Naomba unipe andiko linalo onyesha utabiri wa haile selase
nimewahi kuangalia mkanda wa Bob unaoitwa THE TIME WILL TELL. Kunasehemu bob anasema kwamba haile ni BWANA WA MABWANA NA MFALME WA WAFALME. Jina hilo linamstahili Yesu tu ambae ni mwana wa Mungu Yesu ni Mungu halisi alie fanyika mtu halisi soma Yohana 1:1-3. soma isaya 9 yote utaona. pia ukisoma yohana nane utaona yesu anawaambia wayahudi kwamba "Kabla ibrahimu hajazaliwa mimi niko" hapo Yesu alikua anadhibitisha uungu wake. Yesu tu ndie simba wa yuda. yeye ndie mkombozi wa wanadamu wote na wala sio waafrika peke yao. hata Haile aliwahikukataa kwamba yeye sie Bwana wa mabwana wala mfalme wa wafalme. Yesu ni Mungu anaepaswa kuabudiwa
Bible haikusema kwa kumtaja jina ila ilisema kuwa atatokea mtu ambaye atawatetea wana wa Mungu walioteswa kwa miaka na miaka na hata YHWH alisema atatumia uzao wa Daudi kuwatetea watu wake, Kwanza nipe maana ya Simba wa Yudah, maana yake ni kuwa Mzaliwa wa ukoo wa Yudah (Kwa upande wa baba na mama na sio Mungu na mwanadamu), ambaye atapigania haki za watu wa Mungu zilizopotea na kuteswa kwa utumwa kwa miaka na miaka. Yahshua anastahili sifa ya Mwana kondoo wa Mungu, tittle ya Simba wa Yudah alipewa kwa kuwa kipindi Yahshua alikwepo, wana wa israeli walikuwa chini ya utumwa wa warumi na ndio maana walitegemea Yahshua angewatetea na kuwatoa katika utumwa.
Isaiah 9:6 For unto us a child is born, unto us a son is given: and the government shall be upon his shoulder: and his name shall be called Wonderful, Counsellor, The mighty God, The everlasting Father, The Prince of Peace.
Hakuna ambacho hakukitimiza, Yahshua (ambaye unamwita Yesu) alipokuja na kufa kwa ajili ya dhambi zetu, hakusema kuwa yeye ndie wa mwisho kutimiza agano la kuwatetea wana wa Mungu na ndio maana mpaka anapaa bado waisraeli walikuwa wanateswa na warumi, Isaiah alitabiri mengi na mengine kiukweli kama unasoma biblia utagundua kuwa Yahshua hakuyatimiza mfano Kuzaliwa katika mji mkuu kama messiah, na pia wayahudi waliahidiwa kuwa messiah hatafanya miujiza, ila kurudisha makabila 12 yaliyopotea na kutunza sanduku la agano kwenye hekalu la tatu. Wana wa israeli mpaka leo wanamngojea masihi kwa kuamini kuwa Yahshua hakutimiza vyote, hata Yahshua alisema wapo watakaokuja kwa jina lake, wengine wakweli wengine waongo, is up to you kutopuuzia mambo ambayo unaona yanaendana na yale ya kale yaliyotabiriwa.
Najua wewe unasoma Biblia tu (may be KJV) katika kusoma Imani na kujifunza, lakini endapo ungekuwa unatumia Hebrew Bible na Kebra Negast (Kitabu kilichoandikwa na Malkia Sheba na Suleiman kinachopatikana Ethiopia, kimeelezea sanduku la agano lilipofika Ethiopia kutoka kwa Suleiman kabla ya kuvamiwa kwa Jerusalem baada ya utawala wa Suleiman na ungekuwa unatumia Biblia ya Ethiopia ambayo ni ya kale kuliko yako na ina vitabu vya zamani. Najua unajua kuwa YHWH alishasema kwa wana wa Israeli kuwa Ata stand katika ukoo wa Daudi, ukoo huo upo na umerithishwa mpaka Ethiopia kutoka kwa Suleiman, na tambua Ethiopia ndio nchi ya kwanza kwa kiongozi wake kuwa mkristu, hata kabla ukristu hujafika Roma ulishakuwa Ethiopia na ulikuwa umeenea zaidi.
Kwa miaka zaidi ya 400 mwafrika alikuwa ananyanyasika na kuteswa kwa kila kitengo.
NINGESHANGAA SANA KAMA MWAFRIKA ANGEKOSA MTU WA KUMTETEA NA KUMPIGANIA WAKATI KILA MKOMBOZI WA WAISRAELI MFANO NAUDI, MUSA, SULEIMAN NA WENGINE AWE ANAPIGANIA HAKI ZA WAISRAELI TU JE MWAFRIKA ANGETEWA NA NANI? TUNGESEMA MUNGU YUPO WAPI WAKATI WATU WAKE WANAONEWA?

Ndipo alipozaliwa Selassie na tambua kuwa maneno King of Kings, Lion of Judah ni yalikuwa yanatumika Ethiopia hata kabla ya kuja kwa Yahsua na walikuwa nawapema majina haya Emperors tu, kwa Selassie alijidhihirisha alipotetea tittle hizo kwa kupigania haki za watu, hata jina lake Haile Selassie lina maana ya Power of the trinity, ametoka katika Monarch iliyoanzishwa na Menyelik I mtoto wa Sheba na Suleiman. Sio lazima viongozi wa dini wakufundishe tu, hata wewe unaweza kujifunza kwa kuwa tayari kuujua ukweli. Sio lazima pia ukariri Bible tu kwa kuwa bible imeandikwa mara ya mwisho ni katika kitabu sha ufunua karne ya 1 baada ya Yahsua, kwahiyo yanayoendela hata kama YHWH ndie anayafanya huwezi kujua kwenye bible maana hutaki kutumia macho yako kuangalia. Yahshua alitabiri mengi sana, na mengine yanaweza yakawa yanatokea ila sie tunaona ni uongo tu.
For more links nitakuwa nikiziandaa.
I DONT WORSHIP H.I.M HAILE SELASSIE ILA NAAMINI NI MOJA KATI YA WATU MUNGU ALIOWACHAGUA KUWATETEA WATU WAKE KAMA UNAVYOMWAMINI DAUDI AU MUSA, NAHESHIMU JINSI ALIVYOISHI NA KUPIGANIA HAKI ZA WATU WOTE NA KWAKUWA MUNGU ALISEMA ATABAKI MILELE NA MILELE KATIKA UKOO WA DAUDI. NA PIA HATA SELASSIE ALIFUNDISHA KUWA NJIA YA WOKOVU NI YAHSHUA PEKE YAKE, SO KAMA NAAMINI MANENO YA SELASSIE LAZIMA NA YAHSHUA NIMFUATE MAANA MAISHA YA SELASSIE YALIKUWA NI MFANO WA KUIGWA KWA MKRISTU BORA.
Haile selassie kissing cross.