Boban atinga airport na kandambili

Boban atinga airport na kandambili

bangi mbaya ndugu yangu.

hilo si suala la bangi,na mtetea kwa hilo
kwanza kikawaida unapokuwa ndani ya ndege unashauriwa kuvaa viatu vyepesi ambavyo vitakusaidia kuwanyambulika wakati ukiwa ndani ya ndege na hii husaidia hata kujiaandaa kutoka ndani ya ndege kama kuna chochote kibaya kimetokea

lakini nimekuja gundua kuwa ktk maswala ya kusafiri na ndege ni sisi wabongo ndio huwa tunasababisha maisha kuwa magumu sana,kwani wasafiri wengi wanaotumia ndege utawaona wapo simple sana hawana mambo mengi zaidi ya mabegi baadhi ya rambo na hata mavazi yao ni ya kawaida sana

tatizo wabongo ili uonekane umepanda ndege basi utataka uwe na suti na kiatu kutoka italy

tubadilike
 
Boban wa pili kushoto.

Kiungo mshambuliaji wa timu ya Simba, Haruna Moshi Boban jana alikuwa kivutio kwa mashabiki, wasindikizaji na hata baadhi ya wasafiri waliomuona wakati wakiondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, kuelekea Sudan. Uvaaji wa Boban, ndio uliowavutia watu kumtizama, kutokana na kuvaa kama mtu asiyesafiri.
Boban alikuwa amevaa fulana, suruali ya kimichezo trakisuti na kandambili, hivyo kusababisha watu kuvutika kumuangalia, huku baadhi yao wakibaki kujiuliza kuhusu vituko vya nyota huyo ambaye mashabiki humuita Balotteli wa Bongo.
🤣🤣
 
Mbona hata mie hupendelea kuvaa sandals zozote zitazokuepo around ili kuepa longolongo za kuvua na kuvaa viatu. Ni mapenzi tu ya mtu.
BTW, there is only one Boban, Zvonimir Boban, left-footed na kiungo mpishi mahiri kabisa wa zamani wa Dinamo Zagreb, Milan 1899 na timu ya taifa Croatia, hao wengine wa kwenu ni wakuchonga tu si lolote si chochote...they don't worth the comparison.
Morogoro kuna Fathet pekupeku kokote aendako hutembea peku, hutumia pia baiskeli, (Anita)
 
Back
Top Bottom