Boda aliyegongwa na Mwendokasi kulipwa Milion 88 kama fidia

Boda aliyegongwa na Mwendokasi kulipwa Milion 88 kama fidia

Bawabu wa pili

Senior Member
Joined
Nov 14, 2025
Posts
147
Reaction score
433
Mahamana Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam imeamuru Kampuni ya UDA Rapid Transport Ltd kumlipa fidia ya Sh. milioni 88.8 Frank Zebaza, baada ya kugongwa na basi la mwendokasi, ambapo pia imebainika kuwa Dereva Hafidhi Ally alikuwa akiendesha basi hilo kwa mwendo hatarishi ambaye pia Mahakama imemuamuru kumlipa Frank fidia ya shilingi Milioni kumi.

Soma pia: Bodaboda kuvamia barabara za mwendokasi imekuwa kero, wanafanya ajali zisiishe

1766405957139.png

Hukumu hiyo ilitolewa Desemba 19, 2025 na Jaji Griffin Mwakapeje, kufuatia kesi ya madai namba 28992 ya mwaka 2024 iliyofunguliwa na Zebaza dhidi ya UDA Rapid Transport Ltd, dereva Hafidhi Ally, Shirika la Taifa la Bima (NIC) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), akidai fidia ya jumla ya Sh. milioni 600 kwa madhara aliyopata.

Katika madai yake, Zebaza aliomba alipwe Sh. milioni 350 kama fidia maalumu kwa gharama za matibabu na matumizi mengine yanayohusiana na ajali hiyo, Sh. milioni 150 kama fidia ya jumla kwa maumivu na mateso pamoja na Sh. milioni 100 kama fidia ya adhabu.

Akisoma hukumu hiyo, Jaji Mwakapeje alisema ushahidi uliowasilishwa mahakamani unaonesha wazi kuwa mlalamikaji alipata majeraha makubwa yaliyomlazimu kufanyiwa upasuaji mkubwa na hadi sasa anaendelea kukumbwa na athari za kudumu katika mfumo wa fahamu na hisia, hali iliyosababisha kupungua kwa uwezo wake wa kufanya kazi.
 
Jamaa alitaka hela nyingi mno aisee!
Milioni mia sita!!
 
kwani huyo jamaa aligongwa akiwa kwenye barabara ya mwendokasi au basi basi lilimfata kwenye lami ya kawaida.,,? na DARR wasipomlipa atafanya nini au atakamata mabasi na DART mabasi yao mengi mabovu na hata likiwa zima ataliuza wapi..maana hao wahuni wanaweza kumuachia akamate mabasi mawili apate fidia yake wakijua hana pa kuyapeleka au kuyatumia.! hata kama wakimlipa fedha taslimu lazima agawane na wazee wa urefu wa kamba humo Dart
 
Akikamata mabus mawili anayapaka rangi, yanaanza kupiga root mzee 😃
 
Maswali ya la 4B. Mahakama ikikaza hukumu hata jengo la ofisi linashikiliwa.
kwani huyo jamaa aligongwa akiwa kwenye barabara ya mwendokasi au basi basi lilimfata kwenye lami ya kawaida.,,? na DARR wasipomlipa atafanya nini au atakamata mabasi na DART mabasi yao mengi mabovu na hata likiwa zima ataliuza wapi..maana hao wahuni wanaweza kumuachia akamate mabasi mawili apate fidia yake wakijua hana pa kuyapeleka au kuyatumia.! hata kama wakimlipa fedha taslimu lazima agawane na wazee wa urefu wa kamba humo Dart
 
Kama namwona Lucha anavyowaza na kuwazua ni namna gani asuke tukio la kujigongesha kwenye UDART ili lau aambulie kulipwa fidia.
 
Mahamana Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam imeamuru Kampuni ya UDA Rapid Transport Ltd kumlipa fidia ya Sh. milioni 88.8 Frank Zebaza, baada ya kugongwa na basi la mwendokasi, ambapo pia imebainika kuwa Dereva Hafidhi Ally

Mwenda kwa miguu ashinda kesi dhidi ya UDART kwa ajali ya uendeshaji usio makini wa dereva wa mabasi ya mwendokasi, kumgonga ajivuka ktk alama za pundamulia.

Katika kuthibitisha kesi yake, mlalamikaji, Frank Wilson Robert (PW1),chini ya kiapo, alishuhudia kwamba mnamo tarehe 30 Septemba 2022 karibu saa kumi na moja jioni na dakija 20 (at 5:20 p.m)., alikuwa akivuka kivuko cha pundamilia huko Kariakoo (eneo la Fire kariakoo) pamoja
Barabara ya Morogoro jijini Dar es Salaam alipogongwa ghafla na gari inadaiwa kuwa mali ya mshtakiwa wa 1. yaani UDART Alidai kuwa alikuwa na haki ya njia
kama alama za trafiki zikiwaruhusu watembea kwa miguu kuvuka.
Kulingana naye, gari hilo lilimgonga lilimuangusha chini alipokuwa anavuka
mstari mweupe wa tatu wa kivuko cha pundamilia, na kumsababishia majeraha makubwa kichwani
hiyo ilimfanya kupoteza fahamu. Alikumbuka kupata fahamu akiwa
hospitalini, ambapo alipata ufahamu kutoka kwa jamaa kwamba polisi walikuwa wametoa
PF3 kwa matibabu yake. Hati hiyo ilikubaliwa kama Kitthibitisho namba P1.

Alieleza zaidi kuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili
Hospitali (MOI), ambapo uchunguzi wa CT scan ulibaini fuvu lililovunjika upande wa kulia
upande wa kichwa chake, na kuhitaji upasuaji wa ubongo. Alieleza kuwa alikuwa
kuagizwa kukaa katika mazingira tulivu wakati wa kupona na kuhamishwa...

KESI YA MSINGI:

Kesi ya mlalamikaji ni kwamba mnamo 30 Septemba 2022, wakati wa kutembea kando ya Barabara ya Morogoro, Ilala, Dar es Salaam, aligongwa na basi la mwendokasi, modeli / aina ya Golden Dragon, lenye usajili No. T132 DGW, inayomilikiwa na
Mshtakiwa wa 1 , amewekewa bima na mshtakiwa wa 3 na kuendeshwa kwa uzembe na
Mshtakiwa wa 2. Anahusisha ajali hiyo na uzembe na kupita kiasi
wa dereva wa mwendokasi, kushindwa kuzingatia sheria za trafiki, na ukosefu wa udhibiti sahihi gari. Ajali hiyo iliripotiwa kwa polisi, na akapewa fomu ya
PF3 kwa ajili ya matibabu.
Mlalamikaji anadai alipata majeraha mabaya kichwani na kusababisha hali mbaya
jeraha la kiwewe la ubongo na shida zingine kama vile kupoteza uwezo wa kusikia harufu n.k ..

HUKUMU :

KATIKA MAHAKAMA KUU YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
USAJILI NDOGO WA DAR ES SALAAM
JIJINI DAR ES SALAAM

KESI YA MWANANCHI

Nambari 28992 YA 2024

FRANK WILSON ZEBAZA...........Mlalamikaji

DHIDI YA

UDA RAPID TRANSPORT LIMITED COMPANY [UDART]........MTUHUMIWA WA 1

HAFIDHI ALLY.......MTUHUMIWA WA PILI

SHIRIKA LA TAIFA LA BIMA....MTUHUMIWA WA 3

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI...............MTUHUMIWA WA 4

HUKUMU

Tarehe ya agizo la mwisho: 08/12/2025

Tarehe ya Hukumu: 19/12/2025
MWAKAPEJE, Jaji.:

Mlalamikaji alifungua kesi ya sasa, akidai dhidi ya washtakiwa kwa yafuatayo:

1. Agizo la malipo ya Tshs. 350,000,000/- (shilingi za Tanzania
Milioni mia tatu na hamsini) kama fidia maalum kwa gharama
zinazotumika kwa matibabu na gharama zingine zinazohusiana.

2. Agizo la malipo Tshs. 150,000,000/- (shilingi za Tanzania Moja milioni mia na hamsini) kuwa uharibifu wa jumla kwa maumivu na mateso.

3. Amri ya malipo ya fidia ya kiasi cha Tshs.100,000,000/- (shilingi za Tanzania milioni mia moja)

4. Gharama za kufungua kesi hii

5. Riba yake katika viwango vya Mahakama katika kiwango kilichopo kutoka 30 Septemba 2023 hadi malipo kamili.

6. Msaada mwingine au zaidi kama vile Mahakama hii Tukufu itakavyoona inafaa na kutoa tu.
Baada ya kufikishwa na mshitakiwa, mshitakiwa namba 1, 3 na 4 waliwasilisha taarifa yao ya pamoja ya utetezi (WSD) kukana dhima na kuomba kufutwa kwa shauri hilo pamoja na gharama.

Mshitakiwa namba 2 wala wala hajajitokeza licha ya juhudi za kumlinda mahudhurio, na hivyo kusababisha Mahakama kuamuru shauri hilo kuendelea kwa sehemu
dhidi yake.

Source:

JUDGEMENT :
Hearing date8 December 2025
Court
High Court of TanzaniaCourt registry
High Court Dar es Salaam Zone Registry
Case numberCivil Case No. 28992 of 2024

Judges Mwakapeje, J.

Judgment date 19 December 2025

Language English
Summary
Whether clerical registration discrepancies defeat insurer indemnity where employer's vehicle negligently struck the applicant.

Flynote​

Road traffic accident – pedestrian struck on zebra crossing – driver convicted for dangerous driving – negligence established; vicarious liability of employer – insurer denied indemnity due to vehicle registration discrepancy; award of proven special damages, general damages and punitive damages against driver
 
Mahamana Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam imeamuru Kampuni ya UDA Rapid Transport Ltd kumlipa fidia ya Sh. milioni 88.8 Frank Zebaza, baada ya kugongwa na basi la mwendokasi, ambapo pia imebainika kuwa Dereva Hafidhi Ally alikuwa akiendesha basi hilo kwa mwendo hatarishi ambaye pia Mahakama imemuamuru kumlipa Frank fidia ya shilingi Milioni kumi.

Soma pia: Bodaboda kuvamia barabara za mwendokasi imekuwa kero, wanafanya ajali zisiishe

View attachment 3519049

Hukumu hiyo ilitolewa Desemba 19, 2025 na Jaji Griffin Mwakapeje, kufuatia kesi ya madai namba 28992 ya mwaka 2024 iliyofunguliwa na Zebaza dhidi ya UDA Rapid Transport Ltd, dereva Hafidhi Ally, Shirika la Taifa la Bima (NIC) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), akidai fidia ya jumla ya Sh. milioni 600 kwa madhara aliyopata.

Katika madai yake, Zebaza aliomba alipwe Sh. milioni 350 kama fidia maalumu kwa gharama za matibabu na matumizi mengine yanayohusiana na ajali hiyo, Sh. milioni 150 kama fidia ya jumla kwa maumivu na mateso pamoja na Sh. milioni 100 kama fidia ya adhabu.

Akisoma hukumu hiyo, Jaji Mwakapeje alisema ushahidi uliowasilishwa mahakamani unaonesha wazi kuwa mlalamikaji alipata majeraha makubwa yaliyomlazimu kufanyiwa upasuaji mkubwa na hadi sasa anaendelea kukumbwa na athari za kudumu katika mfumo wa fahamu na hisia, hali iliyosababisha kupungua kwa uwezo wake wa kufanya kazi.
hivi kwa ajali hiyo hapo mwenye kosa nani kati ya boda na mwendokasi. naona kama boda alivamia barabara ya mwendokasi.
 
Maswali ya la 4B. Mahakama ikikaza hukumu hata jengo la ofisi linashikiliwa.
eti mahakama ikikaza hukumu inashikilia jengo.. tena hapo unaongelea jengo la billion.! ingekuwa mahakama za Kenya sawa ila huku kwa machawa aahh.! mkuu amka usingizini
 
Back
Top Bottom