BOAT: 11% Riba ya mikopo karibu ya bure

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,677
BENKI ya "Bank Of Africa Tanzania (BOAT) imetangaza neema kwa watumishi wa umma baada ya kushusha riba ya mikopo kwa kada hiyo kutoka asilimia 14 hadi 11.

Aidha, benki hiyo imepunguza masharti ya ukopaji huku muda wa urejeshaji ukiwa ni mpaka miaka mitano.
"Tumeshusha riba ili kuongeza hamu na urahisi wa upatikanaji wa mikopo kwa wafanyakazi wa serikali ili wengi wanufaike na mikopo" alisema Muganyizi Busheko Mkuu wa Kitengo cha Masoko, Utafiti Maendeleo wa BOAT.

Chanzo: NIPASHE Jumatatu Mei 21, 2018
 

Attachments

  • IMG_20180521_045237 (1).jpg
    60.4 KB · Views: 98
  • IMG_20180521_083306.jpg
    178.7 KB · Views: 129
  • IMG_20180521_083158.jpg
    199.5 KB · Views: 114
sio jambo la kufurahia mkuu,neon MKOPO kaa nalo mbali maana unakuwa unatumia fedha isiyo ya kwako,hawa BOT wameitoa hii kisiasa ila kuna kitu kinaitwa T&C kimejificha between the lines.
 
Kuhusu sekta binafsi: Busheko alisema, benki hiyo inafanya utafiti ili kuweza kuwafikia watumishi wa sekta binafsi na kuongeza wigo wa wateja zaidi
 
Tunawatakia kila kheri watumishi wa umma' mikopo hiyo karibu na bure !
 
hawa wanakutega uingie kwenye mtego wao alafu waje wafanye amendment
 
Swali kwa nini watumishi wa Umma?
 
Sawa tumekuelewa ila BOAT ndio wap huko?
*
*
*****Nakutakia RAMADAN KAREEM*****
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…