Pendragon24
Member
- Aug 8, 2018
- 68
- 97
Katika kuadhimisha wiki ya nenda kwa usalama barabarani 2024.
Tuitumia wiki hii kuwalinda watu wanaotembea kwa miguu katika njia maalumu zilizotengenezwa kwa ajili ya wao kutembea kwa uhuru.
Maana wapo boda boda na baadhi ya bajaji ambao sio wastaarabu huacha njia zao na kutumia njia maalumu za watembea kwa miguu kupitisha vyombo vyao vya usafiri tena kwa spidi isiyokuwa ya kawaida.
Hali hii inapelekea watembea kwa miguu wengi sana kukosa amani wakiwa wanatembea katika njia hizo saa nyingine kugongwa na kusukumiwa njia kuu ambapo magari yanapita kwa kasi sana.
Yaani boda boda anaacha njia kuu aliyotakiwa kupita na kuja kutumia njia za watembea kwa miguu ili awahi kufikisha abiria pasipo kuangalia usalama wake, watembea kwa miguu na hata huyo abiria wake.
Tunaitaka mamlaka kushughulikia kero hii kwa haraka kwani inatishia usalama wa watembea kwa miguuu.
Wiki ya usalama barabarani...
Endesha salama
Fika salama.
Na wengine pia wabaki salama wakiwa njiani.