Greatest Of All Time
JF-Expert Member
- Jan 1, 2017
- 23,620
- 52,790
Wengi wamekuwa wakiwaimba na kuwatukuza akina Mane na Salah pale Liverpool.
Roberto Firmino "Bobby" ana kipaji maridhawa sana, amejaaliwa control ya hali ya juu mno, touch za hatari, bila kusahau utulivu wa aina yake. Anaweza kucheza kama Winga, Kiungo namba 10 lakini hucheza pia kama namba 9 ya uwongo kwa kimombo huitwa "false 9" kama anavyotumika Liverpool kwasasa.
Bobby amekuwa ndiye muhimili mkuu wa Liverpool katika mashambulizi na hata wakati wa kujilinda. Liverpool wanaposhambulia, Bobby amekuwa akipiga pasi zenye macho kwa akina Salah na Mane, kwenye counter attack kwakuwa hana spidi, anaweza aka-hold mpira na kuja kusaidiwa na wenzake. Pia movement zake za akili zimekuwa zikiwasumbua sana mabeki wa timu pinzani. Staili yake ya uchezaji huwa ananikumbusha enzi za fundi wa Kiargentina Ariel Ortega au mchawi wa Kiitaliano kutokea pale jijini Rome, Fransisco Totti "El Capitano de la Roma".
Ila kwakuwa hafungi magoli mengi sana kama Mane na Salah, wapenda soka wengi wamekuwa wakimchukulia kawaida tu huku wakimnyima sifa zake. Binafsi sio mshabiki wa Liverpool ila nafurahishwa na jinsi Firmino anavyosakata kabumbu. Ni wakati sasa wa kumpa sifa zake...