BLUMHOUSE - Wakali wa movies za kutisha duniani

SteveMollel

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2015
Posts
8,797
Reaction score
25,177

Ukiona hii chapa, basi ujue humo ndani sio drama, mapenzi wala vita. Hawa jamaa hawana mambo hayo. Hawa wameletwa duniani kwa kazi moja tu, kuwafurahisha wapenzi wa 'horror' na sie tunawashukuru mno kwa hili.

Hizi hapa ni baadhi ya kazi zao, ukipata muda basi jikonge na roho yako.


1. HAPPY DEATH DAY

Baada ya usiku mrefu wa kunywa na kuparty, mwanafunzi wa kike (Tree) anaamka kwenye chumba cha mwanafunzi wa kiume ambaye hata jina hamfahamu.

Kichwa kinamuuma kwa hangover na leo ni birthday yake.

Anatoka humu chumbani akiwa haelewi lakini kabla hajafanya la maana, anauawa kwa kisu na mtu aliyevaa kinyago. Ajabu anaamka tena palepale, ndani ya chumba kilekile pembeni ya mwanafunzi yuleyule, na akiwa anakumbuka kitu kilichotokea hapo nyuma.

Muda si mrefu anabaini muuaji bado anamuwinda na kila anapokufa anaamka tena palepale. Njia pekee ya kujinusuru ni kumjua muuaji ni nani na amuwahi kabla hajawahiwa la sivyo mzunguko huu wa kuuawa na kuamka tena hapa, hautakaa ukaisha.

2. INSIDIOUS

Baada ya tukio lisiloeleweka, mtoto Dalton anapoteza fahamu kwa muda mrefu. Si hospitali wala muaguzi anayeweza kumsaidia.

Wazazi wake wanakata shauri ya kuonana na mtaalam wa mambo ya kiroho na inapotazamwa inabainika mtoto amekwama kwenye ulimwengu wa pili. Namna pekee ya kumrejesha kwenye ulimwengu wa kawaida ni mmoja kwenda kumfuata huko aliko.

Hili zoezi si jepesi. Ulimwengu huo unatisha, na ukienda huko hauwezi kurejea tena katika hali yako ya kawaida.

Kama ni mwoga, kaa nazo mbali hizi.

3. TRUTH OR DARE

Wanafunzi nane wanatembelea eneo fulani lenye historia ya vifo vya watu saba huko zamani. Wanaenda hapo kama sehemu ya kufurahia weekend ya Halloween.

Lakini muda si mrefu mambo yanabadilika wanapoanza mchezo wa "truth or dare". Humu unapewa options mbili, kujibu chochote utakachoulizwa ama kufanya chochote utakachoambiwa.

Mwanzo wanachukulia hii ni game ya kuchangamsha genge ila si muda watu wanaanza kufa wanapojibu uongo au wanapokataa kufanya wanachoambiwa.

Na ubaya huwezi kuacha kucheza, napo ukiacha unakufa.

Siri zinamwagika na pia watu wanakwisha.

Nani anayewaua na anataka nini? Mzigo wa kwenda huo hapo.

4. GET OUT

Nigga mwenzetu anaona amepata baada ya kuwa na demu mzungu. Wanadumu kwenye mahusiano kwa muda na sasa mwanamke anamwalika kwenye mtoko wa pamoja na wazazi wake ili wapate kumjua vizuri.

Asichojua nigga mwenzetu huu ni mtego, na hawa wenzetu huu ndo mchezo wao. Wanakuvuta kwa gia ya mapenzi kisha ukijaa, wanakuonyesha kazi.

Sasa mtoko wa mapenzi unageuka vita ya kujinusuru. Mwana anataitishwa kwenye kisanga cha aina yake.

5. HUSH

Sema kuna watu wanayapenda matatizo na mmoja wapo ni huyu mwanamke Maddie.

Anajijua kabisa ni kiziwi na pia ni bubu lakini anaamua kujitenga na watu. Anaenda kuishi zake huko porini kwasababu eti anahitaji utulivu kwenye kazi yake ya uandishi.

Sawa, anaupata huo utulivu, lakini si muda anapata na mengine. Bwana mmoja mwenye kinyago na silaha anamvamia na sasa anapata kazi kubwa ya kujiokoa.

Zingatia yuko porini. Zingatia hasikii na hana uwezo wa kuzungumza, maana yake hata simu ni bure.

Sasa anajiokoaje? Cheza na anga hizo.

6. M3GAN

Kwenye kampuni hii kubwa ya teknolojia, boss hataki kuelewa, anachotaka ni wafanyakazi wake waumize kichwa na kuja na project ya maana itakayoteka soko la watoto kwani ushindani ni mkubwa sana.

Basi Gemma, mdada ambaye ni mfanyakazi wa hii kampuni, kwa kutumia akili yake kubwa anatengeneza roboti inayoitwa M3GAN. Roboti hii ina uwezo mkubwa wa kumlelea mtoto, tena zaidi ya binadamu.

Sasa Gemma anapojikuta anatakiwa kumlelea mpwa wake ambaye hayuko sawa, anaona ampatie roboti M3GAN ili kumsaidia.

M3GAN anamsaidia sana lakini kuna kitu hakipo sawa. Roboti huyu anaichukulia kazi yake serious mno. Chochote kinachokuja mbele yake kwenye shughuli ya malezi, basi hakirembi, anakitokomeza mara moja!

Si jirani, si watoto wengine. Miili inaokotwa.

Gemma anajikuta akipambana na ushahidi na huku akipambana na M3GAN ambaye anapendwa mno na mpwa wake.

Weeh! Cheza na button hiyo.

7. SWEETHEART

Baada ya boti yao kukumbwa na dhoruba na hatimaye kuzama, Jenn anakuja kupata fahamu akiwa amesukumiwa na mawimbi kandokando ya bahari iliyozunguka kisiwa.

Kuangaza anakutana na mwenzake akiwa amejeruhiwa vibaya sana. Anajaribu kumsaidia lakini hafanikiwi na kabla ya kufa majeruhi anamuuliza "umemwona?"

Hajui amemwona nani.

Anapofanya doria katika kisiwa hiki anabaini kuna makaburi ya watu wengine walofia hapa, lakini hajui kilichowaua nini, ila inapofika usiku ndo' anakuja kupata majibu yote.

Hapa kisiwani, hayupo mwenyewe. Kuna kiumbe kinachokula samaki na pia binadamu.

Sasa ni jukumu lake, kubaki hai ama kulegea na kuliwa.

Hajakaa sawa, watu wengine wanaibuka hapa kisiwani. Utawaambia nini?

Shughuli inapamba moto. Hamna pa kukimbilia na usiku ukivuka unashukuru Mungu.

8. THE PURGE

Idea ya The Purge na mifululizo yake iko very straight. Katika kipindi ambacho uhalifu umeongezeka na hata magereza yamekuwa yakizidiwa wahalifu, serikali inaweka azimio hatari.

Ambapo inatengwa usiku mmoja, usiku ambao hamna sheria yoyote. Kila kitu kinaruhusiwa, hata kumuua mwingine.

Sasa usiku huu unakuwa hatari mno maana hamna pa kukimbilia na hamna wa kumpigia simu. UKO MWENYEWE. Na wahalifu wanagonga mlangoni ama wanavunja ili kuja kukumaliza kabla muda walopewa haujaisha.

9. THE HUNT

Watu kumi na mbili wanaamka mahali wasipopafahamu na hata hawajui wamefikaje hapo.

Wakiwa wanajitafuta, wanashangaa kikundi cha watu wenye silaha za kila aina kinawashambulia bila ya huruma!

Kikundi hiki ni cha watu wenye pesa na ushawishi katika jamii na hufanya hivi kama sehemu ya mchezo unaowaburudisha, kuwinda binadamu.

Sasa wanaowindwa wanahaha kujiokoa humu ndani na wakati huo wakihaha kuwajua watu hawa ni kina nani.

Muda si muda, wawindaji wanageuka kuwa wawindwaji. Hawakujua moja ya mtu walomteka ni 'waya ya stimaa' (kwa sauti ya dj Afro).

Tembea na reli hiyo.

10. UNFRIENDED.

Wakiwa mtandaoni wanachati, marafiki sita wanaosoma shule moja, wanakutana na kitu cha ajabu. Mmojawao anapokea ujumbe kutoka kwa mwenzao ambaye alishawahi kufariki huko nyuma.

Anawajuza wenzake ila wanaona kama utani. Wanadhani kuna mtu anawachezea, lakini muda si mrefu mtu huyo anayewatext anaanza kuua mtu mmoja baada ya mwingine huku wenzake wakishuhudia online.

Mauaji haya ni ya kisasi.

Ila ni nani anayeua na kwanini? Utajulia humu ndani.

11. YOU SHOULD HAVE LEFT

Ndoa ya Bwana Theo ina matatizo. Ameoa mke dogodogo na mrembo (Susana), basi wivu haumuachi akahema.

Lakini mbali na hayo, bwana huyu anaibeba siri ya kifo cha mke wake wa kwanza ambaye alikufa kiutata. Japo mahakama ilisema hana hatia, yeye mwenyewe anajua ni nini kilitokea.

Sasa ili kuanza upya, Theo na Susana pamoja na mtoto wao wanaenda vacation huko mbali, kwenye nyumba kubwa na nzuri iliyo mbali na mji.

Huko wanafurahia mazingira na utulivu, lakini si muda mambo yanaanza kubadilika. Kuna mtu ama kitu kinawafuatilia humu ndani.

Na ubaya kinafahamu siri ya kila mmoja
wao hata zile ambazo wao wenyewe hawajapata kuambiana.

Hivyo safari ya kuanza upya inageuka kuwa safari ya kifo.
 
Dah we jama ni noma aisee, nimekukubali sana man, mimi ni mpenz sana wa horror movie hata hyo kampuni kweny muv za kutish ni noma pamoja na LION GATE endelea hvo hvo jombaa ngoja nikazisake hzo tambala kali sn
 
Dah we jamaa unakipaji cha kusisimsha akili ya msomaji. Unafaa kuwa na kipindi cha kuelezea movie na kufanya watu wawe na interest ya kuitafuta na kuitazama.

Unanikumbusha miaka ya 1990's kulikuwa na Dada m'moja pale ITV alikuwa anaitwa Manuel kama sio Emanuel Elias, alikuwa anatangaza ratiba ya kipindi kinachofuatia.

Sasa nilikuwa napenda sana akiwa anatoa utambulisho mfupi wa kifuatacho especially movie yaani the way anavyosimulia kwa ufupi anakupa ushawishi wa kuacha kila kitu kutulia na kutazama hiyo movie aiseee na lazima utaipenda.

Nakumbuka alikuwa anaielezea movie ile ya Van damme ya cyborg al maarufu "Van damme Msalabani".

Aaaah aiseee anakupa mzuka balaa.
 
Dah we jama ni noma aisee, nimekukubali sana man, mimi ni mpenz sana wa horror movie hata hyo kampuni kweny muv za kutish ni noma pamoja na LION GATE endelea hvo hvo jombaa ngoja nikazisake hzo tambala kali sn
Hao nikiwaonaga tu, nasema sasa hapa nimefika. Ahsante sana mkuu wa kambi.
 
Ahsante sana kaka, na mimi nafanya yote haya just for hobby. Hamna ninachoingiza wala kupata but I just enjoy it.

Huku navizia vizia kupost, karibu na Telegram kaka.
 
Mkuu kiufupi we ni hatari unajua sana kuchambua movies aiseee yaani hatare mno..

Naomba kama ushawahi icheki hii immaculate ya yule sister naomba uelezee pia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…