BMW X3: UKiweka ufunguo inachelewa kuwaka

conductor

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2013
Posts
811
Reaction score
681
Wakuu, inatokea nikiwasha gari inachelewa kuwaka. Ama nijaribu mara kadhaa ndo inawaka. Msada tafadhali. Naweza kuwa naendesha ikawasha taa kwenye dashboard ya 4x4 eml, handbrake halafu baada ya muda inaishiwa nguvu, haizimi, ila ukizima na kuwasha ina gain power na kuendelea. Pia inatokea ukitaka kukimbizia zaidi ya speed 40. Tatizo nini?

Msaada.
 
Itakuwa inaumwa sana unaiforce tu kutembea...
 
Hilo ndilo tatizo la german over engineering.

Wajerumani wanapenda sheria, kuzitunga na kuzifuata. So BMW anapotengeneza gari anawapa wamiliki sheria za namna ya kulitunza gari hilo. Na wajerumani wanaponunua BMW wanazifuata sheria za matunzo ya gari kisawa sawa.

Tatizo zinapoingia bongo ambapo watu wanapenda shortcuts na kuzunguka sheria husika, hayo magari yanachoka haraka na vibaya sana.
 
Wacheki wataalam wa hayo madude. Unaweza kuta kuna sensor imeloga kwani hizo ndinga zina sensor za kumwaga. Na possible kuna gear haziingii.
Note : usipeleke Kwa fundi yoyote kwani hizo ndiga zinawataalam wake na mpaka wafanye diagnoses ndiyo waelewe ugonjwa.
 
Pole..Kuna specialist wa BMW na Benzi! Kama bado ujapata ufumbuzi njoo DM nikupe no ya muhusika atakusaidia
 
Uko sawa mkuu. Mimi niliambiwa BMW lako weka petroli premium, usiweke regular.

Basi kila nikifika kituo cha mafuta ni " fill it up, premium". Siweki regular.

Kitaa kikiwaka kidogo tu, siku hiyo hiyo nakipatia ufumbuzi.

Hata kama ni kile cha kuonesha upepo umepungua katika tairi tu.

Haya magari yanataka high maintenance, si ya kudharau alerts.

Sasa mtoa mada hata alivyoandika kuelewewa tatizo limeanzia wapi ni kazi, maanq inaonekqnq kuna kitu zaidi ya kimoja kinagomba.

Labda tuulize, limetembea km ngapi?

Maana haya magari mwngine yakifika km za juu sana, kama hayajapata high maintenance, kuwa nalo ni mzigo tu.
 
Kuna Fundi anaitwa magoti,,Facebook anajiita magoti Fundi magari .Mtafute akusaidie japo hiyo Bima itakupuna sana hela.
 
Kuna Fundi anaitwa magoti,,Facebook anajiita magoti Fundi magari .Mtafute akusaidie japo hiyo Bima itakupuna sana hela.

Nampata yule yeye ana chonga na kuprogram funguo, alarm na diagnosis tu. Sio fundi yule.
 
Ok,pia anaweza recommend Fundi mzuri wa Gari yako kama hataweza kufanya kazi yako. Nishatengeneza sana Gari kwake kabla hajaingia kwenye mishe za kuchonga funguo.
Nampata yule yeye ana chonga na kuprogram funguo, alarm na diagnosis tu. Sio fundi yule.
 
Probablly hapo ni Fuel Pump kwenye kukosa nguvu inapopata moto haipamp mafuta yakutosha ndomana ukizima ikapoa inagain power,
Kwenye kipengele cha kuwasha taa ya handbreak chunguza kama ujazo wa break fluid kama ipo kwenye maximum level,endapo yamepungua ongeza tatzo litaisha na kama yapo level sahihi peleka garage yakueleweka ikapimwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…