Ndo tatizo letu waafrika wa kizazi hiki kufikiria "kuvuta cheki" kwa maslahi ya matumbo yetu, kama wazee wetu wangevuta cheki tungekuwa bado tuko kwenye mikono ya mabeberu, kina Mandela hawakushindwa kufanya vile ili washibe wao ila lengo lao lilikuwa kwa maslahi ya taifa/jamii, tofauti na kinachotokea hata hapa nchini, mtu hajali wananchi waliojipanga juani kwenda kumpigia kura ili awe mwakilishi wao kwa kumwamini kabisa, from nowhere mtu anakwambia nimeona niunge juhudi "za mtu mmoja" badala ya maelfu waliomchagua, kizazi hiki kimelaaniwa kwa kuendekeza njaa, naona na wewe unaunga mkono kwamba Bobi Wine apewe cheki na aunge mkono juhudi za Mseveni kuwakandamiza waganda, Afrika Mashariki tumeingia kwa haraka katika utumwa wa nafsi, "mental enslavement. Ngoja tutengeneze historia kwamba kuliwahi kuwa na kipindi cha kuunga mkono, tumuombe Bobi asiwe "Waitara, Mtatiro, Mtulia au Karanga" wa waganda, sijataja madiwani