Moja, droo wanayoiba wakitumai ndani yake ina dhahabu, wanamkuta humo msichana mdogo anayejitambulisha kwa jina la Pearl! Msichana huyo anasema alichukuliwa kutoka mji wa Potemkin na endapo akirejeshwa nyumbani basi zawadi nono itataolewa kwa waliohusika.

Pili, Duncan amejeruhiwa katika zoezi hili na hivyo basi inabidi apate huduma upesi kama kweli wanataka kuokoa maisha yake kwa dhati.

Kutokana na hayo, genge la Dalton linalazimika kufunga safari kuelekea Potemkin. Huko wanakaribishwa kwenye danguro na mwanamke aitwaye Maria … Maria pamoja na wenziwe wanawakarimu vema wageni wao kwa pombe na mapenzi …

Lakini ni swala la muda tu, kundi hili linakuja tambua kuwa limejileta lenyewe kuzimu …

Kila kitu kinabadilika mbele ya macho yao…

04. THE ROOM (2019)

5517233d8396fc73516b2b8ae0418a20.jpg


Matt na Kate ni wapenzi wachanga ambao wanahamia Westminster, Maryland, baada ya kununua jumba kubwa huko lililojitenga. Basi wakiwa wanafanya marekebisho ya makazi yao mapya, wanabaini kuna mlango mkubwa wa chuma unaoingia kwenye chumba kikubwa kitupu.

Hawajui chumba hiko ni cha nini na kwanini kimo humo.

Mbali na hivyo katika makazi yao kuna matatizo ya hapa na pale ya umeme kiasi kwamba wanalizimika kumuita fundi aje kurepea … fundi anakuja na kufanya kazi yake vema lakini kabla hajaondoka anaacha kauli akistaajabu makazi hayo yamepata wateja kwani wakazi wake wa awali waliuawa humo!

Bwana Matt anapata kizungumkuti. Usiku halali akinywa na kutafakari kumhusu muuaji … anafanya utafiti wake na kubaini jina la muuaji ni John Doe, na bwana huyo yupo hai katika hospitali ya wagonjwa wa akili.

Bwana Matt, akiwa ndani ya chumba kile kitupu, anaendelea kunywa na mwishowe akajikuta akitamani apate chupa nyingine ya kileo … basi akaropoka... staajabu, ikatokea chupa nyingine kama ile aliyoigida!

Hapo ndo' akatambua kuwa chumba hiki si cha kawaida.

Yeye na mkewe wanaomba pesa lukuki na hata kufikia kuacha kazi kabisa. Shida nini na pesa zipo? Lakini zaidi ya yote, mwanamke anashida moja kuu, nayo ni shida ya mtoto. Alishawahi pata mimba mbili lakini zote zikaishia kuharibika!

Sasa anashawishika kuomba mtoto kwa kupitia chumba hiki japo kuna mzozo baina yake na mumewe.

Mbali na hapo, bwana Matt anafika hospitali kuonana na John Doe ili kupata kujua kuhusu nyumba waliyomo na visa vyake lakini hapati taarifa anazozitaka, badala yake bwana John Doe anampa onyo kuwa ahame hapo mara moja na wasahau kabisa kuhusu kile chumba na kila kitu chake!

Bwana Matt akiwa anarudi nyumbani, anabaini pesa aliyoweka mfukoni, yaani moja ya pesa ambazo zimetoka kwenye kile chumba, imegeuka kuwa jivu!

Anatahamaki.

05. MEMOIR OF A MURDERER (2017)

ecdcb1feba4b67e65f0f969f75216c9d.jpg


Kipindi hiko cha zamani, Bwana Byung aliwahi kumuua baba yake kutokana na kuwa mzazi 'abusive' sana kwake. Na kwa hilo hakujutia hata kidogo, badala yake ndipo akajenga imani kuna baadhi ya watu wanastahili kabisa kifo kutokana na ushenzi wao.

Na kuanzia hapo, bwana huyo akawa na mfululizo wa kuua watu kadhaa akienda kuwafukia kwenye shamba lake la mianzi lakini ikafikia pahala akaacha kabisa hilo zoezi baada ya kupata ajali iliyomlazimu kuishi maisha ya kawaida na binti yake.

Zaidi ya hapo, ajali hiyo, hapo baadae inabainika kumsababishia ugonjwa wa 'Alzheimer' - ugonjwa unaokula ubongo wa binadamu kadiri muda unavyoenda mbele kiasi cha kupoteza kumbukumbu kwa kiasi kikubwa!


Sasa shida inakuja pale ambapo mfululizo mpya wa mauaji unapotokea katika mji aliopo Bwana Byung … Bwana huyo anapata mashaka kuwa huenda mauaji hayo akawa anayafanya yeye kutokana na kutoamini akili yake ipotezayo kumbukumbu kila saa.

Lakini anapokutana na bwana aitwaye Tae-ju, akili yake nzima inamshuku bwana huyo kuwa ndiye muuaji (waarabu wa pemba hujua kwa viremba). Anaripoti polisi lakini anastaajabu kumbe bwana huyo ni polisi pia!

Anahaha kusaka ushahidi wa kumtia bwana Tae-ju kwenye mikono ya sheria lakini pasipo kujua, anamuingiza bwana huyo kwenye maisha yake kwa kuanza kumfuatilia binti pekee wa Bwana Byung! … kazi inapamba moto.

Sasa Bwana Byung anajikuta akilazimika kutumia akili yake yote (kumbuka hapo ana ugonjwa wa kusahausahau) ili kumnusuru mwanae toka kwenye mikono ya muuaji Tae-ju.

Je, kipi atakachokuwa atakachokuwa anakumbuka toka enzi zake?

Ukitazama mpaka mwisho wa movie hii, utakuja gundua kumbe muda wote huo ulikuwa hujui.

----

Ukitaka kupakua movies hizi for free, nakuwekea link ya Telegram channel. Zama upakue uwezavyo!

Movies Na Stories
 
Mkuu, tufanyie mpango wa exam na pet semetary
 
Mkuu naomba msaad wa kunitajia muvie ambazo mwanzo mwisho wahusika wakuu wasizidi wawili..
 
No escape ni movie nzuri sana. Pia waongozaji wake ni level flani hivi kubwa dunia

Zipo kama "Final destination"
 
Nataka series au movie based on true event au story .. iwe crime, upelelezi au yoyote
 
Back
Top Bottom