Bodaboda afariki Kenya baada ya kukamatwa masaa mawili na Polisi

Bodaboda afariki Kenya baada ya kukamatwa masaa mawili na Polisi

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
977
Reaction score
1,966
Utata umegubika kifo cha mwendesha bodaboda Jack Deon Maloba, mwenye umri wa miaka 23, aliyekamatwa Alhamisi jioni tarehe 11 Disemba, na kufariki akiwa katika kituo kimoja cha polisi jijini Nairobi.

Familia yake inadai kuwa polisi waliwaambia kuwa Maloba alijiua kwa kutumia fulana, lakini uchunguzi wa kifo chake umethibitisha kuwa Maloba aliuawa na kifaa chembamba zaidi ya fulana.

Mamlaka ya Kuchunguza Uwajibikaji wa Polisi imeanzisha uchunguzi kubaini chanzo cha kifo hicho. Hii sio mara ya kwanza kwa vifo vyenye utata kutokea chini ya usimamizi wa polisi.

Itakumbukwa kuwa, wasiwasi uliibuka nchini Kenya baada ya Albert Ojwang, ambae alikuwa ni mwalimu, kupatikana amefariki muda mfupi baada ya kukamatwa na polisi, hivyo kuibua hasira kali na maandamano miongoni mwa wananchi.
 
Back
Top Bottom