BMW X1 aka Baby BMW SUV

Nadhani hujakutana au hujasikia engine mbovu za BMW kama N20, N47 (four) n.k
N43, N46 na N54....

Ukimiliki Gari ina N54 ni kama unamiliki ndege ndogo.

Huko barabarani watakujua, Utanyanyasa gari nyingi sana na hiyo twin turbo inline 6 ila safari za garage hazitokauka.

Ukitaka kuifanya hiyo engine iwe reliable utahitaji kuinvest kiasi kikubwa sana cha pesa.
 
Timing Chain wanashauri kureplace at around mileage ya 140k au 9 years.

N20 nyingi zinafeli kabla ya 100k, Hiyo Chain, guides zake, tensioner, n.k. kibongobongo uwe na 1m.
 

Nilichooverprice hapo ni Oil filter tu, Gari za BMW zinakuwa na Oil filter housing ambapo ndani yake ndio unaikuta Oil filter.

Gari yenye filter hii ndio unanunua kwa 30k au 35k.

Ila ikiwa zile filter ambazo haina hauzing yaani ni moja kwa moja kama ilivyo kwenye toyota nyingi. Basi kwa mjerumani ujiandae 60k to 65k.

Wauza spareparts watakuja kunisahihisha.
 
Duuh. Nimeona N52 nyingi kwenye X1 ni 3000 cc. Naitamani sana X1 kwa sasa nina N46 kwenye e90 ila sijavutiwa na performance yake. Kuna mdau ana N43 kwenye e90 ukigusa tu imeruka fasta.
N43 ni nzuri japo siyo reliable kama N46.

Tafuta e90 ya Cc2500 Bonge Moja la gari tena upate kuanzia 2008 iko facelifted. Utafurahi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…