Zee la madawa
JF-Expert Member
- Nov 28, 2022
- 1,895
- 4,478
Muuguzi msaidizi wa Hospitali ya Mji Same, Asha Bakari (25), amefariki dunia baada ya kuchomwa kisu shingoni na mpenzi wake usiku wa katika makazi ya watumishi wa hospitali hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Same, Kasilda Mgeni, amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo yanayohusishwa na wivu wa mapenzi, ambapo mtuhumiwa ambaye ni dereva bodaboda anadaiwa kumshambulia marehemu baada ya kumvizia kwa simu kufuatia mgogoro wa kimahusiano.
Baada ya kutekeleza unyama huo, mtuhumiwa alitoroka na juhudi za vyombo vya dola kumsaka zinaendelea ili afikishwe mbele ya sheria.
DC Mgeni ametoa wito kwa jamii kutojichukulia sheria mkononi na kutatua migogoro ya mapenzi kupitia njia za amani, huku Diwani wa Kata ya Kisima, Kei Mbwambo, akilaani tukio hilo na kuahidi kuimarisha elimu ya ulinzi na usalama ili kuzuia matukio ya kikatili yasijirudie.