BM Coach: Rekebisheni haya

BM Coach: Rekebisheni haya

CORONAZ

Senior Member
Joined
Apr 26, 2020
Posts
181
Reaction score
341
Nikiri kuwa nimekuwa mpenzi wa BM Coach kwa muda mrefu sasa ila hili la safari hii limeanza kunichefua.

Alhamisi ya tarehe 07/09/2023 nilisafiri na basi la 1.30 asubuhi. Mshangao wa kwanza ni kutokuta basi nililoahidiwa kwenye tiketi kwa kiwango cha nauli. Nilikata basi la 40,000 likaja la 37,000. Wakaomba radhi wakaturudishia 3,000 tukapotezea.

Kurudi 10/09/ 2023 Basi linalopita moshi saa 3 asubuhi jambo lile likajirudia bila hata samahani. KIBAYA ZAIDI HATA CHENJI YEU HATUKUPEWA. Hatujui ni mmiliki/meneja/ au konda aliyepita na chenji yetu. MZEE ANGALIA WATU WAKO. Namba zetu wanazo. Watupe chenji zetu.

Jambo lingine baya ni kuanza kujaza watu. Haswa hapo mbele....tukiwauliza mara oo ndugu wa askari, mara oo staff...haina hata maana kukata siti za mbele... unaishia kuangalia vichogo vya watu.

Lililonitia shaka ni hii biashara ya vifurushi pori anavyopewa konda kabla ya kuondoka na watu wanaomsubiri njiani kumpa na kupokea.... MZEE BM angalia magari yako yasigeuzwe punda wa unga.... vifurushi vipite ofisini. Waache njaa.

La mwisho. Simu za madereva. Ni nyingiiiiii. Kusogoa njia nzima. Wapunguze...ndio zibaki zile muhimu na zingine awaambie tu , nadrive...niakupigia... watu watakuja pokea simu za msiba watubwage....ohooo...

Au mpaka tupeleke ushahidi LATRA? Ya nini yote hayo?
 
Well said
 
Panda Marangu
 
Ni fursa kwako kuanzisha kampuni bora ya usafirishaji ambayo haitakuwa na kasoro pia utapata wateja wengi.
Unapoona apungufu kwenye biashara ya mwenzio sema ili arekebishe/aboreshe. Utafanya biashara ngapi?
 
Mimi kwenye basi sifuati U luxury bali kufikq nako enda,Hakuna cha luxury kwenye basi ni usanii mtupu
Mkuu yapo mabasi siku ukipanda utajua ukweli kuwa yapo mabasi wakati wengine wanalipisha elfu 40 wengine hata elfu 25 unaenda ila unyamaze....mpaka vigoda vipo. Haachi mtu.
 
ukitaka usisumbumbuke kwenye hizi huduma za "public" hakikisha umepata "private"

tunaishi katika ulimwengu wa tatu, mambo ni mengi.

anyway, pole kwa usumbufu mkuu!
 
Tunaikumbuka Fast Jet, ilikuwa mkombozi kwa wasafiri wengi
 
ukitaka usisumbumbuke kwenye hizi huduma za "public" hakikisha umepata "private"

tunaishi katika ulimwengu wa tatu, mambo ni mengi.

anyway, pole kwa usumbufu mkuu!
Nashukuru kwa pole. Private ninazo ila swala la upaikanaji wa mafua bora mafuta lilinisukuma kwenye public. Pia sikuwa na uharaka wa safari.
 
Pole sana bro! Kuna kenge wengine wapo Dodoma wanaitwa Chiloha,nilipanda basi lao juzi kutoka Dar, kwenda Dom, kwanza wezi, unakatiwa tiketi ya mkono 28000,ukiingia ndani, unapewa ya ki electronic inaandikwa 26000! Abiria wengi hawakushitukia hii, mpaka Kati ya safari, mzee mmoja akauliza, alijibiwa kihuni na konda!
Basi linatembea na ma konda kama watano, wanaongea kihuni, maneno ya hovyo sana, yaani kama umekaa na Dada yako, mama, baba, ni aibu tupu!!
Washenzi sana mbwa wale!
Ukitaka safari zenye staha kwa Dom, Dar, mbeya, panda shabiby au ABC
 
Ni fursa kwako kuanzisha kampuni bora ya usafirishaji ambayo haitakuwa na kasoro pia utapata wateja wengi.
Kwa hiyo nchi ikiwa na matatizo anzishe nchi yake?
Sio kila changamoto utaigeuza fursa.
Wenye kampuni waboreshe huduma zao.
 
BM n moja kati ya usafir mzur sana na uhakika.weledi na umahiri wa safari zao hasa dar to arusha

Kuanzia usafi,customer care,bus lenyewe,kujali muda na ufanisi/uzoefu wa madereva (ajali zake n mara chache mno)

Nawasihi wasipuuze maoni ya wateja wao…
 
Back
Top Bottom