BMW x5 na Volkswagen Tourage v6

kama una mishe za town ni nzuri hizo gari..mishe za kukutana na wana kusign mikataba etc etc..ila kama unategemea ikupeleke bukoba kagera mwanza mtwara katika mazingira ya miundombinu isiotabirika ie. matope, mashimo milima ..hell no usichukue kaka, hio hela bora uchukue harrier ya engine ya cc3000..hizo german car boi zitakufilisi..hata kikorokoro kidgo utasema hapa laki tu ***** utashangaa unatumia 1.5m..
 
Kwa uzoefu wangu..chukua E53..tafuta facelifted ya around 2005..
Engine tafuta petrol M54 au diesel M57 kwa misele ya kila siku..
Kama unataka performance zaidi sogea kwa petrol M62..
Hiyo gari ni nzito..kwahiyo petrol itakuwa inabugia kweli kweli..ila handling,comfortability imetulia..
 
Kweli kila MTU anakuwa anapenda kitu Fulani maana Mimi nikipishana na Volkswagen tourage huwa napunguza mwendo ili niichek vizuri hiyo chuma ni 8 speed transmission alafu ni DSG(direct shift transmission).
Kuanzia maporini Hadi mjini hii mashine iko vizuri sana,hii gari ndiyo gari ya ndoto zangu
 
Pitia hapa pia, unaweza kupata mawili matatu.
Ili ukianza kukuna kichwa kila siku usiseme hukua na taarifa.


Hapo unaweza kuangalia gari yoyote. Uzuri hizi changamoto wanazitoa wenyewe huko, hakuna story za... "ulipeleka gari chini ya mwembe au wabongo wanaskiliza story za vijiweni"

Kinachowasaidia wenzetu sana kule ni warrant, ngoma ikibuma unapeleka wana fix. Japo baadhi hata warrant hazijasaidia.

All in all hizi gari ni very conformable. Japo sidhani kama likianza kuzingua utakumbuka hiyo confortability
 
Ikianza kuzingua ni muda wa kutubu tu!😂😂😂
 
X5 m24 kutokea wapi hiyo;
X3 ya miaka ya nyuma ndio inaanzia bei hizo.
Mfano hii, kodi according to TRA ni 9.8 M so tufanye 10 M kabisa inakuja 24.4 M.. Hapo bado huja negotiate.

Tatizo wengi mnadhani hizi gari ni ghali.. Zina depreciation kubwa sana. Gharama zipo kwenye maintainance. Hii imetembea km 78K.
 
Vipi kuhusu Discovery 4..unaizungumziaje?
 
Hizi gari ikifika 100k ndio utajua hujui
 
Hizi gari gharama ya maintenance inakuja kwa sababu mtu ananunua ya zamani sana ishatembea sana.

Mimi nimeendesha X3, ilivyokaribia kufika 100,000 miles nikaitosa na kuchukua X5. Nayo ikikaribbia 100,000 miles nitaitosa sijaamua kuendelea na BMW au kuchukua Porsche Macan.

Ukishakaribia 100,000 miles, kutegemea na service unavyofanya au usivyofanya vizuri, unaweza kuona gari inaanza kukuletea mauzauza, especially kwenye barabara za kibongo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…