Boda , Bajaji na Maguta Walalama kudharauliwa Dar es salaam!

Boda , Bajaji na Maguta Walalama kudharauliwa Dar es salaam!

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2016
Posts
17,434
Reaction score
27,177
Wamiliki na waheshimiwa maafisa usafirishaji wanaotumia Bodaboda, Guta na Bajaji walalamikia dharau dhidi yao kuonekana hawawezi kulipa tozo za maegesho .

Wamesema kwa siku wanaingiza zaidi ya Elfu 50 na kiwango cha chini ni elfu 30 kwa siku , tajiri anapewa 15 na dereva anakula 30.
Kwa Bajaji za Ubungo Changanyikeni , kwa siku wanaingoiza 70 , tajiri anakula 25 na dereva anakula 55 yake.

Bajaji za Tegeta Kariakoo kwa siku wanaingiza elfu 70 , tajiri anakula 35 na dereva 35 .

Sasa , Malalamiko yao ni kutolipa kodi yeyote hasa ya parking ili kuchangia maendeleo na serikali itengeneze vijiwe vyao vizuri,

Wanasema kwamba sehemu nyingi zilizokuwa parking za kulipia za magari wamezzichukua na kupunguza mapato ya jiji , sasa wanataka walipe.

MAPENDEKEZO YA BODA BODA KWA SERIKALI:

Wanataka kwa siku nzima walipe 500 tu yaani Kila lisaa limoja Shilingi 50 tu.
Na bajaji kwa siku iwe shilingi 100, kila lisaa limoja iwe shilingi 100 tu.

Kwa mwezi itakuwa kiasi kidogo sana, walipe kwa scan , na utaratibu ni kwamba vijiwe vyote visajiliwe na wawe na pahala pa kutambulika.
 
Back
Top Bottom