Bobi Wine apinga Matokeo ya Awali yanayotanzwa na Tume ya Uchaguzi

Bobi Wine apinga Matokeo ya Awali yanayotanzwa na Tume ya Uchaguzi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Mgombea wa upinzani nchini Uganda Bobi Wine amepinga matokeo ya uchaguzi ambayo yametangazwa hadi sasa na kujitaja binafsi kama rais mteuli, licha ya tume ya uchaguzi kusema kuwa sio kura zote zilizokwisha hesabiwa.

Bobi Wine anadai uchaguzi wa Alhamisi ulitawaliwa na wizi mbaya zaidi wa kura kuwahi kushuhudiwa katika historia ya Uganda, lakini hakutoa ushahidi wowote kuhusu madai yake. Ametangaza kuwa mapambano ndio kwanza yameanza.

Bobi Wine, ambaye jina lake halisi ni Robert Kyagulanyi, anasema kuwa atazungumza na waandishi wa habari tena mnamo saa chache zijazo juu ya kitakachofuatia.

Matokeo ya awali yanayotolewa na Tume ya uchaguzi yanaonesha Rais Yoweri Museveni anaongoza kwa zaidi ya 60%.

Wanajeshi wamezingira nyumba ya Bobi Wine.
 
Kwani hakusikia yaliyokuwa yakitokea kwa majirani zake wa kusini?

Ya mabegi meusi nayo hakusikia?

Ya kutofanya uchaguzi bila ya tume huru hakuyasikia?

Walidhani dikteta wao huko anatofauti gani na madikteta wengine?

Atashinda mtu huko pia kwa kishindo na kura kama 84%.

Mitano mingine.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Hivi kweli unaamini yule mtu kapigana vita miaka ile na chama chake sasa wanakula matunda halafu wafanye uchaguzi wa haki? ila kama kamwamsha mzee tu kuwa kuna mtu anakuja.

Kuna mganda rafiki leo nimeongea naye kuhusu hili akaniambia sio kwamba anampenda M7 lakini hataka stability ya amani ipotee kwa waganda mambo waliyopitia hawataki wanaogopa.

Nikamwambia hata huyu anaweza jibu lake kasema bora zimwi ulijualo nikaelewa hofu yao hawataki kwenda sehemu wasiyokuwa na uhakika nayo wanaona acha atawale tu ni kama sisi CCM.
 
Kwahiyo nae alitegemea kushinda?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Vituko vingine jamani,

Hana tofauti na Lisu na soon atakimbilia kule kule alikopeleka wanae
 
Yoweri Museven alikuja tanzania kupata "COURSE" ya njia za kuiba kura na jinsi ya kucheza na asilimia za ushindi.

Natabiri Magufuli atakua rais wa kwanza kumpa pongezi za ushindi wa kishindo swaiba wake.

Sio kwamba yeye alitupa kozi. Ameiba kura tokea 2001.
 
Kuna vitu ni ngumu kutokea.

Watu walikesha mistuni wakapata uhuru inakua utata sana kuachia madaraka. Somo lilikua kwa Mugabe Zimbabwe na DJ Morgan.

Leo kwa Museveni na mwanamuziki Bobi.

Mugabe aliamini yeye kukaa msituni kulimpa Morgam uwanja wa kua DJ. Museveni anaona vita alizosimamia ndiyo zimeitengeneza Ug aliyoikuta Bobi.

Ni ngumu sana. Lavda itokee aachie madaraka kama ilivyotokea Zimbabwe.
 
Kwahiyo nae alitegemea kushinda?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Vituko vingine jamani,

Hana tofauti na Lisu na soon atakimbilia kule kule alikopeleka wanae
wafuasi wa Magufuli mna interest na utawala wa dikteta babu Mu7.
 
Back
Top Bottom