Bodaboda: Furaha za punguzo la adhabu ya makosa ya barabara imepotea?

Bodaboda: Furaha za punguzo la adhabu ya makosa ya barabara imepotea?

Chendembe

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2019
Posts
444
Reaction score
488
Tulishuhudia na kusikia shangwe za wabunge, Bodaboda na wamiliki wa pikipiki wakati bajeti inasomwa na mheshmiwa Wazili Mche.

Naomba kufahamu, hali ya sasa katika Hilo nchini kwakuwa, nimeona idadai ya pikipiki inaongezeka katika vituo vya polisi. Mbaya zaidi, nimeona askali wetu wakizisaka Hadi vichochoroni na zaidi weekend, asubuhi saana na jioni.
Nimeona pia wakitumia fuso kusafirisha pikipiki nyingi zilizo kamatwa kupeleka kituoni.

Nimeona pia vijana wakienda kwa diwani kuomba msaada kuhusu Hilo.
Nimesikia pia ni mwendo wa kuandikiwaa makosa mawili au matatu.
Nimeziona pikipiki nyingi mno katika kituo kidogo saana Cha Vikindu.
Nawaza tu labda Kuna zoezi maalum linaendelea!

Sijuwi kwakuwa ulinzi ni Siri.

Hali ikoje katika mazingira mliyopo wadau?
 
Back
Top Bottom