BMW X1 aka Baby BMW SUV

BMW X1 aka Baby BMW SUV

Katika engine zote za Hii gari, N20 ndio engine Kimeo namba moja, Na ndio nyingi zimejaa mtaani. Except N20 zilizozaliswa kuanzia 2015.

Tatizo common kwenye hiyo engine ni Timing Chain. Timing chain mpya unaendesha haitoboi 100,000Km inakuwa imeshastretch. Inaanza kutoa whinning noise.

Kifuatacho timing inahama, engine inakufa, ukifikiria kununua engine nyingine unakutana na bei mlima kana kwamba hiyo hela inatosha kununua Toyota IST.

Hii ishu ya timing Chain ni common kwenye gari nyingi sana za Ulaya na mbaya zaidi karibu kila gari ina mlio wake wa timing chain(Siyo mlio common kwa gari zote). Mimi mtu akija kufanya service kwangu huwa namshauri tutoe top cover tuangalie kama Chain imeanza kulegea. Aanze kujipanga taratibu.

Ushauri wa mwisho mtu akitaka kununua Euro cars aachane na engines ambazo watu walishaburuzana mahakamani mfano hiyo N20.
Mkuu ebu tupe habari za Volkswagen Touareg. Naipenda sana na nishaiweka mkononi nimetoka kwenye crown nimehamia huko, honestly inachonivutia ni ule muonekano wa kibabe na ile mashine uko barabarani ukiituma inakupa majibu yaleyale unayotarajia ni mwaka sasa haijawai nipa shida yoyote, kuna uzi flani niliuona kuna jamaa alizifia sana Touareg alinihamasisha
 
Toureg ya mwaka gani au toleo gani?

Na engine gani au Cc ngapi?

Diesel au Petrol?
 
Toleo la 2006, petrol engine, cc 3200
Achana na 3.2L. Matatizo ni mengi main likiwa Timing Chain.

Kama unaweza kujivuta sogea tu kwenye 3.6L FSI. Difference kwenye consumption ni ndogo pia hii inakupa more power.

Kitu kingine, kama unaweza sogea 2007 upate version ambayo ni Facelifted.
 
Mpinzani wake mkubwa ni B- Class.
412074b3e9cc4209b7916f68c1798922_750x420.jpg
 
Katika engine zote za Hii gari, N20 ndio engine Kimeo namba moja, Na ndio nyingi zimejaa mtaani. Except N20 zilizozaliswa kuanzia 2015.

Tatizo common kwenye hiyo engine ni Timing Chain. Timing chain mpya unaendesha haitoboi 100,000Km inakuwa imeshastretch. Inaanza kutoa whinning noise.

Kifuatacho timing inahama, engine inakufa, ukifikiria kununua engine nyingine unakutana na bei mlima kana kwamba hiyo hela inatosha kununua Toyota IST.

Hii ishu ya timing Chain ni common kwenye gari nyingi sana za Ulaya na mbaya zaidi karibu kila gari ina mlio wake wa timing chain(Siyo mlio common kwa gari zote). Mimi mtu akija kufanya service kwangu huwa namshauri tutoe top cover tuangalie kama Chain imeanza kulegea. Aanze kujipanga taratibu.

Ushauri wa mwisho mtu akitaka kununua Euro cars aachane na engines ambazo watu walishaburuzana mahakamani mfano hiyo N20.
Well said Jitu. Uko deep sana kwenye haya mambo!
 
Unashauri vipi kwa N47 kwenye F10 520d kuanzia 2012 mpaka 2016? Kama timing chain iko fixed.
 
Hii ni Crossover SUV, Tena ni subcompact Luxury cross over kutoka BMW, Yani Baba Mama Watoto walitaka kupata SUV ndogo na luxury inayotumia mafuta vizuri ndo X1 akazaliwa, saa andaa kifungua kinywa then kaa nikupe madini ya hii gari..

2009 ndo BMW X1 amezaliwa na alitambulika kama moja ya SUV ndogo toka BMW chini ya X3, lengo ikiwa gari itumike kwa familia changa ambazo bado kipato hakijasimama ndo Maana kibei uki compare na gari za Juu za BMW iko chini + inatumia mafuta vizuri.

X1 one as we speak Ina Generation 3 tu G1 ikianza 2009-2015, G 2 2016-2022, G 3 imetoka mwaka jana Mwezi wa 6 hii tuachane nayo kwa leo maana bado ni yamoto sana. So nitakuguisa G1 na G2 kwa uchache sana Maana wengi tunadondokea G 1 [2009-2015].

View attachment 2626085

X1 ina luxurious interior ikiwa na dashboard Sawa na 3 Series [Ile BMW kama tax] + Wanashare Platform. Dashboard sitaweka maneno sana nafikiri Wajukuu wa Hitler mnawajua na hawa ndo wanatengeneza na za audi so ziko advanced na clusters zake zimekaa vizuri plus mpangilio wa rangi unaovutia, Infotainment iko safi.

Mziki wake [audio system ] hauhitaji booster upo wa kutosha 8-12 Speakers pia baadhi zina sunroof. Legroom ipo ya kutosha mtu mrefu au mnene anakaa kwa uzuri kabisa, hata kichwa kinakaa vizuri, Hapo Kwenye kichwa ni muhimu maana kuna wadau wana shingo ndefu kwenye bumps huwa wanagusa roof au wale warefu kuanzia kiunoni.

Seat za nyuma nazo ziko poa watu watatu wa kawaida wanakaa vizuri tu legroom iko safi. Kama ni wanene sana kaeni wawili hala pale kati mnashusha cha kuegemezea mkono [center box] mnakua comfortable kabisa.

Ndani ina sehemu za kuhifadhia vitu vidogo dogo kama hand bags za kutosha tu [cabin storage] na seat jacket. Ina cup holders 4 yani kama uko na mama anapiga Fursana na wewe juice ya mzabibu basi inakua safi.

Kuna sehemu za kuzipachika na sio kuzishika mkononi muda wote, Mama anafika mikono inauma kisa alikua ameshika Juice ya Fursana.

Nyuma boot ipo ya wasitani Mizigo ya extended family haitoshi, ni single family tu kama una extended family basi kuna option ya kulaza seat ili kupata extra boot space.

Muonekano wa nje iko na sport look ya kibabe flani hivi ikiwa na umbo kama hatchback Wameipa grill za mbele kubwa kama X3 zikiwa na LED headlights kitu kinachoifanya iwe na uso mzuri...

Umbo lake sio refu wala box lipo kama komwe la slay qn mkibosho [sleek profile} hivi likiwa smooth na sport look.

Gari imekuja na engine option kadhaa zikiwa coded N20 na N46 2.OL 4 cylinder na mkubwa wao N55 3.0L Inline 6, Hii engine kubwa gari nyuma/pembeni utakuta imeandikwa X DRIVE 25I na nyingi zinakua ni All Wheel Drive..

N20 na N46 unaona zina ujazo sawa 2.0L utajiuliza tofauti zake ni nini, utazijua ndani dk 1 na ipi ni nzuri. Iko hivi N20 kwanza ni advanced engine kuliko N46 nikimaanisha iko na technology za kisasa zaidi na ina better fuel economy.

Hapa ni vitu kama direct injection na turbo charge plus ina nguvu zaidi 154-240 Hp [Ina turbo] wakati N46 ana 148-150Hp [inavuta hewa kawaida tu].

Turbo kwa lugha nyepesi ni mfumo wa uingizaji hewa kwenye engine ili kuongeza mchomo na kuipa engine nguvu zaidi, tuendelee.

So the best engine ni N20 then ndo anafata N46, utajiuliza nitajuaje kikubwa angalia engine code utaziona hizo code hapo. Pia kuna ambazo Pembeni/nyuma zimeandikwa S DRIVE 18I [hii ni N46] na S DRIVE 20I [hii ni N20]...

HIzi engine zote ziko linked na 6-7-8 Speed Automatic Transmission, Kwenye gear wajukuu wa Hittler huwa wanacheza vizuri. hizi gearbox zinafanya gari inakua na speed + ina-changanya faster Ikiwa na smooth shifting.

Na ukipata sport mode yenye paddle shifter na ukajua kuzitumia uta-enjoy sana. Mafuta inatumia vizuri sana kwa mkanyagaji inakupa kama 11-12Km/L.

Ukiwa mtu wa speed za 60- 80 na smooth acceleration unaweza kula hata 13++Km/L. na ull tank ni 51 Litres, kwa hizi latest Zinakula mpaka 61L, na acceleration yake inategemeana na engine ila zinarange 6.5Sec-7.7Sec from 0-100Km.

Ile Engine kubwa N52 5.5Sec 0 to 100 na hii N55 engine kubwa kama hutaki nguvu na speed achana nayo, gari top speed ni 260Km/hr ingawa kuimaliza ni mtiti na barabara zetu.

Kama una njia mbaya hasa za utelezi chukua X Drive, Hii inaendesha tyre zote 4 [AWD], X ina mfumo unao control distribution ya torque [kutokana na uhitaji] kati ya tyre za mbele na nyuma [inatumia sensor]. Ila kama uko town tumia Sport Drive inaendesha FWD inakufaa kabisa.

Gari iko very stable barabarani hasa kwenye kona, mtu wa safari itakufaa sana. Ukitia familia na mzigo inakaa barabarani ikiwa speed inageuka bata inaatamia barabara mwenyewe utapenda.

Parts za gari bei iko juu kimtindo ila vinadumu, ukifunga umefunga yani inshort Hii gari unaimudu vizuri tu bila tatizo, kama unaipenda usiiogope ni gari ya kawaida tu.

Binafsi kuna watu nimewaletea wana kipato cha kawaida na wanaimudu. Kikubwa uwe na uwezo wa kupasuka itakapokuhitaji kupasuka na inachukua muda sana mpaka ikupasue.

Na kumbuka hii gari walengwa wake ni kipato cha kati ambao kaka zake X1 kina X3 na X5 imeonekana ni kichomi kwao. Kikubwa ipe service on time na kwenye engine hakikisha mfumo wa upozaji hauna shida, pipe zake zikikamaa badilisha.

Tofauti na hapo gari itakupa maisha marefu tu Na wala haitakusumbua though ina umeme mwingi na tatizo dogo utawashiwa taa utafikiri kuna mtu anataka kufa. so ukiona imewasha taa flani kwa dashboard i sort mapema na iguswe na wataalamu, Usifuge tatizo ukifuga tatizo kama lilikua mjusi litageuka Kenge itakua balaa.

Hii Gari tukikuletea toka Japan mpaka inafika sebuleni kwako gharama ni 18-23++, Bei inaweza panda au shuka kutokana na mwaka + condition husika ya gari. Kama unahitaji kuagiza gari karibu, tuko na network ya trusted dealers kwa Japan, UK, Singapore, Thailand etc.

Dealers wanaotupa gari zenye ubora wa juu kwa bei safi. Tutafanya mchakato wako wa kupata gari kuwa rahisi salama na unaojali muda wako.

Simply call 0714547598 njoo WhatsApp au ofisini Posta Mpya Phoenix House mkabala na Mkapa tower tutaku assist + kukushauri..
.

Kama uko mkoani na unahitaji kuagiza gari karibu, utatupa hitaji lako tutakupa Ushauri pia then tutakutumia options za gari ukishachagua utapewa invoice. Utafanya malipo at cost [no extra cost] huko huko ulipo mpaka gari itafika na utakuja kuichukua au kuletewa ulipo.

Natumaini umejifunza kitu kama jibu ni ndio basi usisahau kushare kwa ajili ya wengine na Kama hujatu follow katika Kurasa zetu za jamii tu follow sasa ili next time usipitwe na madini.

Pia tuna Free coaching group/channel kwa ajili yako, Hapo utakutana na madini kwa undani zaidi kuhusu magari kama uko interested whatsapp 0714547598 Jina lako na unakopatikana tutakuunga.

Asante
Samatime
0714547598
Inaelekea una uzoefu na haya magari, je kwa Tz ni akina nani wako vizuri katika kuyafanyia service au matengenezo ikibidi?
 
Back
Top Bottom