Bobi Wine amwambia Museveni “Msamaha wako haujakubaliwa”

Bobi Wine amwambia Museveni “Msamaha wako haujakubaliwa”

Elias Msuya

Platinum Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
267
Reaction score
1,014
Musician-Bobi-Wine.jpg


Wakati Rais wa Uganda, Yoweri Museveni akiomba msamaha Waganda kwa makossa yaliyofanywa wakati wa utawala wao wa miaka 40, Rais wa chama cha NUP, Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine amekataa msamaha huo, akisema bado wananchi wanaendelea kuteseka katika nchi yao.

Museveni na mkewe Janeth waliomba msamaha huo jana Mei 28 katika hafla ya kidini iliyoongozwa na binti yao, Mchungaji Patience Rwabwogo katika uwanja wa Kalololo jijini Kampala na kuhudhuriwa na waumini wa madhehebu tofauti.

Hata hivyo, Bobi Wine katika ujumbe wake mitandaoni amepinga msamaha huo.

"Wakati yeye anaomba msamaha, ndugu zetu wako kwenye vyumba vya chini wakiteswa. Dada zetu wanabakwa. Watu wetu bado wanafukuzwa kwenye ardhi yao, haturuhusiwi kuwa binadamu kwenye nchi yetu. Nikiwa nimesimama hapa, namwambia Museveni, msamaha haujakubaliwa," ameandika Bobi Wine.
Soma pia: Bobi Wine: Mtoto wa Museveni anatishia kunichinja, Muhoozi asema Baba yake ndiye anayemzuia kumchukulia hatua

Museveni aliyeingia madarakani kwa njia ya vita vya msituni mwaka 1986, amekuwa akilaumiwa kwa kung’ang’ania madarakani, huku akiweka watu wake wa karibu katika nafasi za juu akiwamo mwanaye, Kainerugaba Muhoozi ambaye ni Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Uganda (UPDF).
 
Back
Top Bottom