Bodaboda Dodoma walalamika kupateliwa mafuta kikao cha RC Mtaka

Stuka

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
282
Reaction score
906
Kuna malalamiko makubwa kutoka kwa waendesha Bodaboda na Bajaji walioshiriki kikao baina ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Antony Mtaka kuhusiana na hamasa ya sensa lakini awali wakati wanajiandisha asubuhi waliahidiwa kupewa lita 2 za mafuta.

Baada ya kumaliza mkutano baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kuondoka wale waliowatangazia kuwapa lita 2 za mafuta wakaingia mitini bila kuwapa utaratibu wowote ikiwa siku nzima waliimaliza kwenye kongamano hilo bila ya kufanya kazi na wanahitajika kupeleka matumizi majumbani kwao.

Ombi kwa MTAKA fuatilia vizuri suala hili na ukibaini ukweli chukua hatua kwa waliohusika na kashfa hii maana hao ndio wanaochafua CV yako umefanya kazi kubwa isije ikaonekana shughuli unazoandaa watu wanazitumia kuwadhulumu wanyonge.
 
Mtaka ni Kiongozi SMART sana hili naamini ataliingilia kati ili kumjua huyo aliyewazima hao bodaboda hiyo posho ya mafuta maana ni jambo baya sana Komredi Mtaka fuatilia hili suala
 
MTAKA, usihusishwe na upuuzi wa aina hiyo.

Mmebaki wachache sana mnaotazamwa kwa matumaini na mategemeo ya nchi yetu.
Kalamu ni sahihi kabisa MTAKA asiingizwe kwenye uhuni huu, ameweka rekodi nzuri ya utumishi wa umma tangu akiwa DC Mvomero na Hai kama sikosei asikubali kuingizwa kwenye huo mchezo mchafu, ni vizuri akachunguza na kuwachukulia hatua hao waliowatangazia bodaboda kuwepo mafuta lita 2 baada ya kikao na baadaye wakaondoka patupu
 
Kuna malalamiko makubwa kutoka kwa waendesha Bodaboda na Bajaji walioshiriki kikao baina ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Antony Mtaka kuhusiana na hamasa ya sensa lakini awali wakati wanajiandisha asubuhi waliahidiwa kupewa lita 2 za mafuta.

Baada ya kumaliza mkutano baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kuondoka wale waliowatangazia kuwapa lita 2 za mafuta wakaingia mitini bila kuwapa utaratibu wowote ikiwa siku nzima waliimaliza kwenye kongamano hilo bila ya kufanya kazi na wanahitajika kupeleka matumizi majumbani kwao.

Ombi kwa MTAKA fuatilia vizuri suala hili na ukibaini ukweli chukua hatua kwa waliohusika na kashfa hii maana hao ndio wanaochafua CV yako umefanya kazi kubwa isije ikaonekana shughuli unazoandaa watu wanazitumia kuwadhulumu wanyonge.
Mtoa mada tafadhari usimuhusishe huyo mkuu wa mkoa kwenye jambo hilo, sidhani kama anaweza kufanya jambo kama Hilo.

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Kwani aliyeahidi kutoa hizo Lita 2 ni nani?

Anthony naye ni binadamu mjue!
 
Back
Top Bottom