Bob Mtekama: FBI wa Malawi aliyekamata raia wetu huko Malawi

Bob Mtekama: FBI wa Malawi aliyekamata raia wetu huko Malawi

halafu mnataka jf ifungwe sjui mnataka kuturudisha katika maisha ya karne gani hyo,,Haya mambo mngeyapost wapi sasa
 
na mashaka na mleta mada kama hajatumwa na wamalawi kusifia askari wao na kutoa ramani ya uongo ya gereza ili kutuingiza king sisi maadui zao

ila kama ni kweli yaliyo semwa basi huyo askari ni threat kwetu hakuna namna ni kumuondoa tu , hapo KGB,M16 ,CIA zamani wangesha mrestisha in peace
sijatumwa na Malawi mkuu, mimi ni Mtanzania halisi haswaa tena nimelelewa kiujamaa sana ndiyo maana nikaona ni vyema kujuzana taarifa kuhusu adui yetu ambaye ni miaka kadhaa sasa anatusumbua.
 
Mlta mada hamna intelligensia yoyote aliyoileta , nimeona kama mwalimu yuko darasa la tano anatoa somo la jiografia, kasahau kuwaelezea wanafunzi wake ni mazao gani yanayostawi hapo mzuzu, kuhusu malawi laleni usinginzi wale hawatupi shida kwa lolote, wanajifurahisha tu huu mziki uitwao TANZANIA wanaujua fika, wale tena haina haja ya kuwafalisha magwanda na mabuti mazito vijana wetu wa JWTZ, tunaingia huku tumevaa all stars, new balance na nike air kama tunaenda fiesta huku le mbebezz akiwa mstari wa mbele na computa yake mpakato aina ya apple aliyopewa zawadi, tunamaliza kazi na tunarudi na wakata majani kibao kama fidia.
 
Una kipaji cha ukusanyajji taarifa ikiwa tu kama wewe sio wa kutoka kitengo

Hongers mkuu
Huyu jamaa katutafunia hadi sie vibogoyo!! maneena kama ni kweli vijana wetu wamenyakwa, fina lillah tukawakomboe tu, ujinga ujinga hatutaki na malawi wasizoeee...!
 
Huku mteka teka kule mtekama!!
embombo ngafu!!
 
Ila kitendo cha kuweka izo data apa tayari umekua disqualify...mana watasoma na wataongeza ulinzi.
If these details are true, then they are very minor and less important!! Agents never give everything!!
 
Mlta mada hamna intelligensia yoyote aliyoileta , nimeona kama mwalimu yuko darasa la tano anatoa somo la jiografia, kasahau kuwaelezea wanafunzi wake ni mazao gani yanayostawi hapo mzuzu, kuhusu malawi laleni usinginzi wale hawatupi shida kwa lolote, wanajifurahisha tu huu mziki uitwao TANZANIA wanaujua fika, wale tena haina haja ya kuwafalisha magwanda na mabuti mazito vijana wetu wa JWTZ, tunaingia huku tumevaa all stars, new balance na nike air kama tunaenda fiesta huku le mbebezz akiwa mstari wa mbele na computa yake mpakato aina ya apple aliyopewa zawadi, tunamaliza kazi na tunarudi na wakata majani kibao kama fidia.
Nadhani huna unalofahamu kuhusiana na kazi za jasusi. Jasusi huwa hadharau taarifa yeyote ile, iwe kubwa au ndogo ya kweli au ya uongo. Aipatapo huifanyia kazi ili aone kama INA madhara kwa ustawi wa nchi
 
Hao jamaa zetu wa caritas roman walienda kujifunza madhara ya uchimbaji urani najua wataachiwa bila masharti japo watahojiwa kama dedturi. Kuhusu maelezo ni ya kawaida na yapo mtandaoni Google utapata.
 
Utaifa Kwanza, TANZANIA moja yenye Ushindi.

Wadau hiyo ndiyo salamu yangu hapo juu.

Tujuzane machache kuhusu jirani yetu Malawi hasa katika ule mji wa MZUZU ambapo inasemekana raia wetu wamekamatwa wiki iliyopita na kuzuiliwa nchini humo, haijalishi ni kweli au la! Lakini tujuzane haya machache kuhusu huyu jamaa anaitwa Bob Mtekama na ule Mji wa Mzuzu.

BOB MTEKAMA.

Huyu jamaa ni askari polisi wa malawi ambaye kwa jina lingine anaitwa Bob Hamisi Stambuli Mtekama, umri wake haujathibitika ana miaka mingapi lakini huenda akawa ana miaka 30 hadi 45.

Ni askari wa usalama nchini MALAWI lakini pia hivi karibuni ametajwa na vyombo vya habari vya Malawi kama askari aliyehusika na ukamataji wa Wapelelezi wa Tanzania huko karibu na mgodi wa uranium ulioko Kayerekera wilayani Karonga kaskazini mwa Malawi katika jiji la MZUZU.

Hatahivyo askari huyu haegemei upande wowote wa kisiasa,

ndiyo maana alipokuwa mkuu wa polisi kitengo cha upelelezi wa makosa ya jinai (CID) mkoa wa kusini nchini Malawi alikataa kwenda kukamata wakosaji wa kisiasa dhidi ya wanasiasa wa chama tawala.(ukitaka picha yake nenda ZNZ UNIVERSITY)

ELIMU NA UTALAAMU WAKE:

Vyanzo vichache vinaonyesha kuwa askari huyu amesomea degree au stashahada ya sheria ya makosa ya Jinai katika chuo kikuu cha Zanzibar,

hatahivyo pia ni POLISI PEKEE nchini Malawi mwenye elimu ya sayansi ya itumikayo kwenye makosa ya jinai na madai (forensic science).

Elimu hiyo ya forensic science ameisomea katika chuo kikuu cha Malawi kwenye chuo kidogo cha udaktari, chini ya mwalimu wake mkuu Proffessor George Liomba na Dr. Charles Dzamalala.

Kwa upande wa taaluma, yeye ni mtaalamu wa alama za vidole (fingerprint) na pia ni yeye pekee aliye mtaalamu wa mwandiko(handwriting expert) katika jeshi la polisi nchini Malawi.

MAHUSIANO YAKE NA FBI.

Taarifa nyeti zinaonyesha Bob Mtekama amebobea pia kwenye Upelelezi ambao amefundishwa na FBI nchini Marekani.

Hatahivyo lazima tujiulize je alifundishwa na FBI kuwa Double agent wao(kwa ajili ya Malawi na kwa ajili ya Marekani)? Au alifundishwa na FBI kwa ajili ya Malawi tu?

Lazima tuwe makini na huyu jamaa!!

kwani pia alihamishwa kikazi kutoka mkoa wa kusini mwa Malawi akapelekwa Central Malawi na sasa yuko anafanya kazi kama Mkurugenzi wa CID (Criminal Investigation Department) nchini Malawi akiwa anafanya kazi huko mkoa wa kaskazini ya Malawi!!
Ambapo ndipo penye mgogoro wa mpaka kati yetu na Malawi.

Huenda aliletwa hapo kaskazini kwa kazi maalumu ya usalama wa mpakani.

HISTORIA YAKE YA KAZI:

Huyu jamaa anaitwa afisa wa polisi Mtalaamu kwa umaridadi wake wa kupambana na wahalifu wa makosa ya Jinai nchini Malawi,

ndiyo maana wakati alipokuwa anateuliwa kuwa mkurugenzi wa CID maneno haya hapa chini yalisemwa;

“The IG has made a landmark appointment on Mtekama as he will bring sanity to the CID department. He is a well disciplined and extensively trained and dedicated police officer with a methodological know how on how to curb crime and criminals having been a CID office for a long time.”

Hatahivyo alifahamika sana kama mkamataji hodari wa wahalifu wakati alipokuwa mkuu wa kitengo cha CID katika mkoa wa kusini mwa Malawi.

Inasemekana kuwa alihusika kuwakamata Majambazi wa kutumia silaha kwenye maeneo maarufu ya THYOLO and CHICHIRI waliotuhumiwa kuvamia Benki ya Taifa ya Malawi mwezi wa sita 2012 huko Malawi

pia alihusika katika ukamataji wa watuhumiwa wa wizi wa kijambazi wa Mishahara ya Wizara ya Elimu ya Malawi.

Bob Mtekama pia alihusika kwenye operation maalumu iliyowahusisha maafisa wengine wa kipolisi kama vile detective George Mnjale, detective Mkwate ambao kwa pamoja waliwakamata kwa ustadi wauaji waliokubuhu wa CHIRADZULU (Chiradzulu serial killers’ criminals.)

GEREZA LA MZUZU. (MZUZU PRISON)

Mzuzu ni mji ambao ni makao makuu ya mkoa wa kaskazini mwa Malawi.

Vyombo vya habari vya Malawi vinasema mji huu ni maarufu kwa kilimo na mifugo, hatahivyo taarifa ya hivi karibuni iliyoripotiwa na vyombo vya Malawi kuwa kuna wapelelezi wa nchi yetu wamekamatwa huko Malawi na kupelekwa rumande kwenye Gereza la Mzuzu ambalo lipo kwenye mji wa MZUZU.

HISTORIA YA GEREZA LA MZUZU.

Maelezo yanaonyesha kuwa gereza hili lilijengwa na mwingereza mnamo miaka ya 1950 hadi 1960 kwa ajili ya wafungwa 200 lakini kwa sasa inaonekana kuwa lina wafungwa zaidi ya 500,

hali inayopelekea mrundikano mkubwa wa wafungwa na mahabusu.

Hatahivyo miaka ya hivi karibuni zimejengwa selo mbili katika gereza hilo ila zilishindikana kutumika kwasababu ya kukosa uzio (fence).

Kutokana na sababu hiyo Prophet Bushiri na Mzuzu Lions Club walijitolea kujenga huo uzio kwa kutoa vifaa na pesa taslimu.

Kwahiyo Gereza hili bado linafurika kwa wafungwa na mahabusu, ambapo wengine hulala wakiwa wamekaa sebuleni au kwenye vyumba vya selo.

RAMANI YA UJENZI WA GEREZA LA MZUZU. (ARCHITECH MAP OF MZUZU PRISON)

Nimetafuta sana ramani iliyotumika kujenga gereza hili lililojengwa na taifa la Uingereza ila sijaipata lakini inaweza kupatikana kwa kupitia mfungwa/mahabusu mojawapo aliyewahi kufungwa hapo Mzuzu(sidhani kama huko Songea au Katavi atakosa mtu aliyewahi kufungwa au kuwekwa mahabusu katika gereza hili).

JIOGRAFIA YA GEREZA LA MZUZU.

Gereza hili lipo katika mji wa Mzuzu, mji huu uko kaskazini mwa Malawi ambapo ndipo kuna gereza hilo la Mzuzu.

Njia 2 za kufika Mji wa Mzuzu.

Mahali hapo panafikika kwa bus, treni au ndege ama helikopta. Usafiri wa gari ni km 46.6 unasafiri kwa muda wa dakika 56 hadi kufika hapo kama umepita njia ya Nkhata Bay mpaka mji wa Mzuzu.

Usafiri wa ndege in km 35 kwa muda wa dakika mbili tu kwahiyo kwenda na kurudi ni dakika 4 tu mpaka Nkhata Bay ambapo hapo Nkhata Bay kuna usafiri wa Maji hadi Mbamba Bay Tanzania.

Mzuzu GPS coordinates.
Latitude/ Longitude:
-11.45807, 34.015131 *
-11° 27' 29.0514", 34° 0' 54.471" **

Nkhata Bay GPS coordinates
Latitude/ Longitude:
-11.6085556, 34.29494090000003 *
-11° 36' 30.8016", 34° 17' 41.7876" **

(WGS84):
* Decimal
** Degrees, minutes, seconds

Njia ya pili ni ya kupita majini kutoka Manda ya Tanzania mpaka Chilumba pwani ya Malawi ambayo ipo karibu na Nyika National PARK

AMBAPO kutoka Nyika National Park hadi mzuzu kwa gari kuna umbali wa km156km kwa mwendo wa masaa 2 na dakika 46,

njia hii ni ya mzunguko sana hatahivyo kule karibu na mbuga sidhani kama kuna usalama wa kupita vyema hasa kutokana na wanyama wakali au askari pori.

ZIPO njia nyingine za kufika huko lakini sitazitaja hata kidogo.

ULINZI WA GEREZA LA MZUZU.

Gereza hili lina perimeter fence na ulinzi wa kawaida tu wa polisi wa Malawi japokuwa kuna military base kwenye mji huo wa Mzuzu.

Hatahivyo huu mji wa Mzuzu unakabiliwa na tatizo la kutokuwa na taa za kutosha za kumlika usiku.

Nilipokuwa mdogo nilifundishwa na wazazi wangu kuipenda nchi yangu haswaaaaaaa!

Nimefanya hivi kwa mapenzi ya nchi yangu na sio vinginevyo.

Mwisho.

Inayofuata hapa chini ni link yenye Picha ya mji wa Mzuzu.

C:\Users\TUMAC\AppData\Local\Temp\msohtmlclip1\01\clip_image002.jpg

www.panorama.mzuzu
C:\Users\TUMAC\AppData\Local\Temp\msohtmlclip1\01\clip_image004.gif

Mkuu umetupa hints nzuri sana. "Operation Mzuzu" itabidi ifanyiwe mchakato km ile ya Israel 1976 entebbe! Ngoja nimtafute maj gen Dan Shomron na Yakutiel Adam tupange strategies!
 
Ndo jukwaa hili linanifanya naendelea kubakia jamii forum. Japo wakongwe wamekimbia miye nimo tu...!! Safi sana mleta mada..taarifa zimefika.
Baba yako alikufundisha vyema..tuipende Nchi yetu Tanzania.
 
Baaandaaa wa Malawii, katuvaliaa ngozi ya simbaa, hatujalii, hatujalii.
Wimbo wa mchakamchaka full kinanda, unanikumbusha enzi hizo.
Malawi alikuwa adui mkubwa wa Tz enzi za utawala wa maisha wa rip Hastings Kamuzu Banda.
Kama ilishindikana "kuzipiga" enzi za Nyerere,sasa hivi tutamalizana nao vizuri. Matumaini yangu ni kwamba diplomasia itazaa matumda.
 
Hao mgambo ndo wetu hakuna wengine, kama huwataki nenda kaolewe na CIA.
Kwann wewe ndo wamekupatia mimba . .??..na ulibikiriwa vibaya na hao jamaa maana unakiherehere....
 
Back
Top Bottom