Bobby Firmino Fundi asiyeimbwa

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2017
Posts
23,620
Reaction score
52,790
Wengi wamekuwa wakiwaimba na kuwatukuza akina Mane na Salah pale Liverpool.

Roberto Firmino "Bobby" ana kipaji maridhawa sana, amejaaliwa control ya hali ya juu mno, touch za hatari, bila kusahau utulivu wa aina yake. Anaweza kucheza kama Winga, Kiungo namba 10 lakini hucheza pia kama namba 9 ya uwongo kwa kimombo huitwa "false 9" kama anavyotumika Liverpool kwasasa.

Bobby amekuwa ndiye muhimili mkuu wa Liverpool katika mashambulizi na hata wakati wa kujilinda. Liverpool wanaposhambulia, Bobby amekuwa akipiga pasi zenye macho kwa akina Salah na Mane, kwenye counter attack kwakuwa hana spidi, anaweza aka-hold mpira na kuja kusaidiwa na wenzake. Pia movement zake za akili zimekuwa zikiwasumbua sana mabeki wa timu pinzani. Staili yake ya uchezaji huwa ananikumbusha enzi za fundi wa Kiargentina Ariel Ortega au mchawi wa Kiitaliano kutokea pale jijini Rome, Fransisco Totti "El Capitano de la Roma".

Ila kwakuwa hafungi magoli mengi sana kama Mane na Salah, wapenda soka wengi wamekuwa wakimchukulia kawaida tu huku wakimnyima sifa zake. Binafsi sio mshabiki wa Liverpool ila nafurahishwa na jinsi Firmino anavyosakata kabumbu. Ni wakati sasa wa kumpa sifa zake...
 
unaijua false 9 wewe?

kaangalie Barcelona ya guardiola ile Mechi na Real Madrid
au ya Spain Euro 2012
 
Ukimtoa Mane safu ya ushambuliaji Liver lazima ife kibudu ile mutu ya Senegal ina balaa sana
 
Firimino yupo vizur huyo jamaa , binafs namkubali , mane ndo nguzo ya timu sababu ya speed na maamuz ya haraka kitu ambacho kinawapa temper mabeki Ila ana ka upapara fulani hv sio mtulivu.... Firimino anacheza mpira wa standard gauge
 
Na
Najaribu kukubaliana na hoja yako lakini kila nikifikiria movement za mane uwanjani na namna beki wanavyohaha kumdhibiti nafsi yangu inagoma kabisa.
Nafikiri mleta mada anamaanisha bobby nae anapaswa kuimbwa sio wakina mane tu, that means anajua kuwa mane ni another level ila bobby nae kwenye msafala yumo
 
Firimino yupo vizur huyo jamaa , binafs namkubali , mane ndo nguzo ya timu sababu ya speed na maamuz ya haraka kitu ambacho kinawapa temper mabeki Ila ana ka upapara fulani hv sio mtulivu.... Firimino anacheza mpira wa standard gauge
Sawa mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…