Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Muhoozi ameandika hayo kwenye akaunti yake ya X (zamani Twitter) ambapo Bobi Wine amemjibu na kusema "Kitisho cha Mtoto wa Museveni (ambaye pia ni Mkuu wa Jeshi la Uganda) la kunikata kichwa sio kitu ninachokichukulia kwa wepesi hasa ukizingatia kwamba Watu wengi wameuawa na yeye na Baba yake na kwa kuzingatia pia majaribio kadhaa ya kuondoa uhai wangu, nakataa kutishwa na utawala wa uoga, Dunia inatazama"
Muhoozi katika hatua nyingine amesema lilikuwa ni wazo lake na Majenerali wenzake kumshawishi Rais Museveni kumtumia Bobi Wine kama pandikizi la kumuondolea nguvu Kiza Besigye na kumfanya asiwe Kiongozi wa upinzani mwenye nguvu Uganda huku akisema baada ya kumpa pesa nyingi Bobi Wine na akapata nguvu na umaarufu aliwageuka na kuanza kuwatukana yeye na Baba yake "Kabla sijakukata kichwa Bobi Wine rudisha pesa zetu tulizokukopesha"
Muhoozi pia amesema "Nikiwa ni CDF nawaagiza Wanajeshi wote na Mamlaka nyingine za Usalama kumkamata Bobi Wine (hata kwa kutumia nguvu na vurugu ikiwezekana) pale tu atapomtukana Rais Museveni, Mimi CDF na Wanafamilia wote wa Museveni kwenye tukio lolote hadharani"
Pia, Soma:
• Bobi Wine apigwa risasi ya mguu katika vuta n'kuvute na polisi
• General Muhoozi: Sitagombea Urais 2026, nitamuunga mkono Yoweri Museveni kwenye uchaguzi